NENO LA LEO

155 views
Skip to first unread message

Eliezer Mwangosi

unread,
Dec 4, 2018, 10:38:53 PM12/4/18
to zaina...@yahoo.com, annie...@yahoo.com, dai...@diamondtrust.co.tz, bngan...@yahoo.com, Dorah....@tigo.co.tz, Erick...@hotmail.com, evam...@yahoo.co.uk, csend...@yahoo.com, debok...@yahoo.com, chec...@yahoo.co.uk, annas...@yahoo.com, elig...@yahoo.co.uk, apbw...@yahoo.co.uk, ester...@yahoo.com, cella...@yahoo.co.uk, deoma...@yahoo.com, ema...@serena.co.tz, emap...@yahoo.co.uk, epiphania...@yahoo.com, alfredb...@yahoo.com, bmt...@gmail.com, weddym...@gmail.com, Emmyk...@gmail.com, damar...@ymail.com, elijahc...@yahoo.com, ana...@hotmail.co.uk, emba...@yahoo.com, bar...@yahoo.com, emie...@yahoo.com, ant...@gmail.com, Aru...@grumeti.singita.com, deri...@yahoo.com, emmy...@yahoo.com, anne...@hotmail.com, cjk...@yahoo.co.uk, answ...@yahoo.co.uk, berna...@gmail.com, elyta...@yahoo.com, Dat...@scitz.com, Evel...@gmail.com, devon...@yahoo.com, ckiiz...@yahoo.com, benson...@yahoo.com, Andyni...@yahoo.com, bmas...@gmail.com, aak...@hq.bot-tz.org, yourtr...@googlegroups.com, Edesia.K...@nbctz.com, Buhatwa....@nbctz.com, ymt...@hotmail.com
Salaam,

NENO LA LEO - HATARI YA KUSHIKILIA MAPOKEO YA WANADAMU

2Thesalonike 2:11-12 "Kwa hiyo Mungu awaletea nguvu ya upotevu, wauamini uongo; ili wahukumiwe wote ambao hawakuiamini KWELI, bali walikuwa wakijifurahisha katika udhalimu."

MAPOKEO ni mafundisho ambayo mtu anayapata kutoka kwa mtu mwingine, katika mambo ya kiroho, mafundisho yote yanapaswa kuwa ni maneno kutoka kwa Mungu, hiyo ndiyo inaitwa KWELI, vinginevyo yanaitwa MAPOKEO YA WANADAMU (UONGO). 

Yesu alikemea mapokeo akisema, "Akawaambia, Isaya alitabiri vema juu yenu ninyi wanafiki, kama ilivyoandikwa, Watu hawa huniheshimu kwa midomo ila mioyo yao iko mbali nami; Nao waniabudu bure, Wakifundisha mafundisho yaliyo maagizo ya wanadamu, Ninyi mwaiacha amri ya Mungu, na kuyashika mapokeo ya wanadamu." Marko 7:6-8.

Kama kuna jambo ambalo muhimu la kufanya kwa kila anayejiita Mkristo au Mtoto wa Mungu, au Mcha Mungu, ni kuhakikisha anafanya matengenezo ya kuyaacha mafundisho yote YASIYO MAAGIZO YA MUNGU. Kuna udanganyifu mwingi wa viongozi wa dini wakiwafariji watu kwa maneno laini, huku wakidumu na mafundisho yasiyo maagizo ya Mungu, na wakidai "WEWE AMINI TU .... IMANI NI IMANI".

WITO WA KUJIPONYA NAFSI:

Kabla ya kufungwa mlango wa rehema, Mungu anatoa nafasi tena ya kufanya matengenezo, Viongozi, Manabii, Maaskofu, Wachungaji, n.k. huu ni wakati wa kuifuata kweli inayofunuliwa, na kuachana na Itikadi za Kidini na Udhehebu zilizo NJE YA NENO LA MUNGU. Watumishi wote wasio tayari kufanya matengenezo baada kuifahamu KWELI watapigwa upofu zaidi na kupotea kama Bwana alivyo mwambia nabii Isaya.

Isaya 29:13-14 "Bwana akanena, Kwa kuwa watu hawa hunikaribia na kuniheshimu kwa vinywa vyao, bali mioyo yao wamefarakana nami, na kicho chao walicho nacho kwangu ni maagizo ya wanadamu waliyofundishwa;

kwa sababu hiyo mimi nitafanya tena kazi ya ajabu kati ya watu hawa, kazi ya ajabu na mwujiza; na akili za watu wao wenye akili zitapotea, na ufahamu wa wenye busara wao utafichwa."

Usisahau maneno ya Yesu juu ya Manabii na Mitume wa Uongo, aliotabiri kutokea na kulisambaratisha kundi lake, kwa mafundisho potofu, baada ya yeye kuondoka. Hayo ndiyo matokeo ya siku hizi kuwa na Makundi ya wacha Mungu wenye mafundisho tofauti ... Huku wote wakidai WANAMWAMINI YESU. Lakini sikia Yesu anasema; wengi atawaambia; "SIKUWAJUA NINYI KAMWE, ONDOKENI KWANGU...." Mathayo 7:15-23.

Soma zaidi - Mathayo 24:24-25; 2Timotheo 4:3-4; Ufunuo 1:1-3; Ufunuo 14:6; Ufunuo 14:12; Ufunuo 12:17 .....

NAKUTAKIA SIKU NJEMA YENYE HATUA MPYA YA MATUMAINI NA BARAKA TELE

Na: Ev. Eliezer Mwangosi
Simu: 0767 210 299


Bahati Mashimba

unread,
Dec 5, 2018, 12:34:06 AM12/5/18
to Eliezer Mwangosi, zaina...@yahoo.com, annie...@yahoo.com, dai...@diamondtrust.co.tz, bngan...@yahoo.com, Dorah....@tigo.co.tz, Erick...@hotmail.com, evam...@yahoo.co.uk, csend...@yahoo.com, debok...@yahoo.com, chec...@yahoo.co.uk, annas...@yahoo.com, elig...@yahoo.co.uk, apbw...@yahoo.co.uk, ester...@yahoo.com, cella...@yahoo.co.uk, deoma...@yahoo.com, ema...@serena.co.tz, emap...@yahoo.co.uk, epiphania...@yahoo.com, alfredb...@yahoo.com, bmt...@gmail.com, weddym...@gmail.com, Emmyk...@gmail.com, damar...@ymail.com, elijahc...@yahoo.com, ana...@hotmail.co.uk, emba...@yahoo.com, bar...@yahoo.com, emie...@yahoo.com, ant...@gmail.com, Aru...@grumeti.singita.com, deri...@yahoo.com, emmy...@yahoo.com, anne...@hotmail.com, cjk...@yahoo.co.uk, answ...@yahoo.co.uk, berna...@gmail.com, elyta...@yahoo.com, Dat...@scitz.com, Evel...@gmail.com, devon...@yahoo.com, ckiiz...@yahoo.com, benson...@yahoo.com, Andyni...@yahoo.com, aak...@hq.bot-tz.org, yourtr...@googlegroups.com, Edesia.K...@nbctz.com, Buhatwa....@nbctz.com, ymt...@hotmail.com
Amina mtumishi kwa chakula kigumu cha kiroho maana watu wanapotea
njia ya kweli kwakushikilia na kuamini mafundisho na mapokeo ya
wanadamu.

Mungu akubariki sana
Reply all
Reply to author
Forward
0 new messages