Binadamu huenda tu huko na huko kama kivuli;Hufanya ghasia tu kwa ajili ya ubatili;Huweka akiba wala hajui ni nani atakayeichukua. Zaburi 39:6
Maisha ya mkristo huanzia hapa duniani kwa kuamini jina la Yesu Kristo na mwisho wake ni kwenye mji mtakatifu Yerusalemu mpya.Tunaona watu wengi ambao ni wakristo walivyo busy wa kienda huko na huko kutafuta utajiri kwa njia mbalimbali ikiwa ni pamoja na njia halali na wengine wanatumia njia haramu za wizi, uaji, unyang'anyaji, ufisadi, kshirikina na njia zote mbaya wanazoweza kuzitumia ili waweze kupata utajiri.Utajiri wa mali ni haki ya kila mkristo anayeishi kwa kufuata misingi ya neno la Mungu.
Wapo wanaosabisha ghasia katika jamii, ndugu, kanisa na hata taifa kwa sababu wamebaka haki za watu kwa tamaa zao binafsi za kuwa na utajiri kwa njia haramu.Biblia inatuhimiza hao wanaoweka akiba ya utajiri wao hapa duniani hawatajua nani atachukua mali zao na zitaendelezwaje baada ya kufa kwao.Mtu hatachukua mali zake kwenda nazo kaburini au kuingia nazo kwenye ufalme wa Mungu.
Sisi wakristo tunapoendelea kuishi kwa neema ya BWANA,na pia namna BWANA wetu anavyotubariki katika kazi na biashara zetu halali tukumbuke kuwekeza muda wetu, pesa zetu, mali zetu, maisha yetu kwa BWANA maana tutavuna uzima wa milele.
Baraka za Bwana wetu Yesu Kristo ziwe nanyi daima.
Happiness Mashimba