KUWATAMBUA MANABII WA UONGO

3,384 views
Skip to first unread message

YourTrueVine

unread,
Sep 27, 2011, 2:02:47 AM9/27/11
to YourTrueVine
Salaam,

Kila alhamisi nitakuwa na Somo la Wana Ndoa na kila Ijumaa litakuwa
somo la Vijana

NENO LA LEO: Yeremia14:14

“Ndipo BWANA akaniambia, Hao manabii wanatabiri uongo kwa jina langu
mimi; mimi sikuwatuma, wala sikuwaamuru, wala sikusema nao; wanawapeni
unabii wa maono ya uongo, na uaguzi, na neno la ubatili, na hadaa ya
mioyo yao”

TAFAKARI:

Leo tunaangalia baadhi ya Sifa za Manabii wa Kweli na Uongo.

Yesu alisema “Mtawatambua kwa matunda yao….” Mathayo 7:16. Mtunda ni
matendo ya Mtu. Kwanza lazima tuelewe sifa za watu wa Mungu au
Watakatifu: Yohana aliambiwa maneno haya: “Hapa ndipo penye subira ya
watakatifu, HAO wazishikao AMRI za Mungu na Imani ya Yesu” Ufunuo
14:12. Na nabii Isaya anasema “Na waende kwa Sheria na Ushuhuda; ikiwa
hawasemi sawasawa na neno hili, bila shaka kwa hao hapana Asubuhi”
Isaya 8:21. Na Yohana anasema “Yeye asemaye, nimemjua, wala hazishiki
AMRI zake, ni Muongo, wala kweli haimo ndani yake” 1Yohana 2:4. Hata
hivyo kuna Sheria Zilizoishia msalabani ambazo zilikuwa ni kivuli.
Wengi Wasio na ufahamu wa neno, wamechanganya AMRI kumi za Mungu
zinazoonyesha Dhambi, na Sheria zilizolenga Kifo cha Yesu Msalabani.

Manabii na viongozi wa Dini, wanaokataa Kufundisha Amri za Mungu kwa
sababu zozote zile, Mungu anasema kwa Hao Ni GAIZA hapana Asubuhi.
Amri za Mungu zinaonyesha Dhambi, ni kama Kioo. Na NEEMA ya Kristo
kupitia Kifo chake Msalabani – Inatupatia Msamaha bure baada ya TOBA,
Inatusafisha dhambi na kutupatia Haki mbele za Mungu, na Inatupatia
Nguvu ya Kushinda Dhambi kwa njia ya Roho Mtakatifu.


Ukiona Nabii, Mtume, Mchungaji n.k. anafanya kati ya tabia hizi
zifuatazo, hajatumwa na Mungu:- Upendeleo, Chuki, Tamaa ya Ngono,
visasi, ulevi, wivu, anagombea vyeo, muongo, anapenda wenye Pesa, ana
dharau maskini, mwizi, mdanganyifu, hafundishi Amri za Mungu, hakemei
dhambi, mnafiki, mafundisho makuu ni mibaraka, utajiri na Miujiza,
mshirikina, anamkana Yesu. n.k. Huyo hana Roho wa Mungu – Rafiki! Nuru
na Giza Havikai pamoja. Tunashuhudia wengi wanaodai kujazwa Roho
wanafanya mambo ya kukatisha tamaa – Hao ni wafanya BIASHARA tu kwa
mgongo wa Dini. Soma Neno, Omba, Amini na kutii, bila Kujali ITIKADI
ZA DINI AU DHEHEBU. Kweli itatuweka HURU – Muda si mrefu wengi
watagundua kuwa wamedanganywa, wakiwa wamechelewa.


BABA MUNGU AWABARIKI NA KUWAPATIA SIKU NJEMA YENYE AMANI NA MAFANIKIO
TELE

Na: Eliezer Mwangosi

Japhet Boaz

unread,
Sep 27, 2011, 2:46:44 AM9/27/11
to yourtr...@googlegroups.com
Ubarikiwe Eliezer kwa somo zuri.

Ni somo linalogusa hali halisi ya siku za leo ambapo kanisa limegubikwa na
michanganyo na 'usanii' mwingi.

Hata hivyo naona umeongea kwa ujumla sana juu ya sifa za nabii wa uongo
kiasi ambacho umeelezea mtenda dhambi. Naomba ufafanue ikiwezekana kila sifa
uliyoitaja kwa undani mf. Upendeleo ..katika maswala yapi, wakati gani, na
ka-mfano kidogo.

Mambo mengine hayana mjadala mtu hawezi kuwa nabii huku akiwa mzinzi au
Mwongo.


La mwisho naomba kuuliza... kujazwa Roho ni vibaya?


Ahsante,

J

-----Original Message-----
From: yourtr...@googlegroups.com [mailto:yourtr...@googlegroups.com]
Sent: September 27, 2011 9:03 AM
To: YourTrueVine
Subject: KUWATAMBUA MANABII WA UONGO

Salaam,

Kila alhamisi nitakuwa na Somo la Wana Ndoa na kila Ijumaa litakuwa
somo la Vijana

NENO LA LEO: Yeremia14:14

"Ndipo BWANA akaniambia, Hao manabii wanatabiri uongo kwa jina langu
mimi; mimi sikuwatuma, wala sikuwaamuru, wala sikusema nao; wanawapeni
unabii wa maono ya uongo, na uaguzi, na neno la ubatili, na hadaa ya
mioyo yao"

TAFAKARI:

Leo tunaangalia baadhi ya Sifa za Manabii wa Kweli na Uongo.

Yesu alisema "Mtawatambua kwa matunda yao.." Mathayo 7:16. Mtunda ni


matendo ya Mtu. Kwanza lazima tuelewe sifa za watu wa Mungu au
Watakatifu: Yohana aliambiwa maneno haya: "Hapa ndipo penye subira ya
watakatifu, HAO wazishikao AMRI za Mungu na Imani ya Yesu" Ufunuo
14:12. Na nabii Isaya anasema "Na waende kwa Sheria na Ushuhuda; ikiwa
hawasemi sawasawa na neno hili, bila shaka kwa hao hapana Asubuhi"
Isaya 8:21. Na Yohana anasema "Yeye asemaye, nimemjua, wala hazishiki
AMRI zake, ni Muongo, wala kweli haimo ndani yake" 1Yohana 2:4. Hata
hivyo kuna Sheria Zilizoishia msalabani ambazo zilikuwa ni kivuli.
Wengi Wasio na ufahamu wa neno, wamechanganya AMRI kumi za Mungu
zinazoonyesha Dhambi, na Sheria zilizolenga Kifo cha Yesu Msalabani.

Manabii na viongozi wa Dini, wanaokataa Kufundisha Amri za Mungu kwa
sababu zozote zile, Mungu anasema kwa Hao Ni GAIZA hapana Asubuhi.
Amri za Mungu zinaonyesha Dhambi, ni kama Kioo. Na NEEMA ya Kristo

kupitia Kifo chake Msalabani - Inatupatia Msamaha bure baada ya TOBA,


Inatusafisha dhambi na kutupatia Haki mbele za Mungu, na Inatupatia
Nguvu ya Kushinda Dhambi kwa njia ya Roho Mtakatifu.


Ukiona Nabii, Mtume, Mchungaji n.k. anafanya kati ya tabia hizi
zifuatazo, hajatumwa na Mungu:- Upendeleo, Chuki, Tamaa ya Ngono,
visasi, ulevi, wivu, anagombea vyeo, muongo, anapenda wenye Pesa, ana
dharau maskini, mwizi, mdanganyifu, hafundishi Amri za Mungu, hakemei
dhambi, mnafiki, mafundisho makuu ni mibaraka, utajiri na Miujiza,

mshirikina, anamkana Yesu. n.k. Huyo hana Roho wa Mungu - Rafiki! Nuru


na Giza Havikai pamoja. Tunashuhudia wengi wanaodai kujazwa Roho

wanafanya mambo ya kukatisha tamaa - Hao ni wafanya BIASHARA tu kwa


mgongo wa Dini. Soma Neno, Omba, Amini na kutii, bila Kujali ITIKADI

ZA DINI AU DHEHEBU. Kweli itatuweka HURU - Muda si mrefu wengi


watagundua kuwa wamedanganywa, wakiwa wamechelewa.


BABA MUNGU AWABARIKI NA KUWAPATIA SIKU NJEMA YENYE AMANI NA MAFANIKIO
TELE

Na: Eliezer Mwangosi

--
Usikubali kushindwa na ubaya bali ushinde ubaya kwa wema.Waroma12:21

Warema S.Senzia

unread,
Sep 27, 2011, 3:08:20 AM9/27/11
to yourtr...@googlegroups.com
Asante sana kwa neno la leo.
Mwalimu wa Sheria alimuuliza YESU ni amri gani kubwa kati ya hizi 10??? YESU alimwambia ni upendo, upendo kwa MUNGU na upendo kwa jirani yako.(Marko 12:28 -31).  Biblia yasema ukinipenda itazishika amri zangu, hivyo kama tunampenda MUNGU tutazishika amri zake na tutawapenda majirani zetu.
Mwangosi umesema vema jinsi ya kuwatambua manibii wa uongo, siku hizi hata Dar na Tanzania yetu kumeibuka makanisa mengi ambao wachungaji wanazungumza injili ya utajirisho zaidi kuliko toba ya msamaha. Hao manabii na mitume wamekuwa wakishinikiza waumini watoe mali nyingi nao wakiishi maisha ya anasa, wakiendesha magari ya ghali, wakiishi kwa majumba mazuri ya kifahari na kuwaacha waumini wakiishi maisha ya taabu na dhiki. Hili tunaliona na ushuhuda kuwa hao ndio manabii wa Uongo.
 
Asante sana kwa ujumbe wako wa leo, na MUNGU akubariki.
 
"...Surely goodness and love will follow me
all the days of my life, and I'll dwell in the house of the LORD forever"
 

From: YourTrueVine <yourtr...@googlegroups.com>
To: YourTrueVine <yourtr...@googlegroups.com>
Sent: Tuesday, September 27, 2011 8:02 AM
Subject: KUWATAMBUA MANABII WA UONGO

Eliezer Mwangosi

unread,
Sep 27, 2011, 3:43:41 AM9/27/11
to yourtr...@googlegroups.com
Nashukuru kwa Ujumbe,
Kusema ukweli ninayo mengi juu ya mada hii, ila nabanwa na Muda pia Somo la kila asubuhi halitakiwi kuwa Refu, au laa wengi hawatakuwa na Muda wa kutafakari, wakiwa wanawahi Kazi. Inahitaji Muda zaidi ndio maana nimeeleza kwa kifupi.

Mtu yeyote hawezi kuitwa Mkristo halisi bila Kujazwa Roho Mtakatifu. Ukristo Halisi ni Kuzaliwa upya - Kuzaliwa Upya ni kupokea UWEZO / NGUVU ya Roho Mtakatifu. Siku hizi kuna nadharia nyingi za Kujazwa Roho hadi imefikia wengi kutoelewa. Ulimwengu wetu wa sasa Umevamiwa na ROHO MBANDIA sio ROHO Mtakatifu, ROHO Chafu zimejigeuza kuwa malaika wa NURU, na kutenda Kazi kwa HILA, wengi kwa kutosoma NENO la MUNGU wamezipokea bila kujua, ni hakika mizizi ya Dhambi haikomi maishani Mwao. Matendo yao ya SIRI ni Maovu hata kama mbele za watu wanaonekana wamepokea Roho Mtakatifu.

Shetani anafanya usanii huu: Yuko "very strategic" anawapandikiza watu MAGONJWA, UTASA, ANAVURUGA BIASHARA, MIKOSI n.k. HALAFU ANAWAANDAA WATUMISHI KWA KUWAJAZA UPAKO WA KUYAONDOA MAGONJWA HAYO. Nguvu ileile aliyotumia kuyaingiza ndiyo anaitumia kuyaondoa, na wengi hawajui kuwa wanatumika na Nguvu bandia, ndio maana hata ukiwaonyesha ukweli hawaukubali, wanaamini hawawezi kufanya miujiza bila Mungu. YESU ALISEMA "ANGALIENI NIMEKWISHA KUWAONYA MBELE"

MIUJIZA YA KWELI IPO NA ITAENDELEA HADI YESU ATAPOKUJA KUCHUKUWA KANISA - LAKINI MIUJIZA BANDIA ITAKUWA MINGI ILI KUHAKIKISHA HATA WALIO WATEULE WAPOTEE.

KAENI MACHO NI NYAKATI ZA HATARI ZAIDI YA WENGI WANAVYOJUA.

HAVE A NICE DAY.

Eliezer


Ahsante,

J

Salaam,

TAFAKARI:

Na: Eliezer Mwangosi

Important Notice:

The National Bank of Commerce Limited is a registered Commercial Bank in the United Republic of Tanzania.

This e-mail and any files transmitted with it are confidential and intended for the use of the individual or entity to whom they are addressed.

Please note that there are terms and conditions and some important restrictions, qualifications and disclaimers ("the Disclaimer") that apply to this email. To read this click on the following address or copy into your Internet browser:

http://www.nbctz.com/disclaimer/email

The Disclaimer forms part of the content of this email.

Annajoyce Manyanga

unread,
Sep 27, 2011, 4:10:17 AM9/27/11
to yourtr...@googlegroups.com
Kaka Eliezer,

 Namshukuru Mungu wetu wa Mbinguni kwa kukupa nafasi ya kutupa neno la maarifa kama hili,
Kama alivyosema JB ni kweli sasa hivi kumekuwa na usanii mkubwa sana katika makanisa mengi wachungaji wanahubiri habari za utajiri na safari za njeya Nchi wanasahau kuwa watu wa Mungu wanaangamia kwa kukosa maarifa. Maarifa ya Neno la Mungu linasemaje kwa habari ya Dunia hii na vyote vilivyomo.
Mfano wa mchungaji mwema aliowapa Bwana Yesu wameusahau kwamba mchungaji mwema yuko tayari kuutoa uhai wake kwa ajili ya kondoo zake. Leo hii makanisa mengini yanawachungaji wanaoishi kama wafalme maisha ya kifahari zaidi ya kawaida! Kuna wengine wanamiliki mpaka walinzi (Mabausa) Mchungaji mwenye kumtumikia Mungu wa Mbinguni Ulinzi wake ni kutoka kwa Binadamu au uko kwa Mungu?
 
Mungu aendelee kukupa nafasi ya kutulisha Neno lake.
 
 
 
> Date: Mon, 26 Sep 2011 23:02:47 -0700

> Subject: KUWATAMBUA MANABII WA UONGO

Bahati Mashimba

unread,
Sep 27, 2011, 11:06:09 AM9/27/11
to yourtr...@googlegroups.com
Wapendwa Mungu awaongezee rehema,amani na upendano na tuzidi kuleta mafundisho ya neno la Mungu mara tupatapo nafsi ya kufanya hivyo  japo itakuwa ni kwa ufupi lakini naamini tunabarikiwa,yanatusaidia kutafakari juu ya uweza wa injili na pia kukua kiroho.
 
Asanteni kwa somo hili na mi niandike machache.Hatari iliyopo kwa wakristo wengi ni kushindwa kutumia vizuri zawadi ya Roho Mtakatifu.Kujua matunda ya Nabii au Mtumishi wa uongo ni pale utakapokuwa na nuru ya macho ya kiroho zaidi ndipo utaweza kutambua.Tunasoma katika Agano la kale Mungu alijua wana WaIsraeli watapata shida juu ya kutambua Manabii wa uongo  mioyoni mwao  ndipo alipowaambia 'Nawe ukisema moyoni mwako Tutajuaje neno asilolinena BWANA? Atakaponena nabii kwa jina la BWANA, lisifuate jambo lile wala kutimia,HILO NDILO NENO ASILOLINENA BWANA...Kumbu18:21-22. Mungu aliwapa angalizo hilo kama nabii atatabiri juu ya jambo fulani kutokea na lisitokee huyo ni nabii wa uongo.Tunajua habari za Nabii Eliya alishusha moto kutoka mbinguni nanyakati  hizi tunazoishi  wapo manabii wa uongo wanafanya miujiza kama hiyo  na watu wanasadiki kwa sababu ya upofu wao wa kiroho.
Kuna hatua nyingi ambazo mkristo kwa kusaidiwa na Roho Mtakatifu unaweza kujua kama nabii ni wa ukweli au la.Nitaandika baadhi ya matunda ya manabii au walimu wauongo kama yalivyoandikwa katika waraka wa pili wa Mtume Petro kwa watu wote.Sura ya pili inaelezea zaidi juu ya habari ya kuja,nguvu na maangamizi ya manabii na walimu wauongo natabia zao za kuhadaa watu walioanza kutoka kwenye njia ya udanganyifu na kuwarudisha katika njia ya upotevu.
Baadhi ya matendo ambayo wanayafanya  manabii au walimu wauongo ni:-
  1. Wanaingiza uzushi wa kupoteza
  2. Wanafuata ufisadi wao(mafundisho ya kujitajirisha)
  3. Hufuata  mwili kwa mambo machafu
  4. Wakikufuru katika mambo wasiyoyajua
  5. Wenye kuhadaa roho zisizo imara
  6. Wenye macho yajaayo uzinzi
  7. Wanaahidi mafanikio n.k          (Soma 2 Petro2:1-22)
Petro anaelezea uzushi wa kupoteza ambao humkana aliyewanunua.Ukifuatilia kila dini ya  uongo humkiri Kristo kuwa ni mwalimu mkuu lakini  hawampokei kama MWOKOZI  aliyetununua kwa damu ya thamani.Hawawezi kuuweka msalaba (damu ya Yesu) katika mafundisho yao.
 
Wapenzi  msiiamini kila roho bali zijaribuni hizo roho kwamba zimetokana na Mungu kwa sababu manabii wa uongo wengi wametokea duniani.1 Yohana4:1
 
Mungu azidi kutubariki  sote na tuzidi kukua katika neema ya kumjua BWANA wetu Yesu Kristo.
 
 Humble yourselves in the sight of the Lord and he shall lift you up James4:10

From: Annajoyce Manyanga <anne...@hotmail.com>
To: yourtr...@googlegroups.com
Sent: Tuesday, September 27, 2011 10:10 AM
Subject: RE: KUWATAMBUA MANABII WA UONGO

Reply all
Reply to author
Forward
0 new messages