Amina.Palipo na Upendo pana umoja , amani na maendeleo
Ubarikiwe sana na Mungu
On 11/8/15, eliezer.mwangosi <
eliezer....@yahoo.com> wrote:
> NENO LA LEO - USHAURI KWA WATU WA MUNGU BAADA YA UCHAGUZI
> Mathayo 5:44-45 "Lakini mimi nawaambia, wapendeni ADUI zenu, waombeeni
> WANAOWAUDHI; ili mpate kuwa wana wa Baba yenu aliye mbinguni....."
>
> Nilipokuwa nafuatilia post za wapendwa wengi na wakati mwingine kusikiliza
> wakiongea juu ya matokeo ya uchaguzi hasa wa Uraisi, nimesikitika kugundua
> kwamba wapendwa wengi wameghafilika na kutanga mbali na misingi ya wokovu
> wetu. Wengi wameruhusu shina la uchungu lichipuke ndani ya mioyo yao na
> hatimaye kuwatia unajisi (Soma Waebrania 12:14-15), roho za visasi na uadui
> zimetawala kuwasumbua wengi.
>
> Katika somo langu la 30.08.2015, nilitoa somo lililosema: WATU WA MUNGU NA
> SIASA / UCHAGUZI, likitoa mwanga jinsi Mungu anavyohusika na tawala za
> jamii, na watu wa Mungu wanachopaswa kukifanya na namna ya kuyapokea
> matokeo. Baada ya matokeo nimegundua watu wa Mungu wengi hawajui jinsi Mungu
> anavyotenda kazi hasa katika michakato ya kupata watawala wa serikali
> inayojumuisha WAOVU NA WEMA, mawazo ya Mungu yako tofauti sana na mawazo
> yetu. Hivyo tunapoona mambo hayako sawa, tunapaswa kutulia na kutafuta
> hekima yake.
>
> Neno linasema "Mpende Adui na Kumuombea", Jihoji Kama Mcha Mungu, baada ya
> matokeo ya uchaguzi na Raisi kuapishwa, iwe ni kwa haki au laa, umechukuwa
> hatua gani? Siku moja kabla ya Raisi kuapishwa nilisikia malalamiko mengi
> tena yenye uchungu na wengine kufikia kuombea Mabalaa yatokee ili
> asiapishwe. Hadi leo hii kuna wapendwa wengi wanaombea mabaya yatokee kwa
> Raisi aliye madarakani, ikiwa ni adhabu kutoka kwa Mungu. Kumbukeni Chama au
> Serikali haina Dini, ila ndani yake kuna wacha Mungu na Waovu. Kumbukeni
> Taifa la Israeli lilipigwa na kuhujumiwa haki na mataifa maovu kwa sababu tu
> ya maovu ya watu wachache.
>
> KWA WATANZANIA: Wale wanaoamini kuwa wameporwa haki yao Kupitia mchakato wa
> uchaguzi, ni wakati wa kukaa na Mungu ili awape hekima ya kufanya maamuzi
> sahihi bila kutenda UOVU, wajichunguze na kujihoji, wakiona kuna uovu ndani
> yao juu ya jamii watubu na kuungama, ili Mungu ajidhihirishe juu yao kwa
> wakati. Waombeeni walioko madarakani kwa wakati huu, ili Mungu awape hekima
> na ufahamu wa kutenda mambo kwa HAKI. Kusudi la Mungu ni KUOKOA sio kupoteza
> roho, ombea waokolewe, wawe na hofu ya Mungu, ndipo mtapandishwa juu ya
> Vilima kwa wakati uliokubalika.
>
> KWA WATANZANIA: Wanaoamini wameshinda kwenye uchaguzi; kwa hakika Mungu
> ndiye anayejua, kama ni kwa uhalali au laa. Kama nilivyotangulia kusema,
> ndani ya vyama na serikali kuna WAOVU na WEMA. Ikitokea Mungu ameruhusu
> mafanikio kwa njia isiyo halali, sio kwamba anakubaliana na uovu, ila kuna
> neema inamtafuta mmoja atubu, ili aokolewe. Huu ni wakati wa mpito wa
> kupimwa tena katika mizania ya Mungu. Kama kuna Uovu wowote ni wakati wa
> Kutubu ili Mungu awafanikishe katika HAKI. Kumbukeni hakuna AMANI Kwa Waovu
> (Isaya 48:22).
>
> Kama ushindi ulikuwa ni wa halali, bado mnatakiwa kunyenyekea chini ya Mkono
> wa Mungu, ili azidi kuwakweza na kuwafikisha katika vilele. Bila Mungu
> hekima ya Mwanadamu ni patupu, shetani atawashinda na kuwa na hali mbaya
> kuliko matazamio ya watanzania. 1Petro 5:6-7.
>
> HITIMISHO: Bwana Mungu anasema "Maana mawazo yangu si mawazo yenu, wala njia
> zenu si njia zangu; asema BWANA" Isaya 55:8. Watu wa Mungu tunahitaji kuwa
> makini na kuomba hekima kwa Mungu, hasa tunapojihusisha na mambo ya Vyama
> vya siasa ambavyo havina misingi ya Dini. Sisi tunatazama kwa macho ili
> kutimiza makusudi na mapenzi ya mioyo yetu, lakini Mungu hayuko hivyo.
> Usishindwe na Ubaya, bali uushinde ubaya kwa wema 'Warumi 12:21'.
>
> Watu wa Mungu tunaoishi katika kazazi hiki kiovu, tunapaswa kuwa chachu ya
> kuleta AMANI, tukiwaombea waovu waokolewe, kuchukia UOVU sio kulipa visasi
> na kuombea mabaya, hizo ni roho za yule adui. Waovu wanaonywa kwa upendo,
> wanashauriwa, wanaombewa, wakiendelea na uovu unaotudhuru tutatumia vyombo
> vya sheria na kutafuta haki. Ni agizo la Mungu kuzitii Mamlaka zozote
> zilizowekwa katika Jamii - Warumi 13:1-7. Mwenye Mamlaka ya mwisho juu ya
> Kuziweka na Kuziangusha Mamlaka ni Mungu, kwa njia zozote mwanadamu hawezi
> bila Mungu.
>
> MUNGU BARIKI TANZANIA - TIMIZA KUSUDI LAKO KWA WATANZANIA - KATUONDOLEE UOVU
> - KILA ALIYESHIKA MAMLAKA UKAMTIISHE AKAWE CHINI YA MAMLAKA YAKO - VIONGOZI
> WOTE UWABARIKI NA KUWAPA HEKIMA YA KUONGOZA TAIFA LA TANZANIA KWA WAKATI
> ULIO AMRIWA.
>
> Na Ev. Eliezer Mwangosi - Tel. 0767210299 - Email.
>
eliezer....@yahoo.com.
>
>
>
>
> Sent from Samsung tablet