eliezer.mwangosi
unread,Feb 26, 2018, 12:21:40 AM2/26/18Sign in to reply to author
Sign in to forward
You do not have permission to delete messages in this group
Either email addresses are anonymous for this group or you need the view member email addresses permission to view the original message
to aak...@hq.bot-tz.org, ester...@yahoo.com, annie...@yahoo.com, cella...@yahoo.co.uk, emie...@yahoo.com, Arusha Reception, bmas...@gmail.com, elijahc...@yahoo.com, bngan...@yahoo.com, evam...@yahoo.co.uk, devon...@yahoo.com, ckiiz...@yahoo.com, emmy...@yahoo.com, Andyni...@yahoo.com, benson...@yahoo.com, emba...@yahoo.com, damar...@ymail.com, epiphania...@yahoo.com, bmt...@gmail.com, elig...@yahoo.co.uk, Erick...@hotmail.com, Dat...@scitz.com, Buhatwa Ladislaus, berna...@gmail.com, weddym...@gmail.com, csend...@yahoo.com, Emmyk...@gmail.com, answ...@yahoo.co.uk, alfredb...@yahoo.com, annas...@yahoo.com, ana...@hotmail.co.uk, debok...@yahoo.com, emap...@yahoo.co.uk, chec...@yahoo.co.uk, dai...@diamondtrust.co.tz, yourtr...@googlegroups.com, deri...@yahoo.com, anne...@hotmail.com, deoma...@yahoo.com, ant...@gmail.com, elyta...@yahoo.com, Edesia Kahyarara, apbw...@yahoo.co.uk, Evel...@gmail.com, bar...@yahoo.com, cjk...@yahoo.co.uk, Dorah....@tigo.co.tz, zaina...@yahoo.com, ema...@serena.co.tz, ymt...@hotmail.com
NENO LA LEO: JIPATIE AMANI MOYONI
Wafilipi 4:6-7 "Msijisumbue kwa neno lo lote; bali katika kila neno kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu. Na amani ya Mungu, ipitayo akili zote, itawahifadhi mioyo yenu na nia zenu katika Kristo Yesu."
Ni asubuhi nyingine ya Jumatatu ambayo kila mtu anaamka kwenda kuwajibika, Wakulima wanaenda mashambani, wa maofisini wanakimbizana na usafiri wawahi, wafanya biashara wanawahi wateja, wanafunzi wanajiandaa kuwahi darasani, wanaobaki kwa kazi za nyumbani nao wamedamka kuhakikisha nyumba zinakuwa sehemu ya furaha.
Hata hivyo, pamoja na kila mmoja kuwa na jambo la kufanya asubuhi ya leo, bado kuna wengi wameamka wakiwa na misongo ya mawazo kutokana na changamoto za maisha wanayoyapitia, ni wazi kuna wengine hawajui siku ya leo itapitaje, kila wakitazama njia ya kupata kipato wanaona giza, wanatafuta kazi hadi soli za viatu zinapinda na bahasha za kubebea barua na vyeti zinachanika.
Kuna wengine wana kazi ila afya zimekataa, kuna wengine wana kila kitu, ila mahusiano ya ndoa, uchumba au ndugu, yamekuwa mshale urukao na kujeruhi. Wengine wamevunjwa moyo na viongozi kwa uonevu, wengine wamedhurumia na wateja wao, wengine wamezushiwa uongo n.k.
Neno la leo linatupatia mianzo mipya ya mawazo na kuamsha hisia zetu kumtazama na kumpelekea haja zetu Mungu, ambaye ameahidi kutupatia AMANI yake, isiyotikiswa na mawimbi ya masumbufu haya ya maisha. Itazame na kuianza Jumatatu ya leo kwa IMANI YA USHINDI KATIKA KRISTO YESU.
NAWATAKIA JUMATATU NJEMA .....
Na: Ev. Eliezer Mwangosi
Simu: 0767 210 299.
Sent from my Samsung Galaxy smartphone.