NENO LA LEO

107 views
Skip to first unread message

eliezer.mwangosi

unread,
Oct 19, 2017, 11:30:53 PM10/19/17
to weddym...@gmail.com, csend...@yahoo.com, cjk...@yahoo.co.uk, emap...@yahoo.co.uk, ana...@hotmail.co.uk, zaina...@yahoo.com, elig...@yahoo.co.uk, annas...@yahoo.com, chec...@yahoo.co.uk, Buhatwa Ladislaus, debok...@yahoo.com, damar...@ymail.com, elyta...@yahoo.com, Arusha Reception, anne...@hotmail.com, ant...@gmail.com, Dat...@scitz.com, Emmyk...@gmail.com, dai...@diamondtrust.co.tz, ema...@serena.co.tz, emie...@yahoo.com, deoma...@yahoo.com, ymt...@hotmail.com, devon...@yahoo.com, emmy...@yahoo.com, bar...@yahoo.com, alfredb...@yahoo.com, bngan...@yahoo.com, apbw...@yahoo.co.uk, ckiiz...@yahoo.com, answ...@yahoo.co.uk, emba...@yahoo.com, ester...@yahoo.com, Evel...@gmail.com, annie...@yahoo.com, elijahc...@yahoo.com, Edesia Kahyarara, epiphania...@yahoo.com, deri...@yahoo.com, Andyni...@yahoo.com, yourtr...@googlegroups.com, Erick...@hotmail.com, Brig...@gmail.com, bmas...@gmail.com, cella...@yahoo.co.uk, bmt...@gmail.com, Dorah....@tigo.co.tz, aak...@hq.bot-tz.org, benson...@yahoo.com, berna...@gmail.com, evam...@yahoo.co.uk
NENO LA LEO - VIJANA NA MAISHA YA MAHUSIANO

 MADA:  HATUA NA NJIA ZA KUPATA MCHUMBA

Katika semina ya leo tutajifunza mambo yafuatayo
1. Sehemu ya Mungu katika Mahusiano na Uchumba
2. Hatua za Msingi kufikia Uchumba hadi Ndoa
3. Suluhisho la changamoto unayoipitia

1. Sehemu ya Mungu katika Mahusiano na Uchumba.
Katika masomo yaliyotangulia tuliona mambo yafuatayo:

- Mahusiano ni hali ya mtu au kundi la watu kufanya jambo fulani na mtu au kundi lingine kwa kusudi maalumu. Ni hali ya kuwa pamoja kwa ajili ya jambo fulani ... Mfano: Mwalimu na wanafunzi, wana michezo, nchi moja kuwa na ubalozi nchi nyingine, wachumba, wanandoa n.k.

- Mungu ndiye mwanzilishi wa Mahusiano, kati yake na Adam kwa kumuumba kuanza kumpatia maelezo, na baadaye kuanzisha mahusiano kati ya Adam na Hawa. Alimuumba Adam na Hawa kwa mfano wake, na kuwapatia maagizo ya kutawala - Mwanzo 1:27-28, 2:7, 16, 20.

- Mungu alimpatia Adam Mwenzi, wa kufanana naye - Mwanzo 2:21-23, ni Mungu alimtwalia Adamu mke, ili awe msaidizi, katika kutimiza makusudi yake Mungu, akawapatia agizo la KUZAA, ambalo lilihalalisha tendo la Ndoa, kati ya Jinsia ya Kiume na ya Kike. Mwanzo 1:28

 Hapo tunaona katikati ya Adam na Hawa yupo Mungu, ambaye ndiye anayewaunganisha. Hivyo ni Mungu pekee anayejua, ni nani amempatia kusudi fulani na nani anaweza kumsaidia kutimiza kusudi hilo. Yesu alisisitiza akasema "Basi alichokiunganisha Mungu, mwanadamu asikitenganishe". Marko 10:9.

- Kwa mtu anayejitambua, Ndoa ni muungano wa watu wawili na kuwa mmoja katika Mungu. Tofauti na hapo hizo ni Bora Ndoa, zenye kujengwa katika misingi iliyopasuka. 

- Ni kazi na mikakati ya Shetani kuhakikisha, ndoa zote zinaanzishwa na yeye, nje ya mpango wa Mungu, ili aendelee kuzijeruhi hapa duniani na hatimaye Jehanamu. 

TAHADHARI KWA WANAOJITAMBUA: 
Shetani anaweza kukuanzishia ndoa na ikaonekana kufanikiwa hapa duniani, lakini lengo lake kuu ni kuhakikisha mnaishia Jehanam. Ni heri ukae bila kuoa au kuolewa kama Paulo, kuliko kuingia kwenye ndoa, iliyo kinyume na mapenzi ya Mungu. 

Hivyo mtangulize Mungu asilimia 100, katika mchakato wote wa kumpata mwenzi, Omba kwa Imani, Ongea na Mungu, mfanye awe rafiki ili ujue kusudi na mapenzi yake kwako. Anajua kukupatia kilicho chema, usipopata kwa wakati jua ana makusudi mema nawe, hawezi kukupatia vitu vibovu. 

2. HATUA MUHIMU ZA KUFIKIA UCHUMBA HADI NDOA

a) (Public / Social zone) Mahusiano ya awali, hatua ya kwanza ni Kukutana, hii ni hatua ya kwanza ya mahusiano. Sehemu mnayokutana na kufahamiana na watu, na kuzoeana, mara nyingi inachangia kumpata mwenzi. Yaani huanzisha mahusiano ... Mfano: Chuoni, Kazini, kwenye michezo, Kanisani n.k.

Sehemu mnayofahamiana na watu, na kuanza mahusiano, inasaidia kujua na kufahamu maisha ya Mtu, Kwenye disco, kwenye baa, kwenye kwaya, kanisani, kwa waganga wa kienyeji ... wapi mnaonana? 

Itumie nafasi hii kuwafahamu watu vizuri, bila kuwa na hisia zozote za kuanzisha uchumba. 

b) (Personal zone) Urafiki
Hii ni hatua ya pili inayoweza kukuanzishia safari ya uchumba bora, katika mahusiano yakawaida, pale mnapokutana ... Mfano. Chuoni, ni lazima kutakuwa na Mtu au watu wachache wa Karibu, inaweza kuwa wa Jinsia moja au tofauti. Hii ni sehemu ya kuwa mwangalifu, na unayefanya naye urafiki. 

Mara zote mahusiano ya urafiki yana kua na kukomaa kwa kadiri mnavyopendana na kuhudumiana. Hii ni sehemu ya kuzifahamu tabia za watu kwa undani. Mtu anaweza kuwa na marafiki wengi, atawafahamu wengi. 

Ikitokea marafiki ni wa jinsia tofauti ni rahisi, sana kuanza kuunganisha hisia za mapenzi, sehemu hii sio ya kumtamkia mtu Uchumba, hata kama una wazo hilo, kaa nalo, endelea kuomba Mungu aongoze kufahamu zaidi, tabia, familia, anachopenda n.k.

Kumbuka Urafiki sio Uchumba, hao wana uhusiano wa ndani kama kaka dada katika Kristo. Usiruhusu faragha, maneno na matendo yanayoashiria ngono, messages na picha za kingono ... zote hizo ni mitego ya Ibilisi. 

c) (Intimate zone)Rafiki Mpenzi / Mpenzi. 
Hatua hii ni ya juu sana zaidi ya kuwa rafiki wa kawaida, ni watu walioshibana, haijalishi jinsia zao, maneno haya yalitumika hata kwa wapendwa katika Kristo ... mitume walilitumia kwa washirika wao wa karibu ..

Mungu aliliita kanisa lake Mpenzi - Yeremia 11:1512:7. Pia watumishi wa Mungu waliitana WAPENZI - 3Yohana 1:51:11, Warumi 16:5, 9, 12. Hivyo neno hili halimaanishi mapenzi ya Kimahaba kama wengi wanavyojua. 

Ukiingia katika hatua hii na jinsia tofauti, chunga sana, ni rahisi kuingia katika Ngono. Chukua tahadhari, mara nyingi katika hatua hii, msipoonana unajisika umepungukiwa, unahisi kuna utupu katika moyo. Kwa mwanamke ni rahisi kujihalalishia uchumba kabla ya kutamkiwa. 

Hatua hii bado sio uchumba, wala haipaswi kumwambia, bado ni wakati wa kufahamiana zaidi, kabla ya kutamka. Huu ni wakati wa kuhakiki kila jambo kabla ya kutamka unataka awe mchumba. Wahusishe wazazi kabla unapoona huyo anakufaa, ili wakushauri.  

Usiingie hatua hii ukiwa KIPOFU WA MPENZI, wengi ndipo wanaangukia pua, mabinti wengi wanalia wakiachwa ... huyo sio mchumba, mko huru kuachana. Jiulize ana kidhi vigezo vya kuwa mwenzi kwa mpago wa Mungu?

d) Mchumba
Hii ni ni sehemu, ambayo watu wawili, wameamua na kukubaliana kuwa wawe mwili mmoja. Wakiwa marafiki wa kawaida walifanya kila njia kuchunguzana, na kujilidhisha kwa mapana. 

Wazazi na ndugu wanatakiwa wawe wamehusishwa na kutoa ushauri, kabla ya kutamka kuwa unataka awe wako. Wengi wanasumbuana na wazazi, na wengine hujitangazia uchumba kabla ya wazazi kupatiwa nafasi ya kutoa ushauri  .... NI HATARI. 

Mkipata kibali cha kuwa wachumba, ndipo mnaweza kutangaza kuwa ni wachumba. Hapa hakuna kuchunguzana tena, ni kupanga mipango ya ndoa. 

MAKOSA MAKUBWA KWA VIJANA WENGI

- Ni kosa kutangaza uchumba, halafu ndipo eti wachunguzane, hilo ni kosa, nani ataonyesha madhaifu ili asiolewe? Kuchunguzana na kufahamiana ni wakati, hakuna anayejua kuwa watakuwa wachumba, wakati wa urafiki wa kawaida. 

- Ni kosa, kudai Tendo la Ndoa kwenye Uchumba, au Urafiki, HAKUNA TENDO LA UCHUMBA. Ni kinyume na mpango wa Mungu, ni kujiondoa katika ulinzi na ushirika wa Mungu. Ni kusalimisha mahusiano yenu kwa Ibilisi, ambaye mwisho wake ni majeraha. 

- Ndoa za mwendo KASI, kuzaa na kuishi pamoja katika hatua ya uchumba, hizo ni bora ndoa, hawajitambui, wakati wowote, Ibilisi yuko huru kuwarushia mishale, kuwatenganisha, kuwarushia mapepo ya Ngono, ugomvi, na kila laana .... 

e) NDOA
Kama tulivyoeleza katika masomo yaliyotangulia, NDOA ni kuweka maagano ya wawili waliopendana, mwanaume na mwanamke, kuwa wameamua kuunganishwa kuwa mwili mmoja, kulingana na mpango wa Mungu, na kwa taratibu za kisheria zilizopo, zinazoongoza jamii kulinda haki za ndoa.

Mungu anabariki maagano yao, na hatimaye kufungua rasmi mpango wa uzazi wenye furaha kupitia TENDO LA NDOA. Nguo nyeupe ya Bibi harusi, kama kitani safi, inaashiria kwamba hajawahi KUCHAFULIWA na mwanaume mwingine ... ni BIKRA safi wa kupendeza anayekutana na Mwanaume aliye SAFI bila kuchafuliwa na viruka njia. 

USHAURI:
Kwa WANAOJITAMBUA, wanaume kwa wanawake, wana nafasi ya kujenga misingi imara katika kuanzisha NDOA chini ya Utaratibu wa Mungu. INAWEZEKANA. 

Wanaume:
Inawezekana kuishi bila Ngono hadi siku ya Ndoa, wako akina Yusufu, Daniel, Eliya, Enoko na wengine wengi walioshinda enzi zile,  leo hii katika Roho na Kweli inakuwaje ishindikane? Hata Hivyo ni uchaguzi wenu Kuvuna UPEPO nje ya Mungu au Kuvuna Baraka ndani ya Mungu. 

Jisikieni Fahari kuoa MABIKIRA, jitambueni, kung'ang'ania kula tunda kabla, ni kueneza umalaya ambao, kwa kawaida wote hawaupendi. 

MABINTI:
Badilikeni, jithamini, msiwe chumvi ya kuonjwa na kutupwa, ni short kutolewa usichana na mwanaume asiye kuoa, na wakati wa Harusi unavaa SHELA JEUPE ... 

Msikubali kutembelewa na mende wa chooni wenye lengo la kuchafua na kukimbia,  anayedai anakupenda huju akitaka Ngono, HAKUPENDI, BALI ANAKUTAMANI. 

Wapelekee wengine ujumbe huu - UTABARIKIWA

MUNGU AWABARIKI VIJANA NA WAZAZI WOTE KWA KUZINGATIA UJUMBE HUU. 

Na. Ev. Eliezer Mwangosi





Sent from Samsung tablet
Reply all
Reply to author
Forward
0 new messages