Bwana akaona ya kuwa maovu ya mwanadamu ni makubwa duniani na kwamba kila kusudi analowaza moyoni mwake ni baya tu siku zote (Mwanzo 6:5)
Kusudi kuu la Mungu kumuumba mtu kwa mfano wa sura yake ilikuwa ni kumfanya binadamu aweze kuwaza mema daima, amiliki na kutawala dunia kwa niaba ya Mungu. Adamu na Hawa hawakuwahi kuwaza mabaya kabla ya kuasi.Uwezo huo
ulipotea wakati Adamu na Hawa waliposhindwa kushika makusudi ya Mungu na kukubali jaribu la nyoka lililotoka nje ya miili yao hadi wakala tunda la mti wa ujuzi wa mema na mabaya(Mwenyezi Mungu akamuuliza (Adamu) ' Nani aliyekuambia kwamba uko uchi?Je, umekula tunda la mti nililokuamuru usile?' Mwanzo 3:11). Mungu anasikitika na kuhuzunika sana anapoona mwanadamu kila siku anawaza mabaya na kutamani kuyatenda.
Tunapomwamini Yesu Kristo tunapewa Roho mpya inayotuwezesha kusulubisha mawazo mabaya na tamaa za dunia hii.Watu wanapokataa kumtambua Mungu na kuruhusu Roho Mtakatifu kukaa ndani yao matokeo yake ni kuruhusu fikira potuvu zilizojaa kila aina ya uovu, dhuluma, ulafi, ufisadi, wivu, uuaji,ugomvi, udanganyifu, majivuno,kutotimiza ahadi,
kukosa wema wala huruma kwa wengine na mambo mengine yote yanayofanana na hayo.
Mwamini
Yesu na ukae ndani yake ili uelee juu ya makusudi ya Mungu na
utaokoka kama Nuhu na ndugu zake walivyoelea juu ya maji wakiwa ndani ya Safina wakati
wa gharika .
Nawatakia wote neema ya Mungu iwe juu yenu.
Wale walio na Kristo wameisulubisha hali yao ya kidunia pamoja na mawazo yake mabaya na tamaa zake.Wagalatia 5:24
|