Amina . Bwana azidi kukubariki mtumishi wa Bwana
NENO LA LEO: WAJAPOKUTUPA SHIMONI YEYE ATAKUINUA VILELENI
Mwanzo 39:2 "Bwana akawa pamoja na Yusufu, naye AKASITAWI, naye alikuwa katika nyumba ya bwana wake, yule mmisri."
Hebu tutafakari kisa hiki, Yusufu alichukiwa na ndugu zake kwa sababu ya HAKI, wakaamua kumtupa shimoni ili afe, baadaye akauzwa kwa wafanyabiashara, nao wakamuuza Misri kwa Potifa, baadaye akasingiziwa kubaka mke wa Potifa akatupwa gerezani. Mwanzo 37:21-28, 39:1-23.
Mwisho tunaona Bwana akiwa na Yusufu gerezani, akamtumia kuitafsiri ya ndoto mfalme farao, ndipo farao akaamua kumpatia cheo cha kuwa juu ya misri yote, akawa ndiye mtawala wa pili kwa farao. Mwanzo 41:41-44.
Ni kawaida kukuta watu wanapanga njama za hila ili kumuonea na kumharibia maisha mwenzao, wanapenda asifanikiwe, kwa sababu ya wivu, kwa midomo ya uongo huzusha maneno, huchonganisha, wako tayari wamchafue ili wamharibie maendeleo yake.
Rafiki; ukiona hali hiyo inatokea, iwe ni katika maisha ya kawaida au kwemye kazi ya Mungu, mshukuru Mungu, jua hiyo ni kazi ya shetani, zidi kumtazama Mungu na kuwaombea. Hata wakutupe kwenye shimo la taka kwa namna yoyote ile, Bwana atakupandisha kutoka kilele hadi kilele cha mafanikio.
Mwanadamu anapopanga kukuangusha, kukukanyaga, kukudhalilisha, kukukatisha tamaa, kukuvunja moyo, Mungu yeye anapanga KUKUPANDISHA VILELENI na wao kuwashusha chini, endelea kuwa mwaminifu kwa Mungu siku zote, naye hatakuacha.
WEMA WA BWANA UKAZIDI KUWAFUNIKA SIKU HADI SIKU
Na: Ev. Eliezer Mwangosi
Simu: 0767210299
Tovuti: evmwangosi.blogspot.com.
FB: Ev Eliezer Mwangosi.Sent from my Samsung Galaxy smartphone.
On Thu, Jun 30, 2016 at 6:09, 'eliezer.mwangosi' via YourTrueVine<yourtr...@googlegroups.com> wrote:NENO LA LEO - SIRI YA KUPATA AMANI YA KWELI
Yohana:14:27 "Amani nawaachieni; amani yangu nawapa; niwapavyo mimi sivyo kama ulimwengu utoavyo. Msifadhaike mioyoni mwenu, wala msiwe na woga."
Siku moja nikiwa nasafiri kwa basi, nilikaa karibu na mama mmoja, mara baada ya muda mfupi nikasikia simu yake inaita, alipoipokea akaanza kuporomosha matusi kwa kufoka, huku akifyonya. Muda haukupita nikamuona anaanza kulia. Ilibidi nitulie na kuanza kumuombea kimoyomoyo, ili Bwana atulize dhoruba iliyo katika moyo wake, make niliona akiwa na stress kubwa.
Baada ya nusu saa kipita alionekana kutulia, ndipo nikaamuliza lililomsibu, akaongea kwa jazba akasema "Si MBWA huyu anautesa moyo wangu!" Kupitia maelezo yake niligundua mume wake hakulala nyumbani, alipitia kwa Mchepuko hadi asubuhi. Mke wake alionyesha hali ya kuchoshwa na kuumizwa kwa usaliti wa mapenzi, kiasi kwamba kila siku alikuwa na stress au msongo wa mawazo.
Kadiri siku zinavyosonga, ndivyo idadi ya watu wanaoishi na misongo ya mawazo inavyozidi kuongezeka, huku wakiathirika kiafya na hata katika ufanisi wa kazi zao. Neno la leo, linatuongoza kumtegemea Yesu Kristo wakati wote tunapopitia changamoto zenye machungu na kuumiza mioyo yetu.
Wengi ni mashahidi kuwa AMANI ya kweli na ya kudumu, inapatikana kwa Mungu. Kuna waliojijengea wigo wa Amani kwa wapenzi wao, mara walishangaa wakipitia machungu baada ya kujeruhiwa na waliokuwa wanawaamini. Hakuna kitu chochote kinachoweza kutupatia AMANI ya kudumu nje ya Mungu.
Hebu kila mmoja wetu aweke Imani yake kwa Mungu, usiruhusu mwanadamu mwenzio abebe nafsi yako, wala pesa isishike nafsi yako, wala kitu chochote, hivyo vyote vinabadilika bila kutarajia. Upendo wa mwanadamu kwako unaweza kutoweka na kuhamia kwa mwingine, lakini Upendo wa Mungu kwako ni wa milele. Mwamini na Kumtegemea Mungu, naye ataujaza moyo wako Amani Kamilifu, mawimbi yakipita HUTAFADHAIKA.
AMANI YA KRISTO IKAIJAZE MIOYO YETU FURAHA NA TUMAINI DAIMA.
NAWATAKIA SIKU NJEMA YENYE BARAKA TELE.
Na: Ev. Eliezer Mwangosi
Simu: 0767 210 299. Kwa ushauri na maombi.Sent from Samsung tablet