NENO LA LEO

88 views
Skip to first unread message

eliezer.mwangosi

unread,
Dec 19, 2016, 9:55:21 PM12/19/16
to
NENO LA LEO: WATEULE KAENI MACHO
Mathayo 24:24-25 "Kwa maana watatokea makristo wa uongo, na manabii wa uongo, nao watatoa ishara kubwa na maajabu; wapate kuwapoteza, kama yamkini, hata walio wateule. Tazama nimekwisha kuwaonya mbele".

Kama kuna jambo la hatari ambalo Kristo aliliona juu ya watu wake, ni hila za shetani kuuteka ulimwengu wote hadi kuwayumbisha watoto wake Kwa kutumia Ishara, maajabu au miujiza akiwatumia makristo na manabii wa uongo. Wakati tunaoishi ni wa hatari kuliko Wakati mwingine uliowahi kupita, kwa sababu tayari wengi tumezaliwa katika kipindi cha kutimiza unabii.

Anachokifanya shetani kuwanasa wengi; anawatupia watu mishale ya matatizo mfano, magonjwa ya Kila namna yakiwemo, upofu, ukiwete, utasa, homa zisizoisha, UTI, ukichaa, ugonjwa wa matumbo n.k., ugomvi na kuvunja mahusiano au ndoa, mikosi na laana mbalimbali n.k. Matatizo yote yanayoletwa na roho chafu au roho za mashetani, mara nyingi hayaponi kwa dawa za kawaida yaani dawa za hospitali.

Kwa njia za roho za utambuzi, ambazo zinajigawa zingine kwa waganga wa kienyeji au waaguzi na zingine zinawaendea watu wa dini. Hivyo wapagani wanapoenda kwa waganga, wanaambiwa shida zao na roho zilizosababisha matatizo zinaondoka na mtu anakuwa mzima, ila huyo mtu anakuwa katika himaya ya mashetani, make ndiko alikopata tiba yake.

Kwa watu wa dini, shetani anawatumia watu wasiopenda kusimama katika kweli, anawajaza nguvu ya roho bandia, na kuwapatia roho za utambuzi, wakijua Kila chanzo cha matatizo ya watu, ambayo shetani amewaletea, na kwa kutumia biblia na jina la Yesu, wanayaondoa magonjwa kwa namna ya miujiza, Wakati ni shetani mwenyewe, aliyaweka na kuyaondoa, ndipo wengi wakishuhudia huamini kuwa kweli huyu ni nabii wa Mungu, hivyo hata akiwa anafanya UOVU, watu bado wanaamini ni mtumishi.

Katika kipindi hiki cha NEEMA, kila mtu ana uhuru wa kufanya lolote analo ona linampendeza, bila kufanywa lolote, wengi wanachukuliwa mateka na kuangamia kwa kukosa maarifa, falsafa nyingi juu ya kweli za biblia zimetungwa kuwapoteza wengi, wakitumia Ishara na miujiza. Watu wengi leo wanajenga Imani zao katika Miujiza waliyotendewa, hata wakiona wako kinyume na ukweli wa biblia wanasita kufanya matengenezo. Hiyo ndiyo hatari aliyoiona Yesu Kristo.

Zingatia; pamoja na utitiri wa manabii na watumishi feki, bado kuna manabii na watumishi wa kweli, hivyo tunachopaswa kukifanya ni kuwapima kwa neno la Mungu. Ukiona nabii anakataa wokovu kwa Imani katika Kristo sawa na Injili ya Yesu, au kama hafundishi watu Amri za Mungu (Kutoka 20: 3-17) kwa usahihi huyo hajatumwa na Mungu, sio kati ya watakatifu kwa mujibu wa biblia - Soma na kutafakari mafungu haya: Ufunuo 12:17, 14:12,  1Yohana 2:4, Isaya 24:4-6, Marko 7:6-9, Mathayo 5:17-20.

WITO: Yesu anatoa wito wa mwisho, kwa watu wote kufanya matengenezo, hebu kila mmoja watu auhakikishe wokovu wake kwa kutii neno la Mungu chini ya uongozi wa Roho mtakatifu. Usalama wetu ni kujisalimisha kwa Kristo, haijalishi unapitia changamoto zipi, au umejeruhiwa kiasi gani, bado Mungu anaweza kukutoa katika hali unayoipitia.

NAWATAKIA WOTE BARAKA ZA BWANA HASA TUNAPOFIKA MWISHO WA MWAKA.

Na: Ev. Eliezer Mwangosi - Simu 0767 210 299.
Soma na kuutafakari ujumbe huu halafu wapelekee wengine.




Sent from Samsung tablet

eliezer.mwangosi

unread,
Dec 22, 2016, 9:56:23 PM12/22/16
to
NENO LA LEO: HATARI KWA WASAFIRI WA MBINGUNI
Hosea 4:6 "Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa; kwa kuwa wewe umeyakataa maarifa, mimi nami nitakukataa wewe ....."

Maisha na uhai wa watoto wa Mungu unategemea chakula bora cha kiroho,  ambacho ni neno la Mungu. Katika kizazi hiki cha mwisho, shetani amemwaga virusi vya ugonjwa hatari wa KUKOSA HAMU YA KUSOMA NENO LA MUNGU. Wengi wanahisi hawana muda wa faragha na Mungu, huku wakipoteza muda mwingi kwa mambo ya kidunia yasiyo na tija. 

Utakuta vijana na hata watu wazima, wanatumia masaa mengi wakikodolea macho mitandao na kuzijaza akili mambo ya kidunia na uchafu, lakini ukiwatumia waraka wa neno la Mungu, wanakosa hamu ya kusoma, wanaishia ku "like" bila kusoma ujumbe kwa tafakari. Wengine utasikia wanasema "leo umetuma gazeti" yaani ujumbe ni mrefu, wakati wanatumia masaa mengi kuangalia au kusikiliza saiyo na tija kiroho. 

Wengi wanatembea wakiwa marehemu wa kiroho, kwa kukosa muda wa kutafakari neno, wengi wamebeba mapokeo ya wanadamu badala ya neno la Mungu, kwa sababu hawana muda wa kusoma neno la Mungu na kuthibisha wanachoamini, na mwisho wao ni kuangamia. Tunapaswa kukua kiroho kwa njia ya utakaso kwa neno la kweli la Mungu - Yohana 17:17.

Hebu fikiri; toka asubuhi, mchana kutwa, hadi usiku unapolala, unatumia masaa au dakika ngapi kusoma na kutafakari mada za neno la Mungu?  linganisha na muda unaotumia kuperuzi na kuangalia picha, ku chat mambo yasiyo na tija, kupiga story, kukodolea macho wanaopita mbele yako, kushinda umelala, kusoma magazeti na vitabu vya tamthilia, bila kusahau muda wa TV n.k. 

Sikiliza: Dalili za kuwa na gonjwa hili hatari, ni; mtu anapoanza kusoma neno la Mungu anakuwa na hali hizi,  kuhisi usingizi, kusikia uchovu, kutokuwa na hamu, macho kuwa na ukungu, kuanza kuwaza mengine nje ya unachosoma n.k. Ukiona hali hizo au mojawapo kwako .... Chukua hatua ya haraka kupata tiba, hizo tayari ni nguvu za Adui zinatawala. Simama, mwambie Bwana akupatie nguvu mpya, ushindi ni hakika. 

NAWATAKIA SIKU NJEMA YENYE MAFANIKIO TELE

Na: Ev. Eliezer Mwangosi.
Simu: 0767 210 299 - WhatsApp: 0766 99 22 65.




Sent from Samsung tablet

eliezer.mwangosi

unread,
Dec 27, 2016, 10:33:18 PM12/27/16
to
NENO LA LEO: JIPATIE UHURU WA KWELI
Tafakari: Yohana 8:31 "Basi Yesu akawaambia wale wayahudi waliomwamini, Ninyi mkikaa katika neno langu, mmekuwa wanafunzi wangu kweli kweli, tena mtaifahamu kweli; nayo hiyo kweli itawaweka huru."

Miaka kadhaa iliyopita, kulikuwa na kijana mmoja ambaye alikuwa kibaka, yaani mwizi wa mitaani, mara kadhaa alikuwa anapelekwa mahabusu, lakini jambo la ajabu akitolewa anarudia tena kuiba. Baadaye ikaja kugundulika kuwa, anapenda kukaa mahabusu au rumande, kwa sababu pale analala na kula japo ni mahali pabaya kwa kuishi.

Kuna lugha isemayo, za mwizi arobaini, aliporudia kuiba, zikatimia, wananchi wakamkamata na kuamua kumchoma moto hadi mauti. Kuna wengi wameizoea dhambi, japo kwa mionekano yao ni kama wacha Mungu, wakishinda na vitabu vya dini bila kukosa Misa au Ibada na wengine wakifanya kazi ya Mungu hadi ya kuimba, huku wakidumu kuwa watumwa wa dhambi.

Vitendo vya chuki, hila, unafiki, umbea, masengenyo, kutopendana, kutakiana mabaya, kulipa baya kwa baya na visasi, wivu, kutunga uongo, mafarakano, ubinafsi, kujiona, kujikwenza na kupenda sifa, kuingilia ndoa na kuvuruga mahusiano ya wengine, kujiunza, vitendo vya ngono nje ya ndoa, ulevi, wizi na  kupenda kuhongwa n.k. ni tabia za kawaida hata kwa wanaojiita wacha Mungu.

Wito wa Yesu katika tafakari ya leo, ni wote kutoka katika vifungo hivyo vya shetani na kuwekwa huru kabla siku hazijatimia, mazoea hujenga tabia, na uovu huo ukizoeleka inakuwa ni tabia ya mtu. Ni wakati wa kila mmoja kuchukua hatua ya kuishi sawasawa na neno la kweli la Kristo, peke yetu hatuwezi, bali tukimwamini Yesu Kristo na kuruhusu atawale maisha yetu, ushindi ni hakika.

NAWATAKIA SIKU NJEMA YENYE BARAKA TELE.

Na:  Ev Eliezer Mwangosi
Simu: 0766 210 299 na WhatsApp: 0766 992 265.




Sent from Samsung tablet

Bahati Mashimba

unread,
Dec 28, 2016, 10:05:27 PM12/28/16
to yourtr...@googlegroups.com
Amen.God bless you
--------------------------------------------
On Wed, 12/28/16, 'eliezer.mwangosi' via YourTrueVine <yourtr...@googlegroups.com> wrote:

Subject: NENO LA LEO
To:
Date: Wednesday, December 28, 2016, 6:33 AM
--

Mimi ni mzabibu ninyi ni matawi, akaaye ndani yangu nami
ndani yake, huyo huzaa sana; maana pasipo mimi ninyi
hamwezi kufanya neno lolote.Yohana 15:5

---

You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "YourTrueVine" group.

To post to this group, send email to yourtr...@googlegroups.com.

For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

eliezer.mwangosi

unread,
Jan 2, 2017, 10:00:57 PM1/2/17
to
NENO LA LEO - ANZA NA BWANA - 2017
1Petro 5:6-7 "Basi nyenyekeeni chini ya mkono wa Mungu ulio hodari, ili awakweze kwa wakati wake; huku mkimtwika yeye fadhaa zenu zote, kwa maana yeye hujishughulisha sana kwa mambo yenu."

Nilikuwa nikipitia salaam za mwaka mpya, karibia wote walitakiana KHERI, yaani meema. Ni kawaida kila mwaka unapoisha na kuanza mwaka mpya kutakiana mema, lakini kiuhalisia wengi wanakiri mambo yanabaki vilevile, japo kwa wengine yanaweza kuwa mabaya zaidi au mazuri.

Hebu jaribu kuangalia, maisha ya tarehe 31 Desemba 2016 na hali ya maisha baada ya kuanza 2017; je ni tofauti? watu wengi mifuko imepwaya zaidi, huku wenye nyumba wakidai kodi, bila kusahau ada za shule na mahitaji ya watotot n.k. Heri ya mwaka mpya imeishia wapi? mbona mwaka unaanza na pasua kichwa?

Hata hivyo, wengi wakikumbuka mapito ya mwaka 2016, wanakiri, kama si Mungu, wasingefika salama 2017, ingawa kuna waliopita kwa machungu, wapo pia walioishi kama wako peponi, hata hivyo wote tunamshukuru Mungu tumevuka.

Neno la leo linatukumbusha jambo muhimu na la busara sana, kusalimisha maisha yetu kwa Mungu, ambaye hujishughulisha sana na mambo yetu, ingawa wengi hawajui, kumbuka; uhai tulio nao, afya zetu na mali zote, mwenye maamuzi ya mwisho ni Mungu. Na kadiri tunavyosogea mwisho wa nyakati, maisha bila Mungu ni sawa na kujilisha upepo.

Bila kujali uliyoyapitia mwaka jana au yanayoendelea, yawe ni majeraha au maumivu ya mahusiano, ya ndoa, ya ukata wa fedha, ya kukosa ajira, ya kunyanyaswa, ya kuporwa mume au mke, ya biashara, ya magonjwa sugu, ya mikosi na laana na kila aina ya fadhaa ... Mungu anasema mtwikeni yeye.

Mwaka 2017, unaweza tu kuwa tofauti na 2016, pale tutakapoamua kubadili mtazamo juu ya ahadi za Mungu, ambaye ndiye tu awezae yote, na kutazama upya mipango ya maisha, chini ya uongozi wa Mungu. Tukisalimisha maisha yetu na mipango yetu kwa Mungu, tutakuwa salaama, au laa shetani ataendelea kujeruhi na kutesa wengi.

NAWATAKIA BARAKA TELE MNAPOANZA MWAKA NA BWANA

Na: Ev. Eliezer Mwangosi
Simu: 0767210299 - Ya WhatsApp: 0766 992 265.




Sent from Samsung tablet
Reply all
Reply to author
Forward
0 new messages