NENO LA LEO

81 views
Skip to first unread message

eliezer.mwangosi

unread,
Jul 26, 2017, 10:47:36 PM7/26/17
to
NENO LA LEO: MAISHA SIO MSTARI ULIONYOOKA
Isaya 66:14 "Nanyi mtaona, na mioyo yenu itafurahi, na mifupa yenu itasitawi kama majani mabichi; na mkono wa BWANA utajulikana, uwaelekeao watumishi wake, naye atawaonea adui zake ghadhabu."

Kumbuka maisha sio sawa na mstari ulionyooka, wengi wanapopitia changamoto wanakata tamaa na kuvunjika moyo, wanafumba macho ya mioyo yao na kiona giza tu likitanda mbele ya maisha yao. Israeli walipitia hali hiyo, mara kwa mara, walipo asi walichukuliwa mateka na kuteswa na maadui zao, kila laana ilikuwa juu yao, lakini wakati ulifika neema ya Mungu iliwafunika na kuwaokoa.

Hata leo hii kuna watu wanapitia changamoto, mioyo imevunjika, hawaoni suluhu ya matatizo yao, kuna mizigo mizito mioyoni mwao, wala hawaoni mwisho wake, huenda wamefunga na kuomba bila mafanikio. Wengine wanatamani maneno ya faraja hawapati, wanatafuta wa kuwajali hawaoni, mioyo imejaa simanzi, wanaishi ili mradi bora liende.

Sikiliza; kuna Mungu anayetawala yote, anayeweza yote, neno lake halibadiliki. Lolote unalolipitia lina mwisho wake. Ni kukosa wa kukubembeleza? ni kukosa mwenzi wa maisha? Ni hujuma za mapenzi na mafakano katika ndoa au uchumba? ni magonjwa? ni masomo? ni kazi? ni hali mbaya ya kiuchumi? ni kutengwa au kuonewa? Ni mapito gani unayapitia?

Wewe unayepitia mapito na wewe unayekula maisha, jueni kuwa maisha sio sawa na mstari au ubao ulionyooka, kwa wakati usioudhani hali inabadilika. Mungu ndiye atawalaye na mwenye hatma ya maisha yetu. Wale wanaoumizwa na wenzi wao, au wanaoteswa na wenye uwezo, au wanao onewa na mashetani na umizimu, Bwana ameahidi kuinua ghadhabu juu yao.

Ukisoma Isaya 66:12-13 ... Bwana ameahidi kutupatia AMANI, kutubembeleza na kutupakata miguuni pake, ameahidi kutufariji na kutupatia furaha. Hebu na tuzidi kumtumaini yeye, awezaye kuganga mioyo iliyovunjika, na kukosa AMANI. Kwa wakati tusioudhani Bwana atalitimiza neno lake kwako.

NAKUTAKIA SIKU YENYE FURAHA NA AMANI TELE - BWANA AKUBARIKI.

Na: Ev. Eliezer Mwangosi - Simu: +255 0766 992265 ya WhatsApp.
Email: Eliezer....@yahoo.com & Twitter: EliezerMwangosi

PATA MASOMO ZAIDI KUPITIA
Website: www.mwangosi.com
Blog: evmwangosi.blogspot.com
Instagram: evmwangosi




Sent from Samsung tablet

Bahati Mashimba

unread,
Jul 27, 2017, 3:40:37 PM7/27/17
to yourtr...@googlegroups.com
Amina mtumishi ...Ubarikiwe sana na BWANA

On 7/27/17, 'eliezer.mwangosi' via YourTrueVine
> --
> Mimi ni mzabibu ninyi ni matawi, akaaye ndani yangu nami ndani yake, huyo
> huzaa sana; maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya neno lolote.Yohana
> 15:5
> ---
> You received this message because you are subscribed to the Google Groups
> "YourTrueVine" group.
> To post to this group, send an email to yourtr...@googlegroups.com.
> For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
>

eliezer.mwangosi

unread,
Aug 3, 2017, 1:11:50 AM8/3/17
to
NENO LA LEO: UHAKIKA WA KUPATA USHINDI

1Yohana 4:4 "Ninyi, watoto wadogo, mwatokana na Mungu nanyi mmewashinda, kwa sababu yeye aliye ndani yenu ni mkuu kuliko yeye aliye katika dunia."

Katika mapito ya maisha haya, kila mtu anapitia hali fulani ya mapambano ambayo hatimaye anatakiwa kuyashinda. Baada ya anguko la dhambi, kila mtu anayezaliwa, mbele ya maisha yake kuna pambano la aina fulani, kwa sababu adui shetani hapendi watu walioumbwa na Mungu waishi maisha AMANI na MAFANIKIO siku zote.

Utasikia wengine wanasema "Mimi sijapitia mapito yoyote, kila kitu ninacho, afya, mali, elimu, ndoa, watoto, kazi vyote Mungu kanipa" na anashangaa kwa nini wengine wanapitia maisha ya shida. Mtu kama huyo, hajui kuwa 'HUJAFA HUJAUMBIKA', wakati wowote utamkuta analia baada ya kujeruhiwa na adui.

Mara nyingi shetani anawatumia watu kujeruhi wenzao, 'hivi wewe mvulana uliye mwacha mchumba baada ya kumchezea, unafikiri umemwacha salama? na, ninani aliyekutuma ufanye hivyo?, wazushi wote, wambea, wanaotelekeza familia, wachonganishi, waonevu, wachawi, wanaopendelea na kubagua watu, wanyanyasaji na wanaosababisha machungu kwa wenzao ni siraha za shetani katika vita ya kiroho.

Neno la leo, linatukumbusha kuwa tunamshinda shetani na vibaraka wake kwa sababu tunaye Mungu aliye ndani yetu "Sio aliye nje" ambaye ni mkuu kuliko shetani, wewe unayepitia machungu sasa, kumbuka yupo Mungu aliye mkuu zaidi ya MAPITO hayo. Simama kwa Imani mwambie yeye, nawe utapita SALAMA.

NAWATAKIA WOTE SIKU NJEMA YENYE USHINDI MKUU

Na Ev. Eliezer Mwangosi

Soma zaidi kupitia:
www.mwangosi.com
evmwangosi.blogspot.com




Sent from Samsung tablet

Bahati Mashimba

unread,
Aug 3, 2017, 4:39:45 AM8/3/17
to yourtr...@googlegroups.com
Amina ,Ubarikiwe sana mtumishi katika shamba la Bwana kwa ujumbe wa ushindi


--
Mimi ni mzabibu ninyi ni matawi, akaaye ndani yangu nami ndani yake, huyo huzaa sana; maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya neno lolote.Yohana 15:5
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "YourTrueVine" group.
To post to this group, send email to yourtr...@googlegroups.com.

eliezer.mwangosi

unread,
Aug 8, 2017, 5:32:48 PM8/8/17
to
NENO LA LEO: FAIDA YA KUSULUBISHA MACHO

Mathayo 18:9 "Na jicho lako likikukosesha, ling'oe, ukalitupe mbali nawe; ni afadhali kuingia katika uzima una chongo, kuliko kuwa na macho mawili, na kutupwa katika jehanamu ya moto."

Mtume Paulo anatoa tafsiri ya Ukristo halisi, au wokovu halisi kuwa ni Kuusulibisha mwili wa dhambi na kufufuka na mwili mpya katika Kristo. Warumi 6:6 "mkijua neno hili, ya kuwa utu wetu wa kale ulisulibishwa pamoja naye, ili mwili wa dhambi ubatilike, tusitumikie dhambi tena;" Soma pia Wagalatia 2:20 "Nimesulibiwa pamoja na Kristo; lakini ni hai; wala si mimi tena, bali Kristo yu hai ndani yangu; ...."

Watu wengi wanadai ni wakristo, au wameokoka, au wacha Mungu, wakati ki uhalisia, bado viungo vyao viko hai katika dhambi. Leo tunaangalia kiungo cha MACHO. Kila tamaa mbaya inatokana na macho, macho ni kati ya kiungo ambacho kinatumiwa na shetani kuwatenga Watu na Mungu wao, kwa kuwaingiza kwenye dhambi.

Kwa kutazama tunabadilika, umezoea kutazama nini; ndivyo tabia yako inaumbika. Mfalme Daudi aliingiwa na pepo la zinaa alipomuangalia mke wa Uria akiwa uchi akioga, hadi akazini naye ... 2Samweli 11:2-4, Daudi akajitenga na Mungu kwa tendo hilo dakika chache tu. Hata leo wengi wamenasa na pepo la Zinaa na Uasherati, bila kisahau WIZI, WIVU, Tamaa mbaya n.k. kwa sababu ya kiungo MACHO.

Macho yanayotazama picha za Ngono au Ponograph, mabinti wanaotembea huku sehemu za siri zikiwa nje nje kama wanyama, Mabinti wanaotazama kwa kuzungusha macho utafikiri ya kinyonga, wanaotembea kwa kubinua na kuzungusha makalio utafikiri tairi za isuzu, yote hayo ni mitego ya KUNASA MACHO yasiyosulibiwa yapagawe na roho chafu za ngono.

Daudi alikili akisema "Sitaweka mbele ya macho yangu neno la uovu" - Zaburi 101:3, na baadaye alipoona yeye kwa akili yake hawezi akasema "Unigeuze macho yangu NISITAZAME visivyofaa, unihuishe katika njia yako" Zaburi 119:37. Wachungaji, manabii, watumishi na wapendwa, wengi wamenasa kwa KOPE za wadada, kama Sulemani anavyo onya - Mithali 6:25. "Usiutamani uzuri wake moyoni mwako; Wala usikubali akunase kwa kope za macho yake."

Wapendwa marafiki zangu, tunaweza kushinda uovu wote utokanao na TAMAA ya macho, kwa kuamua kusulubisha kiungo hiki MACHO, yaani kuyasalimisha macho kwa Kristo, ili yafe kwa tamaa ya mwili na yahuishwe kwa mambo matakatifu chini ya utawala wa Roho matakatifu. Hebu kila mmoja ajiulize, macho yake yanatazama nini? kama yanapenda UOVU huo ni mtego wa adui umeshanasa, hayo macho hayajasulibishwa, yatakuangamiza.

NAWATAKIA SIKU NJEMA YENYE MAFANIKIO TELE

Na: Ev. Eliezer Mwangosi (+255 0766 992 265)
www.mwangosi. com
evmwangosi.blogspot.com




Sent from Samsung tablet

eliezer.mwangosi

unread,
Aug 9, 2017, 10:41:32 PM8/9/17
to
NENO LA LEO: KUSULIBISHA MASIKIO

Mithali 17:4 "Mtenda mabaya husikiliza midomo ya uovu;Na mwongo hutega sikio lake kusikiliza ulimi wa madhara."

Kama tulivyoona jana juu ya kusulibisha macho, leo tunaangalia kiungo kingine MASIKIO, kwa kusikia mtu anajengwa tabia au anaharibu tabia. Siku moja nilishuhudia mtoto mchanga, akitikisa kichwa na miguu baada kufunguliwa music kwa sauti ya juu, kumbe kila siku dada wa kazi anashindia kusikikiza music akiwa naye. 

Ubongo wa mtoto huyo umejazwa Bongo flavour na ndiyo itakuwa mazoea na hatimaye tabia yake. Masikio ni njia pana inayolisha ubongo na kuukuza kitabia, ukizoea kusikiliza matusi, utakuwa na tabia ya kutukana, ukizoea kisikiliza music wa SENGELI, kila wakati utajikuta unaimba na kutembea kisengeli.

Pia kuna watu ambao masikio yao yamenyanyuka juu kama ya sungura, muda wote yametega kusikiliza na kunasa vimaneno kama antena, na kusambaza, watu wakiongea au mtu akiongea na simu, anatega sikio, akinasa tu hatulii anaenda kusambaza na kuvumisha maneno, hao ndio huitwa wambea, kila mara kusutwa. 

Shetani anatumia masikio kuharibu tabia za wengi, utamsikia mtu anasema, nimesikia ila sina uhakika; huo ni uovu, kwa nini usikilize na usambaze maneno yasiyokuhusu na huna uhakika nayo?. Bila kuyasalimisha masikio kwa Kristo, maovu mengi yatakuwa ni tabia ya mtu. Mtume Paulo anasema "Basi vifisheni viungo vyenu vilivyo katika nchi ...." Wakolosai 3:5.

UOVU mwingi unakuwa mazoea na tabia ya binadamu kwa sababu ya masikio, tangia utoto unachokisikia ndicho kinakuwa tabia yako, sikio ni kiungo cha pekee kinachokuumbia tabia. Kwa masikio unaweza kujitenga na Mungu na kwa masikio unaweza kuokolewa na kula mema ya nchi

Sikiliza: "Imani chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la Kristo" Warumi 10:17. Hebu kila mmoja ajiulize antena za masikio yake zina nasa mawimbi gani? kama ni mawimbi ya music bongo fleva na aina zake, ubongo utajaa hayo na tabia zingine chafu. 

Neno la leo linamalizia kwa kusema; "Yeye aligeuzaye sikio lake asiisikie sheria, hata sala yake ni chukizo" Mithali 28:9. Wengi wamejitenga na Muumba wao bila kujua, kwa sababu ya kutosulibisha masikio yao, wakayaacha yanase uchafu, wamejitenga na baraka za Bwana, wamenaswa na adui. Maombi yao yanishia hewani, na hatimaye kukosa matumaini.

Hii ni nafasi nyingine tena ya kila mmoja kutafakari, ni wapi masikio yake yanahitaji matengenezo, Yesu alikufa kwa ajili yetu, huu ni wakati wa kukomboa mateka, na kupatanishwa na Baba yetu. USHINDI NI HAKIKA. 

Neema ya Yesu Kristo, na Upendo wa Mungu Baba na Ushirika wa Roho Mtakatifu, ukae nasi sote sasa na hata milele. 

NAWATAKIA SIKU YENYE FURAHA NA BARAKA TELE

Na: Ev. Eliezer Mwangosi
Reply all
Reply to author
Forward
0 new messages