NENO LA LEO

96 views
Skip to first unread message

eliezer.mwangosi

unread,
Jan 15, 2017, 9:33:57 PM1/15/17
to
NENO LA LEO: WEWE BADO NI WA THAMANI
Isaya 43:4-5 "Kwa kuwa ulikuwa wa thamani machoni pangu, na mwenye kuheshimiwa, nami nimekupenda; Kwa sababu hiyo nitatoa watu kwa ajili yako; na kabila za watu kwa ajili ya maisha yako".

Siku moja nikiwa katika kazi ya kuhubiri Injili, nilibahatika kukutana na dada mmoja aliyekuwa amekata tamaa na kukosa matumaini katika maisha. Nilipomuambia habari za Yesu, akacheka kwa kujidharau, akidai yeye hana thamani, kwa wanadamu na kwa Mungu pia, wala hawezi kuwa na thamani tena. 

Akadai kuwa yeye pale alipo ameathirika, anasumbuliwa na magonjwa kwa muda mrefu, jamii inamnyanyapaa, umri umekwenda bila kuwahi kuolewa, anatamani angalau awe na familia lakini tayari anaona imeshakuwa jioni, umri umesogea, giza linaingia. Hivyo hataki kusikia habari zozote zinazohusu maisha, anatamani afe yaishe.

Wapendwa; bila kujali unapitia hali gani, ambayo inaweza kukufanya usijione wa thamani, kwa jamii au watu unaokaa nao, iwe nyumbani au ofisini, kwa mumeo au mkeo, kwa marafiki au ndugu - Mbele za Mungu wewe ni wa thamani na bado kuna tumaini.  

Mpendwa; Watu wanaweza wasikuthamini, wala kukuheshimu au kukupenda, kwa sababu yoyote ile, iwe tabia yako mbaya, au dhambi, au magonjwa, au hali ya kutojiweza kiuchumi, au maumbile yako yalivyo au kwa sababu yoyote ile, Mungu anasema: Wewe ni wa thamani, anakuheshimu na anakupenda. 

Kama Mungu alivyowapenda waisraeli, wangali wakiwa waovu chini ya utumwa wa farao na hatimae kuwakoa, bila kusahau tendo la Yesu kutupenda na kuja kutukomboa kwa damu yake ya thamani, tungali ni waovu, hatuna budi kujisikia wa thamani mbele za Mungu sawasawa na ahadi zake. 

Hebu kila mmoja wetu akajawe na matumaini tena katika siku ya leo, bila kujali hali unayopitia wala watu wanakuonaje, kaza macho kutazama ahadi za Mungu, yeye ataujaza moyo wako tumaini kuu na kubeba haja zako. 

NAWATAKIA SIKU NJEMA YENYE KUJAA AMANI NA TUMAINI KUU. 

Na: Ev. Eliezer Mwangosi - Simu: 0767 210 299, WhatsApp: 0766 992 265.




Sent from Samsung tablet

eliezer.mwangosi

unread,
Jan 17, 2017, 10:07:38 PM1/17/17
to
NENO LA LEO: TENDA UTENDEWE
Mathayo 7:12 "Basi yo yote myatakayo mtendewe na watu, nanyi watendeeni vivyo hivyo; maana hiyo ndiyo torati na manabii."

Katika jamii zote ni kawaida watu kutaka kutendewa haki, au kutendewa matendo mema na wenzao, lakini kwa bahati mbaya, wengi wanaotaka kutendewa hayo, wao wenyewe hawatendi haki kwa wenzao.

Wengi wanajidai wacha Mungu, wakihudhuria kila Ibada makanisani na masjid, lakini roho zao zimejaa ukakasi wa kuonea na kutotenda haki kwa wenzao. Kuoneana kunaanzia majumbani kwa wanandoa, kwa wajakazi, hadi maofisini, kila kona haki ni bidhaa adimu.

Wengi hawapendi kudhulumiwa, kunyanyaswa, kukalipiwa, kuonewa, kusengenywa, kutungiwa uongo, kidhalilishwa, na kutofanyiwa jambo lolote baya. Lakini wao wenyewe wanakuwa wa kwanza kuwafanyia wengine roho mbaya.

Kumbuka: Mungu yuko makini na kila analolitenda mtu kwa binadamu mwingine, kuna siku litamrudia tena katika hali mbaya zaidi ili apate fundisho. Ni hakika, Kila mtu atalipwa ujira wa kile alichomtendea mwenzake, iwe ni jema au baya.

Kwa wale wanaotendewa ubaya; tambueni kisasi ni cha Mungu, jambo la busara ni kumpelekea mashitaka Mungu, wala msilipe ubaya kwa ubaya, ndipo Baba wa mbinguni atawafungulia baraka tele.

MUNGU AWAPATIE MAISHA YENYE AMANI NA BARAKA TELE

Na: Ev. Eliezer Mwangosi - 0766 99 22 65




Sent from Samsung tablet

Bahati Mashimba

unread,
Jan 17, 2017, 11:59:17 PM1/17/17
to eliezer.mwangosi, YourTrueVine
Amina.Tu wathamani sana machoni pa Mungu

Bahati Mashimba

unread,
Jan 18, 2017, 12:25:25 AM1/18/17
to yourtr...@googlegroups.com
Amen


On 1/18/17, 'eliezer.mwangosi' via YourTrueVine
> --
> Mimi ni mzabibu ninyi ni matawi, akaaye ndani yangu nami ndani yake, huyo
> huzaa sana; maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya neno lolote.Yohana
> 15:5
> ---
> You received this message because you are subscribed to the Google Groups
> "YourTrueVine" group.
> To post to this group, send an email to yourtr...@googlegroups.com.
> For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
>

eliezer.mwangosi

unread,
Jan 18, 2017, 10:35:06 PM1/18/17
to
NENO LA LEO: TAFSIRI YA SHETANI JUU YA UPENDO
1Yohana 4:7-8 "Wapenzi, na tupendane; kwa kuwa pendo latoka kwa Mungu, na kila apendaye amezaliwa na Mungu, naye anamjua Mungu. Yeye asiyependa, hakumjua Mungu, kwa maana Mungu ni upendo. 

Kati ya mambo ambayo shetani ameyatumia vibaya ili kuwanasa, na kuwajeruhi wengi ni neno UPENDO. Shetani ameharibu akili za vijana na wazee kwa kutumia neno hili upendo, wengi wameshindwa kujua tofauti kati ya upendo wa kweeli na tamaa ya macho au mwili. Mtu akiambiwa NAKUPENDA, nati zote za mwili zinalegea, bila hata kujua nini kinafuata.

Wengi wamepitia maumivu yasiyoisha, hadi kufikia kujijutia nafsi, kwa sababu tu ya kuukubali upendo feki wa tamaa za ngono, uliokuja kama upendo wa kweli. Vijana wengi wanaanzisha uchumba wa kichina (Feki), na unaishia kwa kuumizana, bila kusahau ndoa zinazogeuka ndoano, yote ni kwa sababu ya kutojua maana sahihi ya Upendo unaoanzisha mahusiano.  

Utasikia kijana anasema; "Naamini hunipendi" eti sababu kakataliwa Ngono. Hivyo tafsiri ya shetani ya neno Upendo au kupenda kwa watu wa jinsia tofauti ni kutimiza tamaa za Mahaba au kudunguana maembe, wakati tafsiri ya Mungu ni kutii AMRI za Mungu ikiwemo ya "USIZINI" au kuwa na tabia ya Mungu - 2Yohana 1:6.

Hebu kila mmoja ajihoji, ni upendo gani uliowaunganisha? au ni upendo gani unaoendelea kati yao? Nani anautawala, ni Mungu au yule mzee wa mkuzimu? Mahusiano yako na huyo unayemwita sweteee au mchumba au hawala, boy friend, babeee au yeyote unayeishi naye na kufanya naye ngono, NJE AU KABLA YA NDOA HALALI, unafikiri mwisho wake ni upi? Usidanganyike huo ni mtego na umeshanasa. 

Bado mlango wa wokovu wa kweli ungali wazi, vijana kwa wazee wanaalikwa kuingia, kwa maana usiku umeendelea sana na pambazuko la kheri liko karibu. Bado tumaini la kumshinda shetani lipo kwa wote wanaosalimisha maisha yao kwa Mwokozi. 

Mtajeruhiwa na muovu shetani hata lini? kujiita, mkristo, nimeokoka, mpendwa, mcha Mungu, mwimbaji, nambii, mtumishi na kuhudhuria kila huduma za ibada na maombi, havina maana kama mkuu wa giza ndiye anayetawala maisha. 

NAWATAKIA SIKU NJEMA YENYE KUJAA WEMA WA MUNGU

Na: Ev. Eliezer Mwangosi 
Mawasiliano: 0767 210 299 - WhatsApp - 0766 99 22 65
Utabarikiwa ukiwasambazia wengine ujumbe huu. 




Sent from Samsung tablet

eliezer.mwangosi

unread,
Jan 26, 2017, 10:49:01 PM1/26/17
to
NENO LA LEO: NI CHUNGU LAKINI NDIO TIBA
Waebrania 4:12 "Maana Neno la Mungu li hai, tena lina nguvu, tena lina ukali kuliko upanga uwao wote ukatao kuwili, tena lachoma hata kuzigawanya nafsi na roho, na viungo na mafuta yaliyomo ndani yake; tena li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo."

Ni kawaida ya binadamu kupenda kuambiwa mambo mazuri, yanayofurahisha moyo, mfano kusifiwa au kuambiwa maneno yasiyokinzana na matakwa yake. Watu wengi wanachukia wanapoambiwa ukweli ili wajirekebishe wanapokosea, ndio maana waswahili wakaishia kusema "UKWELI UNAUMA". Iwe ofisini, kwenye biashara, majumbani watu hawapendi kukosolewa, au kambiwa ukweli pale wanapokwenda tofauti.

Kwa bahati mbaya sana tabia hii imetanda hata kwa watu wanaodai ni watu wa Mungu, katika kizazi hiki cha giza nene la mioyo iliyojaa uovu, watu hawapendi kuambiwa neno la Mungu linalokosoa tabia zao zilizo kinyume na mapenzi ya Mungu, wengi wanapenda maneno laini,  vichekesho, baraka, mafanikio na yanayofanana na hayo. Neno la maonyo na kukemea dhambi linazidi kuadimika masikioni mwa wanadamu.

Hata kwenye mitandao, mtu akirusha ujumbe wa kidunia, mfano: Binti akapiga picha yenye kuacha embe dodo nusu wazi, au akaonyesha maungo ya makalio, hata kama ni ya kuazima kwa wachina, halafu akaandika na ujumbe usemao "Sema neno moja tu", utashangaa comment zikimiminika utafikiri mvua. Lakini mtu akituma ujumbe wenye kuleta uzima, wanapita au ana bofya "like" bila hata kusoma na kutafakari.

Kazi ya neno ni kufanya "operation" au upasuaji ili kugawanya mwili (nafsi) na roho, yaani kukata na kutupa nje mazoea ya mwili na kuunganisha tabia ya Kristo kwa njia ya Roho mtakatifu. Sijawahi kuona mtu akifanyiwa upasuaji, katika machungu ya kisu, eti anacheka mwanzo mwisho, au mtu anameza dawa ya chloroquine huku anacheka. Lakini siku hizi,  mahubiri mengi na yanayopendwa na wengi ni ya wenye dhambi kurudi nyumbani na dhambi zao, huku wakidai wamebarikiwa kwa vichekesho na jumbe laini za baraka. Lengo la wahubiri wengi ni kutaka kupendwa na kujikusanyia sadaka, huku watu wakibaki chini uovu.

Zingatia: Ukiona umehubiriwa na umesikia au umesoma neno la Mungu, na ukaona liko tofauti na unayopenda kuyafanya, au linakosoa unachokiamini, na ukasikia kuumia moyoni, unapaswa kumshukuru Mungu, hilo ndilo lengo la neno la Mungu. Ulimwengu unazidi kuwa chini ya laana ya dhambi, kwa sababu watu hawako tayari kuonywa na kuambiwa ukweli kupitia neno la Mungu.

HEBU MUNGU AMSAIDIE KILA MMOJA AWEZE KUSHINDA

NAWATAKIA SIKU NJEMA YENYE KUJAA BARAKA ZA BWANA.

Na: Ev. Eliezer Mwangosi
Simu: 0767210299 na WhatsApp - 0766992265.




Sent from Samsung tablet

eliezer.mwangosi

unread,
Feb 2, 2017, 6:57:57 PM2/2/17
to
NENO LA LEO - USIJALI MUNGU YUKO PAMOJA NAWE
Matendo ya mitume 7:9-10 "Wale wazee wetu wakimwonea wivu Yusufu, wakamwuuza aende misri. Mungu akawa pamoja naye, akamtoa katika dhiki zake zote, akampa fadhili na hekima mbele ya farao, mfalme wa Misri; naye akamfanya awe mtawala juu ya misri na nyumba yake yote".

Ni jambo la kawaida kushuhudia baadhi ya watu wakipitia changamoto zinazosababishwa na watu wenye tabia ya WIVU, kama Yusufu alivyofanyiwa na ndugu zake. Wivu ni tabia chafu ya shetani, inayomfanya mtu ajisikie vibaya juu ya mafanikio ya mtu mwingine, ni hali ya mtu kuumia moyoni kwa mafanikio ya wengine.

Dhambi ya wivu ni mshale wenye sumu anaotumia shetani kuwatesa wengi, tabia ya wivu huambatana na masengenyo, kuzua uongo, maneno ya hila, kuteta, kubeza, kuchonganisha, kwa nje wanaweza kuonekana ni marafiki na wanakupenda, kumbe ndani kunafuka moto. Kila wakati wanakuwa na mawazo hasi juu ya wengine na kuwatakia kushindwa.

Nilishuhudia mama mmoja aliyesababisha binti kuachwa na mchumba, kwa kumtungia na kueneza sifa mbaya, akishuhudia uongo kuwa si mwaminifu, na ndivyo hata ndoa nyingi zinavyoyumba kama sio kusambaratishwa, bila kusahau wivu maofisini, mashuleni, Makanisani, kwenye biashara, hata mtu akinunua nguo nzuri, utashangaa wanapokutana wanamsifia, akiwapa kisogo tu wanabinua midomo ya kubeza. Maneno ya kusemana vibaya hayaishi kwa sababu ya tabia hii ya WIVU.

ATHARI: Wale wote wenye tanzi hii ya wivu, wanaokerwa na mafanikio ya wengine, hawatafanikiwa, na mwisho watakufa kimwili na zaidi sana kiroho, kwa sababu wanafanya kazi ya adui shetani. Neno linasema "Kwani hasira humwua mtu mpumbavu, nao WIVU humwua mjinga" Ayubu 5:2, ndio maana waswahili wakaishia kusema "Mwenye WIVU ajinyonge".

USIOGOPE: Kwa wote wanaopitia changamoto za kuonewa wivu na watu wengine, kwa mafanikio ya aina yoyote, yawe ya kimwili au ya kiroho, kupitia neno la leo, wakumbuke kuwa Mungu yupo kwa ajili ya kuwashindia, kama Yusufu alivyotolewa katika dhiki hadi utawala, ndivyo itakavyokuwa kwa kila mmoja, atakayefanyiwa hila kwa WIVU atakavyotoka kwa ushindi mkuu. Bwana yuko upande wako, wewe ni mshindi daima .... USIOGOPE.

WEMA WA MUNGU UMZUNGUKE KILA MMOJA WETU APATE KUUSHINDA WIVU

NAWATAKIA SIKU NJEMA YENYE MAFANIKIO NA BARAKA TELE.

Na: Ev. Eliezer Mwangosi
Simu: 0767 210 299 na WhatsApp - 0766 992 265




Sent from Samsung tablet

Bahati Mashimba

unread,
Feb 2, 2017, 7:15:10 PM2/2/17
to YourTrueVine, eliezer.mwangosi
Amina.Ubarikiwe na Bwana

Mtoka James

unread,
Feb 2, 2017, 10:47:06 PM2/2/17
to yourtr...@googlegroups.com

Amen mtumishi barikiwa sana

Reply all
Reply to author
Forward
0 new messages