BIBLE STUDY - KRISTO ALIKUWA WAPI KABLA YA KUJA DUNIANI?

368 views
Skip to first unread message

Saimon

unread,
Feb 28, 2011, 7:47:13 AM2/28/11
to YourTrueVine
Mpendwa rafiki katika kristo nashukuru Mungu kwa neema yake mimi na
wewe tu wazima na anaendelea kutubariki katika shughuli zetu za kila
siku.Naomba tushiriki pamoja katika kujifunza biblia japo kwa dakika
chache kila wiki ili tuzidi kumjua Mungu vizuri na kuishi maisha ya
mfano wa Kristo.
Tutakuwa tunajifunza kwa kuuliza maswali au kujibu maswali
yaliyoulizwa na mwana mzabibu wako wa kweli au wewe unaweza kuandika
somo lako sehemu ya Subject kwenye email yako nauanze kichwa cha somo
BIBLE STUDY - Kisha andika wazo kuu la somo lenyewe kisha tuma kwenye
yourtr...@googlegroups.com

Mpendwa mkristo katika maisha yetu ya kawaida tumekuwa tukijifunza
mambo mbalimbali ili kuendana na hali halisi ya ukuuaji wa
tekenolojia.Ni mara chache tumekuwa tukipata muda wa kujifunza biblia
peke yetu au na wakristo wenzetu.

Mpendwa mkristo tunatakiwa tujifunze neno la Mungu ili tuweze kumjua
Mungu vizuri zaidi,ili tuweze kuufuata mfano wa Kristo kwani sisi tu
wanafunzi wake, ili tuweze kuwaeleza wengine habari za Kristo na ili
tuzidi kukua kiroho.

Nafikiri ni jambo muhimu kwangu na kwako na kwa Mkristo kujifunza
maisha ya Yesu Kristo.

Mpendwa rafiki katika Kristo kwa juma hili tujadiliane wote juu ya
swali hapo juu KRISTO ALIKUWA WAPI KABLA YA KUJA DUNIANI?

Jibu la swali hili linapatikana katika injili ya Yohana1:1 tunasoma
'Hapo mwanzo kulikuwako Neno naye Neno alikuwa Mungu'

Katika mstari huo Kristo alikuwa wapi kabla ya kuja kwake hapa
ulimwenguni?

Kwa msaada wa kuelewa zaidi naomba tusome Yohana1:14 'Naye Neno
alifanyika mwili,akakaa kwetu nasi tukauona utukufu wake,utukufu kama
wa Mwana pekee atokaye kwa Baba,amejaa neema na kweli'.

Neno alifanyika mwili maaana yake Neno alifanyika mwanadamu.Mwana
pekee atokaye kwa Baba ni Yesu Kristo.kwahiyo Neno ni Yesu Kristo.

Mpendwa unakaribishwa kutoa ufafanuzi zaidi juu ya jambo hili kwa
namna unavyoelewa.

Asante

Mungu akubariki na kukulinda.

Saimon(BEM)

James Malima

unread,
Feb 28, 2011, 8:32:47 AM2/28/11
to yourtr...@googlegroups.com
Naamini kabisa kwamba kwa mujibu wa Yohana, hilo ndo jibu sahihi. Hili jina Yesu limekuja katika agano jipya baada ya Mariamu kupata mimba kwa uweza wa Roho Mtakatifu na kumzaa Yesu. Kabla ya hapo, Yesu, kama nafsi ya pili ya Mungu, na kabla ya kuvaa mwili, ili aweze kutukomboa kutoka katika dhambi zetu, alikuwa akijulikana kama Neno la Mungu.
 
Ni muhimu sana kwa Mkristo yoyote, msingi wake kuwa ni Neno la Mungu. Kama jinsi Mungu alivyo, kwamba habadiliki, ukilishika Neno la Mungu, unakuwa umemshika Mungu mwenyewe. Watu wengi siku hizi wanavutwa na miujiza, matokeo yake wamejikuta kuangukia mikononi mwa Manabii wa uwongo.
 
Neno la Mungu ndio Yesu mwenyewe, na tukilishika Neno, basi tunakuwa tumemshika Yesu mwenyewe. Ukristo, kwa kifupi, ni kuishi kwa kufuata mfano na tabia za Yesu alivyokuwa hapa duniani.
 
Mbarikiwe sana.
 
Malima

2011/2/28 Saimon <bmas...@gmail.com>

--
Humble yourselves in the sight of the Lord and he shall lift you up James4:10



--
James Joseph Malima

E-mail: James....@gmail.com
Phone: +255 754 845 613 - Mobile

"If you fail to plan,..... you're planning to fail"

Saimon

unread,
Mar 2, 2011, 1:53:42 AM3/2/11
to YourTrueVine
Asante sana James kwa ufafanuzi wako ni kweli Neno la Mungu ndio Yesu
Kristo mwenyewe na tukilishika Neno la Mungu tutakuwa tumemshika
Yesu mwenyewe na Yesu atakuwa ndani yetu kwani yeye ni mzabibu wa
kweli na sisi tu matawi ya mzabibu.
Maisha ya Kristo haya kuanza wakati alipozaliwa hapa duniani kama
mtoto mchanga kwani yeye ni Neno na alikuwako kwa Mungu na alifanyika
mwili kama tulivyoona kwenye Yohana1:1, na 14.

Kuna dini nyingi ambazo siyo wakristo zimekuwa zikijaribu kupotosha
ukweli huu.Kwahiyo mimi na wewe inabidi tuwaeleze wengine habari za
Yesu kuwa kabla ya kuja hapa duniani alikuwa kwa Mungu na hata baada
ya kufanyika mwili wa kinadamu huko Bethlehemu yeye ni Neno na ni
Mungu.

Tuone neno la mwanafunzi wa Yesu aitwaye Filipo alinena maneno haya
kwa Yesu ''BWANA,utuonyeshe Baba, yatosha.Yesu akamwambia,Mimi
nimekuwako pamoja nanyi siku hizi zote,wewe usinijue, Filipo?
Aliyeniona mimi(Yesu) mimi amemwona Baba(Mungu),basi wewe
wasemaje ,utuonyeshe Baba(Mungu)? '' Yohana 14:8 -9.Katika maneno haya
Kristo,maana ya Baba ni Mungu.Kwahiyo tunapo jua habari za Kristo
tunajua habari za Mungu.

Neno la Mungu linatuambia kwamba Mungu ni pendo.Yesu Kristo
alituonyesha upendo wa Mungu katika maisha yake.Yesu aliwapenda watu
wote,watoto,wenye dhambi,matajiri,maskini,wenyekazi,wavuvi na
wagonjwa.

James kama ulivyoeleza 'Ukristo, kwa kifupi, ni kuishi kwa kufuata
mfano na tabia za Yesu alivyokuwa hapa duniani' Ni kweli ili tuweze
kuishi maisha ya kufuata mfano na tabia za Kristo ni lazima tujifunze
maisha yake.
Wakati Yesu alipokuwa hapa duniani alituonyesha mambo mengi yaliyo
mema.Tunapokuwa na tatizo yatupasa tufikiri juu ya maisha ya Kristo
alifanya nini juu ya tatizo kama hili.

BWANA akubarikie na kukulinda.

Saimon(BEM)



On Feb 28, 3:32 pm, James Malima <james.mal...@gmail.com> wrote:
> Naamini kabisa kwamba kwa mujibu wa Yohana, hilo ndo jibu sahihi. Hili jina
> Yesu limekuja katika agano jipya baada ya Mariamu kupata mimba kwa uweza wa
> Roho Mtakatifu na kumzaa Yesu. Kabla ya hapo, Yesu, kama nafsi ya pili ya
> Mungu, na kabla ya kuvaa mwili, ili aweze kutukomboa kutoka katika dhambi
> zetu, alikuwa akijulikana kama Neno la Mungu.
>
> Ni muhimu sana kwa Mkristo yoyote, msingi wake kuwa ni Neno la Mungu. Kama
> jinsi Mungu alivyo, kwamba habadiliki, ukilishika Neno la Mungu, unakuwa
> umemshika Mungu mwenyewe. Watu wengi siku hizi wanavutwa na miujiza, matokeo
> yake wamejikuta kuangukia mikononi mwa Manabii wa uwongo.
>
> Neno la Mungu ndio Yesu mwenyewe, na tukilishika Neno, basi tunakuwa
> tumemshika Yesu mwenyewe. Ukristo, kwa kifupi, ni kuishi kwa kufuata mfano
> na tabia za Yesu alivyokuwa hapa duniani.
>
> Mbarikiwe sana.
>
> Malima
>
> 2011/2/28 Saimon <bmashi...@gmail.com>
> E-mail: James.Mal...@gmail.com
> Phone: +255 754 845 613 - Mobile
>
> "If you fail to plan,..... you're planning to fail"- Hide quoted text -
>
> - Show quoted text -
Reply all
Reply to author
Forward
0 new messages