UMUHIMU WA MAOMBI KWA MKRISTO

17,814 views
Skip to first unread message

Bahati Mashimba

unread,
Jun 5, 2011, 4:20:08 PM6/5/11
to YourTrueVine

Maombi ni ushiriki wa mtu na Muumba wake.Ni hali ya kiroho zaidi ya hali ya mwili.Ni hali ya kuamini Mungu zaidi kwa kutaja mahitaji yetu.Maombi ni njia tunayopata kuungana na Mungu kwa namna ya Roho.Maombi kwa wakati mwingine yanaonekana ni kama adhabu kwa baadhi ya Wakristo na kupelekea watu kufanya sala fupi wakati wa chakula, wakati wa usiku(wanapo taka kulala), asubuhi na wakati wanapokuwa kanisani au kwenye mikutano ya dini.Tunaona waziwazi wanafunzi wake Yesu wakati Yeye akiwa anasali Bustanini Gethsemane huku wanafunzi wake wakishindwa kukesha pamoja naye katika maombi hata saa moja.Tunaposhindwa kufanya maombi ya hata muda kidogo kwa siku tunampa nafsi shetani ya kutushambulia utakatifu wetu, uchumi wetu, afya zetu na hata kutuingiza majaribuni.

Yesu aliwaambia wanafunzi wake na sisi tudumu katika maombi ili tusije tukaingia kwenye tamaa za dunia hii.Neno la Mungu linasema 'Kesheni na kusali ili msije mkaingia katika majaribu.Roho iradhi lakini mwili ni dhaifu'Mathayo 26:41

Kanuni muhimu katika kuomba kwa Mkristo yoyote kwanza ni kuomba toba kabla ya kutaja mahitaji ya kuombea na pia kuwa na imani kwamba tunachoomba Mungu atatupatia kwa mapenzi yake(Mathayo11:24-25 - Kwa hiyo nawaambieni, mnaposali na kuomba kitu aminini kwamba mnakipokea nanyi mtapewa.Mnaposimama katika kusali, msameheni kila mtu aliyewakosea chochote, ili Baba yenu aliye mbinguni awasamehe nyinyi makosa yenu).

Katika hali ya sasa Wakristo wengi wamejikuta katika hali ya kukata tamaa kimwili na kiroho pia, na hadi kusabisha neno MAOMBI kwao kuwa ni kama mzigo au kuwa hayana umuhimu kwao au maombi ni ya akina fulani tu kanisani.Na wapo Wakristo wengine hawajali kabisa kuomba.Lakini Neno la Mungu linatuambia maombi ni silaha ya Mungu ya kutuwezesha kuyapinga mashamubulizi dhidi ya jeshi ovu la ulimwengu wa roho na ya watawala wakuu wa giza.Tunasoma Neno la Mungu katika waraka wa Mtume Paulo kwa Waefeso ' Salini daima, mkiomba msaada wa Mungu.Salini kila wakati kwa nguvu ya Roho.Salini bila kuchoka mkisali kwa ajili ya watu wote wa Mungu.'Efeso 6:18

Maombi yana tusaidia kujiweka tayari kwa siku ya mwisho.Tunasoma katika maandiko matakatifu kuwa 'Mwisho wa vitu vyote umekaribia, kwa hiyo mnapaswa kuwa na utaratibu na kukesha ili muweze kusali'1Petro4:7

Maombi ni alama ya ushindi ya kuonyesha kuwa sisi tuwategemezi wa Mungu.Mfalme Daudi alimulilia BWANA (Zab22:1-4 .....Waezee wetu walikutegemea nawe ukawaokoa)

Mpendwa tuombe Mungu kwa neema yake atupe nguvu na msaada ili tudumu katika maombi na kumshukuru Mungu kwa kila jambo.Neno la Mungu linasema 'Msiwe na wasiwasi juu ya kitu chochote ila kwa kila hali mwombeni Mungu katika sala juu ya mahitaji yenu kwa shukrani'.Filipi 4:6.

Mpendwa napenda kukushirikisha kwa juma linaloanza kesho tuombe kila siku juu ya mahitaji yafuatayo.

1.TUOMBEE TAIFA 
Ezekiel 21:21-22. Tumwombe Mungu kwa ajili ya madhabahu zilizoinuliwa na waovu katika nchi- mikoa, wilaya na vijiji ili kumiliki maeneo ya nchi kinyume na taratibu za Mungu. Tuzungumze na ardhi ya Tanzania itapike waovu wote wanaofanya iugue (Warumi 8:22). Achilia Damu ya Yesu kwenye mikoa yote,wilaya,vijiji na kwenye jua,mwezi,nyota na anga lote kwenye mito na bahari haribu ratiba na kumbukumbu zote za waabudu sanamu.
 
2.TOBA KWA KANISA
Ezra 10:1 -2 - Tuungame mbele za Mungu wetu kwani tumemkosa kwa uovu mkuu kwa kanisa kujiunganisha na sanamu. Aidha uasherati tunaofanya kwenye madhabahu ya Bwana ni kulinajisi jina la lake (2 Nyakati 20:9) - tuungame kwa ajili ya taifa. 
Tuombe Mungu aachilie kisasi juu ya wale maadui wanaosimama kinyume na nyumba yake Wakolosai 3:1-2. Kama kanisa tuombe Roho Mtakatifu aturudishe rohoni tuweze kumtafuta Mungu katika mapenzi yake (2 Wakor. 5:18-19), tuombe huduma ya upatanisho iliyo ndani Kristo Yesu ituwezeshe kuwa na mshikamano katika kanisa.
 
3. TOBA KWA FAMILIA- Kutoka 12 :22-24- Tuungame na familia zetu na baada ya toba ya familia tunampaka Damu ya Yesu kila aliye katika familia kwa njia ya maombi. Futa kwa Damu ya Yesu manuizo yaliyofanyiwa familia yako (Ufunuo 9:4).
 
4.ISRAELI- Yeremia 33:6-11 - Tusome yote na tuombe Roho Mtakatifu aiponyeshe Israeli na Mungu awaondolee uovu wote.
 
5.AFRIKA -Ezekieli 36:32-36 - Tumwombe Mungu aachilie na kusamehe uovu wa Afrika na mkono wake wenye nguvu ujenge Afrika kwa upya.
 
Na sisi tuko dhabiti  mbele ya Mungu kwani tuna hakika kwamba tukimwomba chochote kadiri ya matakwa yake, yeye hutusikiliza 1 Yoh5:14

Deborah Mgedzi

unread,
Jun 6, 2011, 6:25:13 AM6/6/11
to yourtr...@googlegroups.com
Ubarikiwe kwani nimewapelekea na wenzangu!


From: Bahati Mashimba <bmas...@gmail.com>
To: YourTrueVine <yourtr...@googlegroups.com>
Sent: Sun, June 5, 2011 1:20:08 PM
Subject: UMUHIMU WA MAOMBI KWA MKRISTO
--
Usikubali kushindwa na ubaya bali ushinde ubaya kwa wema.Waroma12:21

Saimon

unread,
Jun 6, 2011, 7:59:09 AM6/6/11
to YourTrueVine
Bwana apewe sifa.Kuomba kwake mwenye haki kuna faida sana kama akiomba
kwa bidii(Yakobo5:16)

On Jun 6, 12:25 pm, Deborah Mgedzi <deborahmge...@yahoo.com> wrote:
> Ubarikiwe kwani nimewapelekea na wenzangu!
>
> ________________________________
> From: Bahati Mashimba <bmashi...@gmail.com>
> Daudi alimulilia BWANA(Zab22:1-4 .....Waezee wetu walikutegemea nawe ukawaokoa)

Bahati Mashimba

unread,
Jun 10, 2011, 4:55:19 AM6/10/11
to YourTrueVine, Ezekieli Peter, richard mjaki

Ikiwa njaa katika nchi, au tauni au ukosefu wa mvua, au ukungu au nzige au panzi,au ikiwa watu wako wamezingirwa na adui zao katika mji wao wowote ule au yakiwa mapingo mengine yoyote au ugonjwa wowote, tafadhali usikie maombi yoyote yaatakayoombwa na  mtu yeyote au watu wako wote Israeli, watakaojua kila mtu pigo lake mwenyewe  na maumivu yake mwenyewe, akinyoshea  nyumba hii  mikono yake basi usikie kule mbinguni,  pahali  unapokaa , usamehe na kurudishia kila mtu kwa kadiri ya njia zake zote, wewe unayejua moyo(Kwa sababu wewe ndiwe mwenye kujua mioyo ya wanadamu wote).Ili wakuogope wewe(watakutii), waende katika njia zako siku zote watakazoishi katika nchi ambayo uliwapa baba zetu. 2 Nyakati 6:28-31

 

Ikiwa watu wangu walioitwa kwa jina langu wakijinyenyekesha na kuomba na kuutafuta uso wangu na kuacha njia zao mbaya, basi nitasikia toka mbinguni na kusamehe  dhambi yao na kuponyesha nchi  yao.Sasa macho yangu yatafumbuliwa na masikio yangu yatasikia maombi ya watu wanaoomba pahali hapa.2 Nyakati 7:14-15.
 
Humble yourselves in the sight of the Lord and he shall lift you up James4:10
 


2011/6/6 Saimon <bmas...@gmail.com>
Reply all
Reply to author
Forward
0 new messages