Zaburi40:1-3
Nalimngoja BWANA kwa saburi,Akaniinamia akakisikia kilio changu.Akanipandisha toka shimo la uharibifu,Toka udongo wa utelezi, Akaisimamisha miguu yangu mwambani, Akaziimarisha hatua zangu.
Mpendwa katika Bwana Yesu Asifiwe.Wakati tunapokuwa kwenye changamoto yoyote ile kwenye maisha yetu ni Mungu pekee anayejua ,anayesikia na kutusikiliza vilio vyetu tunavyomlilia kupitia maombi.
Wakati tunapojihisi tupo kwenye shimo la uharibifu na hatuna msaada wa kututoa humo , na tunapotaka kutoka humo kwenye shimo tunateleza.
Ni Mungu pekee wa kutushika na mkono na kutusimamisha mahali salama kwenye mwamba ambaye ni Yesu Kristo na ndiye anayeimarisha hatua zetu.Yawezekana upo kwenye changamoto kwenye ndoa, uchumba, kazi, biashara,kupata ajira, mtaji, afya,huduma na unajiona ni kama upo kwenye shimo linaloteleza, mwamini Yeau na paza sauti ya kilioa chako ili kimfikie Mungu na aweze kukusikia na kukutoa katika changamoto ulizo nazo.
Mungu akujibu sasa na haja ya moyo wako