WAJIBU WA WAZAZI KUWALEA WATOTO WAO

335 views
Skip to first unread message

Bahati Mashimba

unread,
Apr 26, 2012, 4:50:15 PM4/26/12
to yourtr...@googlegroups.com
 
 Wakolosai 3:21 "Ninyi akina baba, msiwachokoze watoto wenu, wasije wakakata tamaa"

 Niwajibu muhimu wa wazazi baba na mama kuwapa watoto wao maelekezo na kuwarudi kwa namna ya malezi ya kristo.Wazazi wanapaswa kuwa mfano wa maisha na mwenendo wa kikristo wakiujali zaidi wokovu wa watoto wao kuliko msimamo wa kijamii.

Lazima wazazi wajifunze kweli ya Mungu na kuitii ndipo wanaweza kufundisha kweli hiyo kwa watoto  wao na kuwalea katika maadili mema.Pia wazazi wanaoifahamu kweli inawapasa kuwasaidia wazazi wengine  ili nao waijue kweli ya Mungu na waweze kufundisha watoto wao. Kanisa ni lazima liwasaidie wazazi wajue kweli ya Mungu.
 
Watoto ni urithi wa Bwana 'Zab127:3 " Tazama,wana ndio urithi wa BWANA, Uzao wa tumbo ni thawabu"

Ni wajibu wa wazazi kuwapa watoto wao malezi yatakayowandaa kuishi maisha ya kumpendeza Mungu.Lakini leo tunao wazazi wengi hawajuii kuwafundisha watoto Neno la Mungu nyumbani mwao. Wajibu huu wameuacha katika mikono ya Kanisa/shule/vyuo na dunia.

Ya wezekana hawajui au wamepuuza neno la Mungu linalosisitiza wajibu huo.Biblia inatuonyesha mafundisho ya kikristo ni kazi ya nyumbani baba na mama Kumbukumbu la Torati 6:4-9 " Sikiza,Ee Israeli;BWANA,Mungu wetu,BWANA ndiye mmoja.Nawe mpende BWANA,Mungu  wako,kwa moyo wako wote,na kwa roho yako yote,na kwa nguvu zako zote. Na maneno haya ninayokuamuru leo,yatakuwa katika moyo wako,nawe uwafundishe watoto wako kwa bidii, na kuyanena, uketipo katika nyumba yako,na utembeapo njiani,na ulalapo,na uondokapo.Yafunge yawe dalili juu ya mkono, nayo  yatakuwa kama utepe katikati ya macho yako.Tena yaandike juu ya miimo ya nyumba yako,juu ya malango yako" 

 na kama ilivyoandikwa kwenye injili ya  Mathayo28:19-20"Basi,enendeni,mkawafanye mataifa yote kuwa  wanafunzi,mkiwabatiza  kwa  jina la Baba, na  Mwana, na Roho Mtakatifu, na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru Ninyi;na tazama, mimi nipo pamoja nanyi sikuzote,hata ukamilifu wa dahari"

Moja ya njia kuu za kuonyesha upendo wetu kwa Mungu ni kujishughulisha na maendeleo ya kiroho ya watoto wetu mapema.Kutojali na mitazamo tofauti hutufanya tusibebe wajibu wetu kama wazazi.

Mitazamo  mbalimbali kama watoto hawana dhambi,watoto hawahitaji injili,haiwezekani mtoto kuamini na kumtegemea Mungu hufanya wazazi wasione umuhimu wakuwafundisha neno la Mungu watoto wao.Hatujui hatari inayowakabiri  watoto katika maisha yao.Watoto wamezaliwa ulimwengu tofauti na ule tunaoujua sisi(maadili).
Shetani anawatamani na anafanya kila mbinu ili awaharibu na kuwaangamiza Yoh10:10a " Mwivi haji ila aibe na kuchinja na kuharibu" Watoto hawa hawana msaada mbele ya hayo maangamizi na hawawezi kusimama wala kuepukana na anasa za dunia hii.

Tukizijua sababu hizi na zingine ndipo tutaitika wito wa kuwafundisha watoto wetu kwa bidii na kuwalea katika njia ambayo hawataiacha.


Mch G.Bundala
AICT

Reply all
Reply to author
Forward
0 new messages