NENO LA LEO

586 views
Skip to first unread message

eliezer.mwangosi

unread,
Apr 5, 2016, 12:30:16 AM4/5/16
to
SIKILIZA - INJILI YA MILELE - MAZIWA YASIYOGHOSHIWA
MADA : AMRI ZA MUNGU - NI UPENDO
Tangu zamani Mungu ameyafunua mapenzi yake katika vizazi vyote, na sifa kuu ya Mapenzi ya Mungu ni Upendo, ndio maana Mungu ni Upendo. 1Yohana 4:16 "... Mungu ni Upendo... ".

AMRI za Mungu kama zilivyotolewa katika mlima Sinai ni muhtasari tu wa mapenzi ya Mungu, alioutoa kwa mkono wa Musa kuwakumbusha waisraeli baada ya kuzisahau kwa kukaa utumwani. Mapenzi ya Mugu yapo milele zote ni tabia yake, hayawezi kubadilika, tangia Adam, Ibrahim, Nuhu, Mitume hadi Kanisa la Kristo, yatadumu milele.

Yesu alisema - Mkizishika Amri zangu mtakaa katika pendo langu kama mimi nilivyozishika Amri za Baba yangu na kukaa katika pendo lake. Yohana 15:10. Amri 10 ni ufupisho, Yesu alikuja kuzifafanua zaidi na kutoa kielelezo namna ya kuziishi ikidhihirisha tabia ya Upendo kwa Mungu na Mwanadamu.

Amri za Mungu zilizoandikwa na Mungu katika Mbao za Mawe, zinapatikana katika - Kutoka 20:3-17 - Ni Jumla ya Mapenzi ya Mungu, ambazo zimegawanywa katika Amri kuu mbili kama ifuatavyo;

1. Mpende Bwana Mungu wako, Kwa moyo wako wote, na Kwa Roho yako yote, na akili zako zote. Mathayo 22:37 - [Upendo kati ya Mwanadamu na Mungu] - Ni wajibu wa Mwanadamu kwa Mungu, kwa ajili ya kumpa utukufu Mungu, kwa Jinsi anavyotaka Yeye.

AMRI YA I.
Usiwe na Miungu mingine ila mimi

AMRI YA 2.
Usijifanyie sanamu ya kuchonga, wala mfano wa kitu chochote kilicho juu mbinguni, wala kilicho chini duniani, wala kilicho majini chini ya dunia. Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi, Bwana, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu; nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao, name nwarehemu maelfu elfu wanipendao, na kuzishika Amri zangu

AMRI YA 3.
Usilitaje bure jina la BWANA, Mungu wako, maana Bwana hatamhesabia kuwa hana hatia mtu alitajaye jina lake bure

AMRI YA 4.
Ikumbuke siku ya sabato uitakase. Siku sita fanya kazi, utende mambo yako yote, lakini siku ya saba ni sabato ya BWANA, Mungu wako, siku hiyo usifanye kazi yo yote, wewe, wala mwana wako, wala binti yako, wala mtumwa wako, wala mjakazi wako, wala mnyama wako wa kufuga, wala mgeni aliye ndani ya malango yako. Maana, kwa siku sita Bwana alifanya mbingu, na nchi, na bahari, na vyote vilivyomo, akastarehe siku ya Saba; kwa hiyo BWANA akaibarikia siku ya sabato akaitakasa.

2. Mpende Jirani yako kama nafsi yako.Mathayo 22:39 - [Upendo kati ya Mwanadamu na Mwenzie] - Ni wajibu wa Mwanadamu kwa Mwanadamu mwenzake.

AMRI YA 5.
Waheshimu baba yako na mama yako; siku zako zipate kuwa nyingi katika nchi upewayo na BWANA, Mungu wako.

AMRI YA 6.
Usiue

AMRI YA 7.
Usizini

AMRI YA 8.
Usiibe

AMRI YA 9.
Usimshuhudie jirani yako uongo

AMRI YA 10.
Usitamani nyumba ya jirani yako, usitamani mke wa jirani yako, wala mtumwa wake, wala mjakazi wake, wala ng’ombe wake, wala punda wake, wala chochote alicho nacho jirani yako.

Shida kubwa kwa waisraeli na hata kizazi chetu ni hizi;
1. Walitegemea nguvu zao kuzishika, jambo ambalo haliwezekani, ni kwa Roho mtakatifu kutawala maisha yetu, ambaye anatupatia tabia ya Mungu ndani yetu na kutufanya tuishi sawa na Amri zake.

2. Kutegemea kupata HAKI kwa kuzishika au Kuzitenda, Haki tunaipata kwa neema kwa njia ya Imani Kwa Yesu Kristo, Matendo ya Utii ni matokeo ya kuokolewa katika Tabia ya Uasi wa Mapenzi ya Mungu.

3. Kuchanganya Mapenzi ya Mungu na Mapokeo ya Imani za Mababa au Mapokeo nje ya neno la Mungu. Wakazifanya Amri hizo kuwa mzigo badala ya kuwa Baraka kwa Ulimwengu, ulimwengu ukajaa laana kama ambavyo kizazi chetu kinatatarika na kubeza mapenzi ya Mungu, na hatimaye kuwasha hasira ya Mungu.

4. Kukosa ufahamu wa maana halisi ya Amri hizo.... mfano. Usizini.... Walijawa na Tamaa za Zinaa, japo waliogopa kuuwawa kwa mawe endapo wangezini, hivyo waliasi kwa Zinaa iliyokuwa ndani ya mioyo yao. Walikuwa wenye Chuki, Hasira, Visasi, nk. Waliikosa Nuru halisi ya kuwaangazia tabia na mapenzi ya Mungu.

HATA HIVYO KUNA SHERIA ZILISHOISHIA MSALABANI AMBAZO ZILIKUWA KIVULI CHA KUTULETA KWA KRISTO - NITAZIFUNDISHA KATIKA SOMO LINGINE.

By. Ev. Eliezer Mwangosi - 0767210299.




Sent from Samsung tablet

bmashimba

unread,
Apr 5, 2016, 4:40:09 AM4/5/16
to YourTrueVine

Amen

---------- Forwarded message ----------From: "eliezer.mwangosi" <eliezer....@yahoo.com>Date: Apr 5, 2016 7:30 AMSubject: NENO LA LEOTo:
Cc:

eliezer.mwangosi

unread,
Apr 7, 2016, 12:56:53 AM4/7/16
to
NENO LA LEO - USIFADHAIKE BADO KUNA TUMAINI

Isaya 54:4 "Usiogope; maana hutatahayarika; wala usifadhaike; maana hutaaibishwa; kwa kuwa utaisahau aibu ya ujana wako, pia mashutumu ya ujane wako hutayakumbuka tena". 

Katika ulimwengu huu wa dhambi, mwanadamu anapitia changamoto mbalimbali, ambazo wakati mwingine zinaleta kukosa matumaini na kuvunjika moyo.

Ninaamini hata siku hii ya leo, kuna mtu fulani anapitia changamoto ambayo imedumu kwa mda mrefu bila kupata ufumbuzi.

Bila kujali umejeruhiwa kiasi gani, bila kujali tatizo limedumu muda mrefu kiasi gani, bila kujali uzito wa tatizo lako, hata kama huoni mwisho wa shida yako. Hata ujione umeaibika na watu wanakubeza na dhihaka juu.

Neno la leo linasema, siku yaja, tena iko mbele yako, ambayo HUTAYAKUMBUKA mapito haya na changamoto zake. Kuna wengi wanashuhudia jinsi Bwana alivyowapitisha katika dhiki fulani, huenda hata wewe una ushuhuda ukiyakumbuka ya zamani.

Ni kazi ya shetani, kuvunja moyo na kutia Giza akili ili tusione Nuru kupitia ahadi za Mungu wetu. Hebu tumtazame Yesu aliye mwokozi wetu, kudumu kumpatia fadhaa zetu, naye ni mwaminifu, atatenda.

NAWATAKIA SIKU NJEMA YENYE BARAKA TELE NA AMANI MOYONI.

By. Eliezer Mwangosi
Simu: 0767210399.




Sent from Samsung tablet

bmashimba

unread,
Apr 7, 2016, 4:44:48 AM4/7/16
to eliezer. mwangosi, YourTrueVine, Mgedzi Deborah

Amina. Ubarikiwe na Bwana

Safari Daudi Buganda

unread,
Apr 7, 2016, 9:24:27 AM4/7/16
to yourtr...@googlegroups.com
Ubarikiwe mtumishi habari za Congo?

Sent from my Windows Phone


Sent from Samsung tablet

______________________________________________________________________
This email has been scanned by the Symantec Email Security.cloud service.
For more information please visit http://www.symanteccloud.com
______________________________________________________________________

--
Mimi ni mzabibu ninyi ni matawi, akaaye ndani yangu nami ndani yake, huyo huzaa sana; maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya neno lolote.Yohana 15:5
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "YourTrueVine" group.
To post to this group, send email to yourtr...@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

CONFIDENTIAL NOTE:
The information in this E-mail and any attachments transmitted are originated by SABMiller or any of its subsidiaries companies, is intended to be privileged and/or confidential and only for use of the individual, entity or company to whom it is addressed. If you have received this e-mail in error please destroy it and contact the sender. If you are not the addressee you may not disclose, copy, distribute or take any action based on the contents hereof. Any total o partial unauthorized retention, dissemination, distribution or copying of this message is strictly prohibited and sanctioned by law

eliezer.mwangosi

unread,
Apr 7, 2016, 11:58:52 PM4/7/16
to
NENO LA LEO - PENDO LISIWE NA UNAFIKI

Warumi 12:9 "Pendo na lisiwe na Unafiki; lichukieni lililo ovu,  mkiambatana na lililo jema".

Kama kuna changamoto kubwa katika kizazi chetu ni kuupata Upendo wa kweli. Vijana Kwa wazee na wanaume kwa wanawake, asilimia kubwa wanajeruhiwa kwa Upendo wenye Hila na Unafiki ndani yake.

Mabinti na hata akina mama wengi, wamepitia majeraha na kuumizwa na wapendwa waliojifanya wanawapenda, kumbe lilikuwa ni Pendo la Kinafiki na hila. Lakini pia ndivyo ilivyo kwa Wavulana, wengine wamejikatia tamaa hawataki kusikia Mahusiano Kwa jinsi walivyoporwa wapenzi wao na wenye nazo.

Bahati mbaya Sana, hata wanaojiita watoto wa Mungu wanapitia, majeraha haya ya Upendo Feki. Wengi wamejikatia tamaa ya Kuolewa na Kuoa, na wengine wako kwenye ndoa zilizogeuka Ndoano, ni vilio na adha zisizokoma.

Kizazi chetu kwa ujumla kinazidi kupoteza Upendo wa Kweli, kwa sababu KUMCHA MUNGU kunazidi kupotea, wengi wanamrudia Mungu wakiwa tayari ni Majeruhi.

Mtume Paulo, anatoa onyo kwa watoto wa Mungu, wasiotulia na kuhemea kwa Pendo la Unafiki wenye Kujeruhi dhamiri za wenzao, sawa na wakorintho walivyotendeana.

1 Wakorintho:8:12 "Hivyo, mkiwatenda dhambi ndugu zenu na kuitia jeraha dhamiri iliyo dhaifu, mnamtenda dhambi Kristo".

Ukimkosea mwenzio kwa jambo lolote, unamtenda dhambi Kristo, mwisho wake ni kilio cha kusaga meno. Ni wakati wa kumrudia Mungu wetu, atuepushe na mitego, ili tusinaswe na tusiwe na Upendo wenye Unafiki na Hila.

MUNGU NA AWAPATIE NEEMA YA KUISHI MAISHA YENYE FURAHA NA AMANI.

NAWATAKIA SIKU NJEMA YENYE BARAKA TELE.

Na. Ev. Eliezer Mwangosi
Simu: 0767 210 299.




Sent from Samsung tablet

eliezer.mwangosi

unread,
Apr 11, 2016, 11:35:21 PM4/11/16
to
NENO LA LEO - MSHALE ULIOWAJERUHI WENGI

1 Wakorintho 6:18 "Ikimbieni ZINAA. Kila dhambi aitendayo mwanadamu ni nje ya mwili wake; ila yeye afanyaye zinaa hutenda dhambi juu ya mwili wake mwenyewe".

Kati ya mishale yenye sumu anayotumia mkuu wa Giza "aka" Shetani kujeruhi na kuua wengi ni ZINAA na UASHERATI. Hili limekuwa janga la kimataifa, bila kujali una Dini au Laa.

Ndoa nyingi zimejeruhiwa na zingine kusambaratika, bila kusahau uchumba kuvunjika huku wengi wakiishia kuumia na kuvunjika moyo, kwa sababu tu ya mmoja kati yao kuhemea mapenzi nje ya fungate yao.

Wengi wametengwa na Uso wa Bwana kwa kunaswa na mtego huu wenye sumu, unaopofusha macho na masikio ya Kiroho. Waimbaji na hata wahubiri wa Injili wanaweza kuimba "Usizini", "Acha dhambi", "Tumeokolewa", "Tuko ndani ya Yesu " n.k. Huku ni wazinifu ingawa ni kwa siri, hao wote ni Marehemu wanaotembea.

NENO la leo linasema IKIMBIENI ZINAA, Wengi wamejikuta wamejeruhiwa bila kutarajia kwa sababu ya kuruhusu mjadala na Shetani, zinaa inakimbiwa, haijadiliwi. Mazingira yoyote ya faragha mfano; chumbani, kwa watu wawili walio jinsia tofauti ni hatari, Wengi ni mashahidi, na wengi yamewakuta.

Wito: Ni wakati wa kuvaa SILAHA zote za Mungu kwa njia ya Roho mtakatifu. Ni nani Yusufu wa leo? Kwa nini usiwe wewe?. Wapendwa msidanganyike hakuna faida kwenye maisha ya Dhambi, ni HASARA TU NA VILIO NA MWISHO KUDHARAULIWA.

MUNGU WA AMANI ATAWALE MAISHA YENU NA KUWAPATIA BARAKA TELE.

Na. Ev. Eliezer Mwangosi
Simu: 0767 210 299




Sent from Samsung tablet

bmashimba

unread,
Apr 12, 2016, 1:40:46 AM4/12/16
to eliezer. mwangosi, YourTrueVine, Mgedzi Deborah

Amina. Ubarikiwe na Bwana

Happines Francis

unread,
Apr 13, 2016, 6:50:19 AM4/13/16
to yourtr...@googlegroups.com

Ubarikiwe sana Kwa somo zuri na lisilohubiriwa na wengi  Kwa kuwa shetani amewanasa wengi hapa na wanashindwa kuhubiri kwani nao wamenaswa.

--

eliezer.mwangosi

unread,
Apr 13, 2016, 10:31:14 PM4/13/16
to
NENO LA LEO - MAJIBU KWA MASHAKA YAKO

Yohana15:5 "Mimi ni mzabibu; ninyi ni matawi, akaaye ndani yangu nami ndani yake, huyo huzaa sana; maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya neno lo lote".

Ni jambo la kawaida siku hizi kusikia watu wakisema "Katika kizazi chetu hakuna awezaye kushinda Dhambi", jambo la kusikitisha sana, ni pale unapouasikia maneno kama hayo katika midomo ya wacha Mungu.

Wengi wanakata tamaa katika safari ya wokovu, wanapoona watu maarufu katika Imani wakianguka katika Dhambi. Kugombania madaraka, chuki, kitosamehe, ubinafsi, hasira na Visasi, Uzinifu, Uongo, Umbea, udanganyifu, Wizi, masengenyo, mawazo machafu n.k. huonekana katikati ya watoto wa Mungu na hata kwa Viongozi wa Kiroho.

Kuna makelele ya Shetani, yamejaa kwenye fahamu za watu yakisema, "Huwezi Kushinda DHAMBI", yakisonda vidole walioshindwa, hivyo wengi wanaizoea Dhambi na kuwa sehemu ya maisha, bila hofu ya Mungu.

Yesu Kristo aliliona tatizo hili pia kwa wanafunzi wake, ndipo akasema ... "Pasipo Mimi Ninyi hamuwezi kufanya neno lolote".

Haijalishi umenasa katika matope ya dhambi kwa muda mrefu kiasi gani, Yesu yupo kwa ajili yako, ni Kweli dhambi hiyo imekushinda, Yesu alikuja kuwasaidia walioonewa na Kushindwa, ili awaokoe kabisa na kuwaweka HURU. Hii ni FURSA yako, usikubali kubaki kifungoni, fanya uamuzi, mruhusu Yesu atawale maisha yako, ATAKUSHINDIA.

NAWATAKIA SIKU NJEMA YENYE MAFANIKIO NA BARAKA TELE

Na: Ev. Eliezer Mwangosi.
Simu: 0767 210 299




Sent from Samsung tablet

Bahati Mashimba

unread,
Apr 14, 2016, 12:51:33 PM4/14/16
to yourtr...@googlegroups.com

eliezer.mwangosi

unread,
Apr 17, 2016, 5:13:37 PM4/17/16
to
NENO LA LEO - CHUKUA TAHADHARI KABLA YA HATARI

Waefeso 6:13 "Kwa sababu hiyo twaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kushindana siku ya uovu, na mkiisha kuyatimiza yote, kusimama".

Ni kawaida kuona wakati wote vikosi vya Jeshi la ulizi vikifanya mazoezi ya kivita, bila kujali kutatokea vita au laa. Muda wote vikosi vinapangwa, silaha na magari ya vita, vinawekwa tayari. Muda wote mipaka inalindwa na maskari wakiwa na silaha tayari kwa vita.

Kama ilivyo maandalizi katika vikosi vya jeshi la ulizi, ndivyo inavyotakiwa katika ulinzi wa mambo ya Kiroho. Kwa bahati mbaya sana, asilimia kubwa ya watu wanakimbilia kuvaa Silaha wakiwa tayari wamejeruhiwa, na wengi wanapoteza maisha bila matumaini.

Rafiki unayesoma ujumbe huu; ni kawaida kumkuta mtu anafunga, anaomba na hata kukesha, akiwa tayari katika mawimbi au dhoruba ya maisha, na wakati mwingine kumlaumu Mungu kuwa hajibu maombi. Neno la leo linatukumbusha kuvaa silaha wakati hali ni shwari.

Kumbuka kila dhambi anayoitenda binadamu, hata iwe tamu kiasi gani, bila kujali anaifaidi kwa muda mrefu kiasi gani, hilo BOMU ambalo adui amelitega, muda usiodhani litalipuka tu, na mwisho ni uchungu na kujijutia nafsi. Wengi waliorubuniwa wananielewa ninachokiongea.

Wito: Kwa walio ndani ya wokovu, simameni imara bado tuko vitani, kwa wale walio katika mashimo ya Dhambi, ni wakati wa kusema - Basi; yatosha siku za uovu, na kumkimbilia Kristo kabla ya Hatari.

NAWATAKIA SIKU NJEMA YENYE KUJAA BARAKA ZA BWANA.

Na. Ev. Eliezer Mwangosi
Simu: 0767 210 299.




Sent from Samsung tablet

eliezer.mwangosi

unread,
Apr 24, 2016, 3:41:49 AM4/24/16
to
NENO LA LEO: USIWAZE KURUDI MISRI - BWANA AMESIKIA KILIO CHAKO. 

Hesabu 11:18 "Kisha uwaambie watu hawa, Jitakaseni nafsi zenu kabla ya Kesho, nanyi mtakula nyama; kwa maana mmelia masikioni mwa BWANA, mkisema, ni nani atakayetupatia nyama, tule? maana huko misri tulikuwa na uheri. Basi kwa sababu hiyo Bwana atawapa nyama, nanyi mtakula".

Kuna wengi wanarudi misri ya kiroho, japo kwa nje wanaonekana ni wasafiri waaminifu wanaoelekea kanani. Wakiwa safarini wanakumbuka, starehe zinazokidhi tamaa za mwili, wanapozirudia japo kwa siri, ndivyo macho ya kiroho yanavyozidi kupofuka na kuingia katika giza, lenye kuleta majuto zaidi, na kuendelea kukosa baraka za Bwana.

Waisraeli walipotolewa utumwani Misri, wakiwa safarini, walikuwa wanapewa MANA, chakula bora, kilichokuwa kinakidhi mahitaji yote kiafya, kikitengenezwa na Mungu mwenyewe. Kwa kuwa walikuwa watu wa mwilini, hawakuweza kutambua uthamani na Ubora wa kile chakula. Wakaanza kulalamika na kutamani kurudi Misri ili kukidhi tamaa mwili juu ya chakula cha nyama. 

Mungu alisikia kilio chao, na kuamua kuingilia kati kuwapatia nyama, lakini alihitaji mioyo yao Kwanza  itiwe ufahamu wa kujua Upendo na Wema wa Mungu, ndio maana aliwaambia "JITAKASENI NAFSI ZENU". Kitendo cha kutaka kurudi misri kwa tamaa zao kilionyesha dharau juu ya Mungu, na kilimuudhi Bwana, japo aliwapatia nyama kwa kuwaletea kware, hawakufaidi ile nyama. Wale wote waliodumu kuutazama mwili na kufurahia kupata NYAMA walipigwa na kufa wakiwa na nyama midomoni mwao. Hesabu 11:33.

Mpendwa! Inawezekana unawaza kurudia au tayari umeyarudia yale uliyokiri kuyaacha siku ulipokata shauri kuwa upande wa Bwana, tafakari juu ya MANENO, MATENDO na MAWAZO yako je; ni kweli yanapatana na Kristo? Je ni changamoto gani inakufanya URUDI MISRI na kumuacha Bwana wako kwa kufanya dhambi za Siri au za uwazi? 

NENO LA LEO linasema; Jitakase, kwa maana Bwana amesikia kilio chako, yuko tayari kutupatia macho ya kuona na kupokea Baraka zake daima, na kuweza kuona hasara ya kurudi Misri kwa kukidhi matakwa na tamaa za mwili. Kuna faida kubwa kubaki hemani mwa Bwana tukiwa TUMETAKASWA.

MUNGU BABA AWAJAZIE KILA NAMNA YA BARAKA SAWASAWA NA AHADI ZAKE

Na: Ev. Eliezer Mwangosi
Simu: 0767 210 - Kwa wanaohitaji ushauri na maombi. 




Sent from Samsung tablet

Bahati Mashimba

unread,
Apr 28, 2016, 11:01:02 PM4/28/16
to yourtr...@googlegroups.com
Amen.Mtumishi wa Bwana ubarikiwe

eliezer.mwangosi

unread,
May 2, 2016, 5:49:38 PM5/2/16
to
NENO LA LEO - YEYE ANAWEZA ZAIDI YA HAYO
Waefeso 3:20 "Basi atukuzwe yeye awezaye kufanya mambo ya ajabu mno kuliko yote tuyaombayo au tuyawazayo, kwa kadiri ya nguvu itendayo kazi ndani yetu."

Nakumbuka kisa cha kijana mmoja ambaye alipitia changamoto za maisha, akiwa ni msomi alyemaliza na kufaulu vizuri masomo ya chuo kikuu, lakini kwa bahati mbaya alikosa ajira. Zaidi ya miaka mitatu aliishi kwa kuomba misaada kwa watu huku akitegemea siku moja angepata kazi. 

Katika hali ya kusikitisha, baada ya muda fulani kupita, alionekana hali imebadilika, anaongea peke yake barabarani na hakuwa na uwezo tena wa kiakili. Alipofanyiwa uchunguzi alionekana akili zimevurugika, kutokana na msongo wa mawazo. Mwisho ilibidi arudishwe kwao kijijini na ikawa ndio Mwisho wa ndoto za maisha yake. 

Wewe na mimi tungali tunaishi hapa duniani, hatujawa salama kukutwa na hali kama hiyo, kutokana na sababu nyingine yoyote, tusipokuwa na elimu hii ya neno la Mungu. Tunashuhudia kila siku, vijana kwa wazee wakianza ulevi wa pombe au madawa, wengine tabia za kutoka nje ya ndoa au kusaliti wapenzi, ili kupoteza au kupunguza msongo wa mawazo. Mpendwa; Unawaza jambo gani kubwa? Ombi lako kuu la kila siku ni lipi?, kwake yote yanawezekana na zaidi.

Tunashuhudia watu wengi na hata wanaojiita watu wa Mungu, wakienda kwa waganga wa kienyeji japo kwa siri, kutafuta dawa za kutatua shida zao, na wengine ni kuhama kanisa hadi kanisa, nabii hadi nabii na mwisho wa yote anaambulia kufadhaika na kuvunjika moyo, japo wakati mwingine unaweza kujiona umefanikiwa kumbe mwisho wake ni majanga. 

Neno la leo; linatuongoza kuona ufunbuzi wa changamoto zetu kupitia uweza wa Mungu. Lolote uliwazalo, bila kujali ni kubwa kiasi gani, na umeliombea kwa muda mrefu kiasi gani bila mafanikio, neno linasema; Mungu ANAWEZA KUFANYA ZAIDI YA HAYO. Tatizo kubwa ni mahusiano yetu na Mungu, wengi wanahitaji na kutamani Mungu awapatie mahitaji ya Mwili, lakini ndani ya mioyo yao hawako tayari kusalimisha maisha yao yatawaliwe na Mungu. HILO NI TATIZO KUBWA.

Mpendwa; neno linasema, yote na Zaidi yanawezekana ... "Kwa kadiri ya NGUVU itendayo kazi ndani yenu", siri kubwa ya mafanikio ni kuwa chini ya Uongozi wa Roho mtakatifu ambaye anaweza kukuvusha salama katika kila Dhoruba. Kutegemea akili zetu, waganga au mafundi,  kutafuta sehemu ya kupoteza mawazo n.k, ni kujilisha upepo. Hata Manabii, wachungaji, mitume, wainjilisti nk, hatupaswi kuwatumainia, kila mtu binasi anapaswa kuishi katika nguvu na uweza wa Mungu kwa njia ya Roho Mtakatifu.

MUNGU BABA AWAJALIE WOTE NEEMA INAYOWEZA KUBADILI MAGUMU KUWA RAHISI NA ZAIDI YA MAHITAJI YENU.

NB: Usikose kusoma MADA za INJILI YA MILELE zinazoendelea kutolewa kwa ajili ya wito mkuu wa matengenezo kwa watoto wa Mungu kabla ya mlago wa Rehema kufungwa.

Na. Ev. Eliezer Mwangosi.
Namba ya Simu: 0767 210 299 - Kwa ajili ya ushauri na maswali.




Sent from Samsung tablet

eliezer.mwangosi

unread,
May 10, 2016, 11:17:27 PM5/10/16
to
NENO LA LEO: WIMBO WA BWANA UGENINI

Zaburi 137:3-4 "Maana huko waliotuchukua mateka Walitaka tuwaimbie; Na waliotuonea walitaka furaha; Tuimbieni baadhi ya nyimbo za Sayuni. Tuuimbeje wimbo wa Bwana Katika nchi ya ugeni?".

Mara nyingi waisraeli walipokuwa wanachukuliwa mateka, walikuwa wanaombwa kuimba nyimbo walizokuwa wakiziimba walipokuwa kwao katika Ibada za Mungu wao. 

Walitaka wawaimbie kwa ajili ya dhihaka, juu ya Yehova, katikati ya sherehe za Miungu yao. Izraeli walitundika vinubi vyao na kuhoji - Tuimbeje wimbo wa Bwana katika nchi ya Ugeni? .

Nakumbuka kisa kilichotokea kwa wainbaji waliokuwa katika huduma ya Injili, jioni walipomaliza kuimba, mwalimu wa kwaya na mwimbaji wa kike kinara wa sauti ya kwanza, walitoroka wenzao na kwenda guest house kwa ajili kujipa maraha. 

Kabla ya yote wakiwa chumbani,  mwalimu akaomba aimbiwe wimbo akiwa amempakata, kwani alijisikia raha akisikia sauti ya binti ikiimba. Alipoanza kuimba, kabla hajamaliza mstari, akadondoka chini huku damu ya hedhi ikibubujika mithili ya bomba la maji. 

Ikawa ndio mwisho wa starehe, binti akakata roho, mwalimu wa kwaya akashikwa na kuwekwa ndani kuisaidia polisi, huku huduma ya Injili ikiwasubiri pasipo mafanikio - zikatimia za mwizi arobaini. 

Kuna vijana wengi wa kike na wa kiume na hata wazee, wanamdhihaki Mungu, wanaimba nyimbo za kumtukuza Mungu, huku wakivinjali na mahusiano ya mapenzi. Kuna baadhi ya wanakwaya, mashemasi, wachungaji, wazee, wainjilisti, manabii na mitume, ambao wako katika utumwa wa Zinaa na Uasherati.

Kila anayejiita mtumishi wa Mungu; akifanya dhambi kusudi, ni sawa na kuimba wimbo wa Bwana katika nchi ya Ugeni, kwa ajili ya shetani na mizimu kumdhihaki Yehova. Soma: Waebrania 6:4-6, 10:26-27. Kutenda dhambi kwa Mkristo ni Kumsulubisha na Kumfedhehi kwa dhahiri. 

Wakati shetani akizidi kushangilia, kwa kuwa na waimbaji wengi, wakiwa upande wake wakiimba nyimbo ugenini, bila hata kujali; wito unatolewa tena, wa Kurudi nyumbani. TOKENI KWAKE ENYI WATOTO WA MUNGU, Kabla ya siku ya kisasi cha BWANA. Huu ni wakati wa Kusema Bye Bye shetani, kwa Jina ya Yesu.

NAWATAKIA SIKU NJEMA YENYE MAFANIKIO TELE. 

Na Ev. Eliezer Mwangosi

Simu no. 0767 210 299.



Sent from Samsung tablet

Bahati Mashimba

unread,
May 11, 2016, 2:32:51 AM5/11/16
to yourtr...@googlegroups.com

Amina mtumishi katika shamba la Bwana

eliezer.mwangosi

unread,
May 15, 2016, 7:05:10 AM5/15/16
to
SIKILIZA: INJILI YA MILELE - MAZIWA YASIYO GHOSHIWA

MADA: UHUSIANO KATI YA NEEMA YA KRISTO NA SHERIA - 3

Karibuni katika mfululizo wa Mada hii ya Uhusiano kati ya NEEMA na SHERIA. Somo hili ni la 3, ni imani yangu kuwa, ulishasoma na kutafakari somo la 1 na la 2, kama bado jitahidi kuyasoma masomo hayo kabla ya kuanza kujifunza somo hili.

Zingatia: Katika somo hili, tunajifunza juu ya NEEMA na Sheria za Maadili (Amri za Mungu) zinzoonyesha Dhambi. Tofauti na zile zilizokuwa kivuli cha Kristo na kukamilishwa au kuishia pale msalabani.

MAANA YA NEEMA.
Mtume Paulo anasema: Waefeso 2:8-9 "Kwa maana mmeokolewa kwa NEEMA, kwa njia ya IMANI; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni KIPAWA cha Mungu; wala si kwa MATENDO, mtu awaye yote asije akajisifu". Hapa tunaona NEEMA ni kipawa cha Mungu, au Zawadi ya wokovu tunayopewa bure bila kulipa chochote. Tunapewa tusichostahili, wala hakuna matendo yoyote tunayopaswa kutenda ili tupewe.

NEEMA Ndiyo asili ya pekee ya watu kupewa HAKI ya kuwa watoto wa Mungu kwa Imani. Warumi 3:23-24 "Kwa sababu wote wamefanya Dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu; wanahesabiwa HAKI bure kwa NEEMA yake...". Kama ndivyo; AMRI au Sheria zina Kazi gani? Kuna haja gani ya kuzitii? 

Tafakari mfano huu:
Kulikuwa na mtu aliyekuwa anaendesha Gari kwa Kasi zaidi ya mwendo ulioonyeshwa kwenye kibao cha alama za barabarani, mbele yake kukawa na mataa (traffic light). Kwa sababu ya mwendo kasi alijikuta amepita mataa yakiwa na rangi nyekundu (RED). Mara baada ya kupita mataa akasimamishwa na Askari, na kupewa adhabu ya kulipa faini ya Sh. 60,000. Kwa makosa mawili, mwendo kasi na kupita mataa na rangi nyekundu.

Bahati mbaya alikuwa hana pesa, akiwa anasubiri kupelekwa kituoa cha polisi kwa ajili ya mashitaka, akatokea mtu mmoja anayemfahamu, akamuonea huruma, na kumlipia faini aliyokuwa anadaiwa. Hatimaye akaachiwa huru na kuendelea na safari yake. Kuanzia pale, katika safari yake yote, aliendelea kukumbuka upendo wa Rafiki yake, na akasukumwa moyoni kuwa mtiifu na mwangalifu kwa Sheria zote za Barabarani, na hakushikwa tena hadi alipofika safari yake.

FIKIRIA: Huyu dereva angerudia kosa la kutojali Sheria za barabarani, angekamatwa tena, na angeonekana Mpuuzi asiye na Akili. Hivyo ndivyo ilivyo Uhusiano kati ya Neema na Sheria. Na NEEMA ya Mungu ni zaidi ya msaada uliotolewa kwenye kisa hicho.

Neema ya Mungu kupitia kafara ya Kristo inafanya mambo makuu matatu yafuatayo:
1. Inatoa msamaha wa Adhabu ya Mauti bure kwa mdhambi, kupitia Mauti ya Kristo msalabani. Kwa sababu mshahara wa dhambi ni mauti. Tukiwa tungali tuna kesi ya kufanya Dhambi, tukingojea adhabu, Yesu Kristo, alijitokeza kutulipia Deni la Dhambi, Wakolosai 2:14. Sasa tuko huru, tunaendelea nasafari.

2. Inatupatanisha na Mungu, na kutupatia HAKI ya kuwa watoto wa Mungu. Kwa dhambi zetu hatukustahili kuitwa watoto wa Mungu wenye kupokea Baraka zake katika ulimwengu huu wa sasa na katika ulimwengu ujao. Katika mwili tulikuwa maadui wa Mungu kwa kutotii Sheria zake - Warumi 8:7.

3. Inatupatia UWEZO wa kutii SHERIA za Mungu kwa njia ya Roho mtakatifu, ambaye huziandika katika mioyo yetu, na kutufanya tuishi maisha matakatifu kwa Imani. Tunatiwa mhuri wa tabia ya Mungu kwa njia ya Roho mtakatifu. Waebrania 10:16 "Hili ni AGANO nitakaloagana nao baada ya siku zile, anena Bwana, nitatia Sheria zangu mioyoni mwao, Na katika nia zao nitaziandika". Tunadumu kusafiri Salaama, bila kunaswa na Traffic, kwa sababu Roho matakatifu ametupatia Utii kuwa tabia.

HITIMISHO:
Kamwe mwanadamu hawezi kuhesabiwa haki kwa matendo ya Sheria. Wagalatia 2:16 "Hali tukijua ya kuwa mwanadamu hahesabiwi HAKI kwa kwa matendo ya Sheria, bali kwa Imani ya Kristo Yesu; sisi tulimwamini Kristo Yesu ili tuhesabiwe haki kwa Imani ya Kristo, wala kwa matendo ya sheria hakuna mwenye mwili atakayehesabiwa haki". Leo kuna wengi watapotea kwa kutegemea matendo yao mema, yasiyo matokeo ya kubadirishwa na kuongozwa na Roho mtakatifu, na wengine wanakataa na kupinga WOKOVU katika Kristo, Watapotea bila matumaini.

Walio na Imani ya kweli katika Yesu Kristo, wanakuwa chini ya uongozi wa Roho mtakatifu, hao ndio waabuduo halisi, wamwabuduo Mungu katika Roho na Kweli. Hawa wanatembea katika utii wa Amri za Mungu kama Yesu Kristo alivyotii (Hawatendi Dhambi au UASI) - Yesu anasema; Yohana 15:10 "Mkizishika Amri zangu mtakaa katika pendo langu, kama mimi nilivyozishika Amri za Baba yangu na kukaa katika pendo lake". Yakobo anasema "...Imani pasipo MATENDO imekufa" Yakobo 2:26.

Wale wote, wanaodai wako chini ya Neema, wakidai wako huru na Sheria, na kutotaka hata kusikia Sheria ya Mungu, watapotea milele. Kuchukia Amri za Mungu ni tabia ya yule Adui Joka kwa Kanisa la Kristo - Ufunuo 12:17 "Joka akamkasirikia yule mwanamke (Kanisa), akaenda zake afanye vita juu ya wazao wake waliosalia, wazishikao Amri za Mungu, na kuwa na Ushuhuda wa Yesu.....". Shetani, amelitumia somo hili la Neema na Sheria kuwapofusha wengi, wasiopenda kuisikia kweli ya Mungu na kuzigeukia hadithi za Uongo. Tunaishi nyakati mbaya zilizotabiriwa za Ukengeufu mkuu - heri wewe usomaye ujumbe huu na kuufanyia kazi. 2Timotheo 4:3-4, 2Petro 3:14-18.

Mungu awabariki wote, mnapoendelea kutafakari ujumbe huu wa Injili ya Milele, yenye wito wa Kumcha Mungu katika kizazi hiki kilichojaa uovu, na mioyo mikaidi isiyotaka kumtii Mungu. Usikose somo la 4, linalohusu kukamilishwa kwa Upendo wa Mungu kupitia NEEMA.

Na: Ev. Eliezer Mwangosi
Simu: 0767 210 299 - Email: eliezer....@yahoo.com.




Sent from Samsung tablet

eliezer.mwangosi

unread,
May 24, 2016, 12:18:30 PM5/24/16
to
SIKILIZA - INJILI YA MILELE - MAZIWA YASIYOGHOSHIWA
MADA : KUKAMILISHWA KATIKA PENDO KWA NEEMA YAKE - 4

Karibuni wote katika mfululizo wa masomo haya ya Injili ya Milele, yenye ujumbe wa marejeo unaowaongoza watoto wa Mungu kuukulia wokovu, na kuwatoa katika ukengeufu wa neno la Mungu, unaotokana na Injili za Kisasa kupitia walimu wasiomtii Mungu kama Yesu na mitume walivyotabiri - 2Timoyheo 4:2-4, Mathayo 7:21-23. Wengi watatimiza unabii huu bila kujua, kwa sababu ya hila za adui, katika kizazi hiki cha mwisho. Kila kunapokucha tunashuhudia Giza likiendelea kufunika kabila za watu, ucha Mungu unazidi kupotea.

Injili ya milele inafunua siri ya tabia ya Mungu ya Upendo kwa maana Mungu ni UPENDO - 1Yohana 4:16 "Nasi tumelifahamu PENDO alilo nalo Mungu kwetu sisi, na kuliamini. Mungu ni UPENDO, naye akaaye katika pendo, hukaa ndani ya Mungu, na Mungu hukaa ndani yake". Na kwamba, ni mapenzi ya Mungu tabia yake iwe ndio tabia yetu, na hilo limetimilika kwa NEEMA yake kupitia mwana wake Yesu Kristo kuja kutufia msalabani.

Yohana anasema "Katika hili pendo la Mungu lilionekana, kwamba Mungu amemtuma Mwanawe pekee ulimwenguni, ili tupate UZIMA kwa yeye. Hili ndilo pendo, si kwamba sisi tulimpenda Mungu, bali kwamba yeye alitupenda sisi, akamtuma mwanae kuwa kipatanisho kwa Dhambi zetu" 1Yohana 4:9-10. Hili linawezekana tu kwa Imani juu ya Neema hii ya Mungu, ambayo hutupatia Mungu kuwa ndani yetu kwa njia ya Roho mtakatifu. 1Yohana 4:13.

Biblia nzima kutoka kitabu cha Mwanzo hadi Ufunuo, inafunua UPENDO wa Mungu kwa Mwanadamu na Uasi juu ya tabia ya Mungu ya Upendo. Na njia pekee aliyoiweka Mungu ya kudhihirisha kuwa tuna tabia ya Mungu au laa, kwa KUTII AMRI zake au Kutotii (KUASI). Yesu alisema - Mkizishika Amri zangu mtakaa katika pendo langu kama mimi nilivyozishika Amri za Baba yangu na kukaa katika pendo lake. Yohana 15:10.

TORATI (SHERIA) KUTIMILIZWA KATIKA UPENDO
Pambano kuu kati ya Mungu na Shetani ni juu ya tabia au Amri za Mungu. Ni Yesu pekee anayeweza kuifunua tabia ya Mungu kwetu kuipitia Amri zake, ndiyo maana Mafarisayo walishindwa kumwelewa, hadi wakafikia kusema amekuja kuitangua torati. Naye akathibitisha kuwa hakuja kuitangua Torati au manabii, bali KUTIMILZA. Mathayo 5:17-18 "Msidhani ya kuwa nalikuja kuitangua torati au manabii; la, sikuja kutangua, bali kutimiliza. Kwa maana, amin, nawaambia, mpaka mbingu na nchi zitakapoondoka, yodi moja wala nukta moja ya torati haitaondoka, hata yote yatimie".

Yesu aliitimiza torati na mafundisho ya manabii Kwa kufanya mambo makuu mawili yafuatayo:

1. ALIFUNUA MAHITAJI HALISI YA SHERIA YA UPENDO
Aliifundisha torati au sheria ya Mungu kwa muktadha wa tabia ya Mungu - Upendo. Mafarisayo waliifundisha kwa njia ya Mwili kama makatazo kwa kuwa walitumia akili zao bila kuruhusu Mungu awaongoze. Mfano: Zinaa kutendeka moyoni kwa njia ya Tamaa, Tendo KUUA kuwa ni matokeo ya moyo wenye Hasira, Visasi na kutosamehe, Sabato ya Siku ya Saba kuwa Siku Uponyanyi wa Mwili na Roho, kuwa Siku ya watu kuonyesha Upendo kwa kuhudumia wanaoteseka n.k.

2. KUTIMIZA MPANGO WA UKOMBOZI
Tangia mwanzo Mungu aliweka mpango wa ukombozi kwa mwanadamu aliyeanguka dhambini, kupitia kafara ya Mwanakodoo halisi Yesu Kristo - Ufunuo 13:8. Hata hivyo katika Agano la kale kabla ya Kristo kuja duniani, Mungu alitoa mpango mbadala wa wanadamu kupatanishwa na Mungu, ulikuwa ni wa kutoa Kafara za wanyama, huduma hizo zilikuwa zinaambatana na matoleo ya vyakula na vinywaji. Hayo yalikuwa ni kivuli, yalilenga kifo cha Yesu pale msalabani.

Yesu Kristo alitimiza hitaji la torati juu ya Ukombozi, sheria zote zilizokuwa zikiambatana na huduma za Upatanisho kupitia kafara za wanyama, zilikamilishwa na huduma halisi ya Kristo.... Sheria hizo za kafara zilitimizwa, hazikuondolewa kwa kutohitajika bali sheria zilitimizwa. Kupitia kafara ya Kristo, tunakamilishwa, tunasafishwa dhambi, tunapewa moyo wa nyama, unaoweza kupokea Amri za Mungu kwa moyo wa furaha na Upendo.

Mafarisayo walimtega Yesu wakitaka kumshika uongo, kama kweli anaifundisha Torati au laa, mwanasheria mmoja akamuuliza - "Mwalimu, katika torati ni Amri ipi iliyo kuu?. Akawaambia, Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa Roho yako yote, na kwa akili zako zote. Hii ndiyo Amri iliyo kuu tena ni ya Kwanza. Na ya pili yafanana nayo, nayo ni hii, Mpende jirani yako kama nafsi yako. Katika Amri hizi mbili hutegemea torati yote na manabii". Wakanyamaza kimya, ndipo Yesu akaendelea kuwafundisha zaidi juu ya kazi yake aliyotumwa kuifanya.

WITO:
Ujumbe huu ni kwa ajili yetu sote, ili tuweze kukua kiroho, na kufanya matengenezo, kwa kadri tunavyoangaziwa nuru. Kumbuka tunaishi katika kizazi kilichoathiriwa na mapokeo ambayo yamepofusha akili za watu kwa hadithi za kutungwa ili wote wahukumiwe kwa kutotii maagizo ya Mungu. Wewe ni shahidi, leo kuna Injili nyingi na zenye mafundisho yanayokinzana na Amri za Mungu, kinyume na mafundisho ya Kristo. Lakini pia wegi wako nje ya Neema ya Kristo, wakiukataa wokovu halisi, wakijitahidi kutii kwa nguvu zao, na kujikuta wakiangukia katika utumwa wa Dhambi kila iitwapo leo.

MUNGU AKUBARIKI UNAPOFUNGUA MOYO WAKO NA KURUHUSU ROHO MTAKATIFU AENDELEE KUTAKASA KWA NENO LA MUNGU.

Na. Ev. Eliezer Mwangosi
Simu:  0767210299 - Kwa ajili ya Maswali, ushauri na Maombi.




Sent from Samsung tablet

eliezer.mwangosi

unread,
May 24, 2016, 3:03:42 PM5/24/16
to
NENO LA LEO - JAMBO LILILOWASHINDA WENGI
Warumi 12:21 "Usishindwe na ubaya, bali uushinde ubaya kwa wema".

Ni jambo la kawaida siku hizi kusikia, vyombo vya habari vikitangaza mauaji yanayotokea kutokana na wivu wa mapenzi. Sitasahau baba mmoja aliyemkata mke wake sehemu ya siri na kuichemsha ili aile nyama.

Akiwa akiendelea kuchemsha, mke wake, akazidiwa na kuzimia baada ya kutokwa na Damu nyingi, mwishowe alikata roho. Mumewe aliishia jela akikabiriwa na kesi ya mauaji.

Kuna wengi ambao, hawataurithi uzima wa milele kwa dhambi ya kulipa UBAYA UBAYA, hata wakiombwa msamaha, wanasamehe mdomoni, huku mioyo yao ikiwa imejaa visasi, utawasikia wakimwambia kila wanayemuona.

Kuushinda ubaya kwa wema, ni tabia inayoweza kupatikana kwa watoto halisi wa Mungu. Kila kona ya magenge ya watu, hutakosa kusikia watu wakieleza ubaya wa wenzao, hata katikati ya wanaojiita watoto wa Mungu, utasikia lugha za visasi, malaumu n.k.

Neno la leo linatutaka tuushinde ubaya kwa wema, kwani kisasi ni cha Mungu.

NEEMA YA MUNGU NA BARAKA ZAKE ZIWE JUU YA KILA MMOJA WETU SASA NA HATA MILELE

Na. Ev. Eliezer Mwangosi
Simu: 0767210299.




Sent from Samsung tablet
Reply all
Reply to author
Forward
0 new messages