MWALIKO

26 views
Skip to first unread message

eliezer.mwangosi

unread,
Sep 11, 2016, 3:06:14 PM9/11/16
to
MWALIKO WA KUSHIRIKI BARAKA ZA BWANA:

Mathayo: 9:35-36 "Naye Yesu alikuwa akizunguka katika miji yote na vijiji, akifundisha katika masinagogi yao, na kuihubiri habari njema ya Ufalme, na kuponya magonjwa yote na udhaifu wa kila aina. Na alipowaona makutano, ALIWAHURUMIA ......."

Kumbuka: Tuko hai leo kwa kusudi maalumu la kumtukuza Mungu na kuwasaidia wengine wanaoteseka.

Nachukua nafasi hii kukushirikisha wewe kama mmoja wa watoto wa Mungu kushiriki katika mpango wa kusaidia wengine waliochoka na wanaoteseka, kama ilivyokuwa wakati wa Yesu, ndivyo ilivyo hata leo, wengi zaidi wanahitaji mkono wa msaada, wamekosa amani na matumaini katika ulimwengu huu.  

Katika kutimiza kusudi la Yesu la Kuokoa na kusaidia wanaoteseka, tumeandaa mkakati wa kuisaidia jamii ya  wilaya ya Mkuranga, kwa mkutano wa neno la Mungu utakaoendesha huduma zifuatazo kwa wiki tatu kuanzia Tarehe 8 hadi 29 Octoba 2016. ENEO LA KISEMVULE. Mkutano huu ni wa watu wote, bila kujali Dini wala madhehebu.

Mhubiri wa Habari NJEMA ni mimi: Ev. Eliezer Mwangosi.

Kusudi la Mkutano ni: KULETA AMANI NA MATUMAINI MAKUU KATIKA JAMII

Kauli mbiu yetu ni KUPIGA VITA mambo yafuatayo:
1. UOVU NA UVUNJIFU WA MAADILI
Mfano: Ujamabazi, Ulevi wa aina zote, Ubakaji, Mafarakano, Uonevu, Ndoa kuvunjika, Mauaji, Uchawi na Ushirikina, Ugaidi n.k.

2. UMASKINI NA MAISHA TEGEMEZI

3. MAGONJWA YATOKANAYO NA MTINDO WA MAISHA
Mfano: Saratani, Kisukari, Shinikizo la Damu, Kiharusi, Ukimwi, Misongo n.k.

4. MAFARAKANO KATIKA FAMILIA
Mfano: Kuvunjika ndoa, kutelekeza watoto, tabia mbaya za watoto, kuvunjika uchumba n.k.

HUDUMA ZITAKAZOTOLEWA KWA WIKI 3:
1. Mafundisho ya Neno la Mungu, kuirudisha jamii kwa Mungu awezaye kubadili tabia za watu.
     - Kuombea wagonjwa, wanaoteseka na nguvu za mashetani na wenye shida mbalimabali ili Mungu awaweke huru.

2. Kuendesha semina ya Ujasiliamali bure, na elimu ya namna ya kufanikiwa katika maisha kwa ujumla.

3. Kutoa elimu ya kuzuia magonjwa tishio Kisukari, Saratani, Kiharusi, Ukimwi n.k. Kwa kubadili mtindo wa maisha na Chakula au Lishe.

- Kupima Afya Bure hasa Kisukari, Presure, Uzito n.k.
- Kupata ushauri na elimu bure ya kidaktari kwa matatizo yoyote ya kiafya yayoikumba jamii.

4. Kutoa Ushauri nasaha juu familia zenye Mafarakano au changamoto zozote, na mtu yeyote anayepitia misongo ya maisha.

5. Kutoa misaada kwa makundi maalum ya wahitaji mfano: vituo vya watoto yatima.

6. Kuhamasisha jamii juu ya kuchangia Damu kwa ajili ya kusaidia wanaoteseka katika hospitali kwa kukosa Damu.

7. Pia tutaiomba serikali ya eneo husika ije itoe elimu ya usalama kwa jamii.

ILI KUFANIKISHA HUDUMA HII YA KUSAIDIA NA KUOKOA JAMII, UNAOMBWA KUCHANGIA CHOCHOTE UNACHOWEZA KATI YA HIVI:
1. Fedha kwa ajili kununulia vifaa vya Afya, kulipa watalaamu, chakula, malazi, usafiri, mahema nk.
2. Misaada ya Nguo, chakula, nk.
3. Mahema na viti - Tunatumia uwanja wa Mpila.

Kwa yeyote atakayekuwa tayari kuchangia huduma hii, nitaomba tuwasiliane kwa maelezo zaidi - juu ya utaratibu wa kutuma pesa au vifaa au kupata maelezo zaidi, wasiliana na wahudumu wafuatao:

Ev. Eliezer Mwangosi - Simu: 0767210299, Email: eliezer....@yahoo.com.
Pastor Kibunto - Simu: +255 769 337 471
Ev. Ezrony Monde - Simu +255 787988 885

Mungu awabariki wote kwa moyo wa kupenda kuisaidia jamii yetu inayoteseka.

Wenu katika shamba la Bwana Ev. Eliezer Mwangosi

Wapelekee wengine mwaliko huu wa kushiriki Baraka za Bwana bila kujali Dini au dhehebu ni kwa watu wote.




Sent from Samsung tablet
Reply all
Reply to author
Forward
0 new messages