NENO LA LEO

144 views
Skip to first unread message

eliezer.mwangosi

unread,
Mar 8, 2018, 11:24:46 PM3/8/18
to aak...@hq.bot-tz.org, ester...@yahoo.com, annie...@yahoo.com, cella...@yahoo.co.uk, emie...@yahoo.com, Arusha Reception, bmas...@gmail.com, elijahc...@yahoo.com, bngan...@yahoo.com, evam...@yahoo.co.uk, devon...@yahoo.com, ckiiz...@yahoo.com, emmy...@yahoo.com, Andyni...@yahoo.com, benson...@yahoo.com, emba...@yahoo.com, damar...@ymail.com, epiphania...@yahoo.com, bmt...@gmail.com, elig...@yahoo.co.uk, Erick...@hotmail.com, Dat...@scitz.com, Buhatwa Ladislaus, berna...@gmail.com, weddym...@gmail.com, csend...@yahoo.com, Emmyk...@gmail.com, answ...@yahoo.co.uk, alfredb...@yahoo.com, annas...@yahoo.com, ana...@hotmail.co.uk, debok...@yahoo.com, emap...@yahoo.co.uk, chec...@yahoo.co.uk, dai...@diamondtrust.co.tz, yourtr...@googlegroups.com, deri...@yahoo.com, anne...@hotmail.com, deoma...@yahoo.com, ant...@gmail.com, elyta...@yahoo.com, Edesia Kahyarara, apbw...@yahoo.co.uk, Evel...@gmail.com, bar...@yahoo.com, cjk...@yahoo.co.uk, Dorah....@tigo.co.tz, zaina...@yahoo.com, ema...@serena.co.tz, ymt...@hotmail.com
NENO LA LEO - UDANGANYIFU KATIKA MAHUSIANO NI SAWA NA KULA CHANGARAWE.

Mithali 20:17 "Chakula cha uongo ni kitamu kwa mtu; Lakini halafu kinywa chake kitajaa changarawe"

Mithali hii inamaanisha kuwa, mara nyingi mtu anaweza kunufaika kwa maneno ya udanganyifu lakini mwisho wake, aliyedanganya na aliyedanganywa wanadhurika, matokeo ya uongo, udanganyifu au hila ni madhara sawa na mtu anayejikuta anatafuna changarawe badala ya chakula.

Vijana wengi na hata wazee, wakike na wakiume, wamejikuta wanatafuna changarawe au kokoto, badala ya UTAMU wa mapenzi walioanza nao, wengi wamejeruhiwa na wenzi wao waliojidai wanawapenda, kumbe wana mapenzi ya hila na udanganyifu.

Japo kuna wavulana wanao TOSWA na mabinti, tena wengine baada ya kuwagharamia hata masomo, lakini asilimia kubwa ya majeraha ni mabinti, wavulana wengi ni wadanganyifu, japo wanaanza kwa mahaba mubashara, wanaishia kujeruhi na kuumiza.

Neno la leo, linawaonya vijana wa kiume na mabinti, UONGO una madhara kwa wote wawili, japo wavulana wanajiona wana uhuru wa Kuharibu na kutafuta wengine, LAANA ya udanganyifu inawafuata hadi kwenye ndoa zao, vivyo hivyo kwa wasichana wadanganyifu.

Vijana; muombeni Mungu, msidanganye wala kudanganywa. Mabinti usikubali mahusiano ya ku "PASS TIME", muda ukipita haurudi na huku sifa za Ubinti zikizidi kuyoyoma. Usikubali kuwa chombo cha KITULIZO, ndani ya shimo la udanganyifu ... UTAUMIA.

Kumbuka; kisasi ni cha Mungu kwa kila aliyemuumiza mwenzie, na yeyote aliyetendwa, Bwana atamtegemeza.

MUNGU AWAPATIE SIKU NJEMA YENYE MIANZO MIPYA.

## Wapelekee wengine ujumbe huu ##
## Nipatie namba za wengine wanaohitaji NENO LA LEO ##

Na: Ev. Eliezer Mwangosi
Simu: 0767 210 299
evmwangosi.blogspot.com

Sent from my Samsung Galaxy smartphone.

Bahati Mashimba

unread,
Mar 8, 2018, 11:28:11 PM3/8/18
to Eliezer Mwangosi, ana...@hotmail.co.uk, Erick...@hotmail.com, Dorah....@tigo.co.tz, devon...@yahoo.com, cella...@yahoo.co.uk, dai...@diamondtrust.co.tz, berna...@gmail.com, Andyni...@yahoo.com, ema...@serena.co.tz, Buhatwa Ladislaus, damar...@ymail.com, Arusha Reception, ant...@gmail.com, csend...@yahoo.com, annas...@yahoo.com, Emmyk...@gmail.com, alfredb...@yahoo.com, emie...@yahoo.com, zaina...@yahoo.com, yourtr...@googlegroups.com, Dat...@scitz.com, elig...@yahoo.co.uk, bmt...@gmail.com, aak...@hq.bot-tz.org, Edesia Kahyarara, deri...@yahoo.com, debok...@yahoo.com, emmy...@yahoo.com, deoma...@yahoo.com, benson...@yahoo.com, ymt...@hotmail.com, bar...@yahoo.com, answ...@yahoo.co.uk, elyta...@yahoo.com, Evel...@gmail.com, chec...@yahoo.co.uk, epiphania...@yahoo.com, anne...@hotmail.com, weddym...@gmail.com, emba...@yahoo.com, annie...@yahoo.com, bngan...@yahoo.com, apbw...@yahoo.co.uk, ckiiz...@yahoo.com, elijahc...@yahoo.com, ester...@yahoo.com, emap...@yahoo.co.uk, cjk...@yahoo.co.uk, evam...@yahoo.co.uk

Amen Ubarikiwe sana na Bwana azidi kukupa nafasi ya kutulisha kwa neno la uzima.

eliezer.mwangosi

unread,
Mar 18, 2018, 11:57:46 PM3/18/18
to aak...@hq.bot-tz.org, ester...@yahoo.com, annie...@yahoo.com, cella...@yahoo.co.uk, emie...@yahoo.com, Arusha Reception, bmas...@gmail.com, elijahc...@yahoo.com, bngan...@yahoo.com, evam...@yahoo.co.uk, devon...@yahoo.com, ckiiz...@yahoo.com, emmy...@yahoo.com, Andyni...@yahoo.com, benson...@yahoo.com, emba...@yahoo.com, damar...@ymail.com, epiphania...@yahoo.com, bmt...@gmail.com, elig...@yahoo.co.uk, Erick...@hotmail.com, Dat...@scitz.com, Buhatwa Ladislaus, berna...@gmail.com, weddym...@gmail.com, csend...@yahoo.com, Emmyk...@gmail.com, answ...@yahoo.co.uk, alfredb...@yahoo.com, annas...@yahoo.com, ana...@hotmail.co.uk, debok...@yahoo.com, emap...@yahoo.co.uk, chec...@yahoo.co.uk, dai...@diamondtrust.co.tz, yourtr...@googlegroups.com, deri...@yahoo.com, anne...@hotmail.com, deoma...@yahoo.com, ant...@gmail.com, elyta...@yahoo.com, Edesia Kahyarara, apbw...@yahoo.co.uk, Evel...@gmail.com, bar...@yahoo.com, cjk...@yahoo.co.uk, Dorah....@tigo.co.tz, zaina...@yahoo.com, ema...@serena.co.tz, ymt...@hotmail.com
NENO LA LEO: SUBIRI, WAKATI  WAKO UTAWADIA

1Samwel 1:20 "Ikawa, wakati ulipowadia, Hana akachukua mimba na kuzaa mtoto mwanamume; akamwita jina lake Samweli, akisema, Kwa kuwa nimemwomba kwa BWANA."

Neno la leo linatukumbusha kisa cha Hana mke wa Elkana ambaye alipitia hali ya kubezwa, alidharauliwa, alichekwa na kuteseka kwa maneno ya kejeri, kwa sababu ya kutofanikiwa kuzaa mtoto. Alikaa kwa muda mrefu bila kupata mimba wakati mke mwenza Penina alifanikiwa kuwa na watoto, ambaye muda wote alikuwa anamchokoza kwa maneno ya dhihaka.

Wakati ulipowadia Bwana akamkumbuka, Hana akapata mimba na hatimaye kuzaa mtoto Samwel, kwa wakati asioujua, huzuni zake zote zikakoma, japo ilichukua muda mrefu, Bwana akatimiza kusudi lake kwa Hana, dharau na kubezwa vikakoma.

Ni hakika siku ya leo kuna mmoja anapitia mapito kama ya Hana, inawezekana ni kutopata watoto, huenda ni kukaa muda mrefu bila kupata mwenza wa maisha, huenda ni changamoto ya kazi, huenda ni mapito ya magonjwa, inawezekana ni mateso katika ndoa, inawezekana ni janga la watoto kusombwa na dunia, huenda kuna jambo ambalo sasa linaenda kuwa fedheha kwa jamii, na unaomba na sasa ni muda mrefu huoni  nuru mbele yako.

Sikiliza, haijalishi tatizo lako limedumu muda mrefu kiasi gani bila kupata majibu, haijalishi tatizo ni kubwa kiasi gani, neno la leo linasema, kwa wakati usioujua, wakati UTAKAPOWADIA, Bwana ATAKUKUMBUKA. Dumu kumtazama na kumtumaini yeye siku zote, kama Hana alivyofanya, yeye Bwana ni mwaminifu ATATENDA, naye atafanya njia pasipo njia.

MUNGU AZIDI KUKUFUNIKA KWA WEMA WAKE. UWE NA SIKU NJEMA.

Na: Ev. Eliezer Mwangosi
Simu: 0767 210 299
Tovuti: evmwangosi.blogspot.com.
FB: Ev Eliezer Mwangosi.

eliezer.mwangosi

unread,
Mar 19, 2018, 11:50:42 PM3/19/18
to aak...@hq.bot-tz.org, ester...@yahoo.com, annie...@yahoo.com, cella...@yahoo.co.uk, emie...@yahoo.com, Arusha Reception, bmas...@gmail.com, elijahc...@yahoo.com, bngan...@yahoo.com, evam...@yahoo.co.uk, devon...@yahoo.com, ckiiz...@yahoo.com, emmy...@yahoo.com, Andyni...@yahoo.com, benson...@yahoo.com, emba...@yahoo.com, damar...@ymail.com, epiphania...@yahoo.com, bmt...@gmail.com, elig...@yahoo.co.uk, Erick...@hotmail.com, Dat...@scitz.com, Buhatwa Ladislaus, berna...@gmail.com, weddym...@gmail.com, csend...@yahoo.com, Emmyk...@gmail.com, answ...@yahoo.co.uk, alfredb...@yahoo.com, annas...@yahoo.com, ana...@hotmail.co.uk, debok...@yahoo.com, emap...@yahoo.co.uk, chec...@yahoo.co.uk, dai...@diamondtrust.co.tz, yourtr...@googlegroups.com, deri...@yahoo.com, anne...@hotmail.com, deoma...@yahoo.com, ant...@gmail.com, elyta...@yahoo.com, Edesia Kahyarara, apbw...@yahoo.co.uk, Evel...@gmail.com, bar...@yahoo.com, cjk...@yahoo.co.uk, Dorah....@tigo.co.tz, zaina...@yahoo.com, ema...@serena.co.tz, ymt...@hotmail.com
NENO LA LEO: WAJAPOKUTUPA SHIMONI YEYE ATAKUINUA VILELENI

Mwanzo 39:2 "Bwana akawa pamoja na Yusufu, naye AKASITAWI, naye alikuwa katika nyumba ya bwana wake, yule mmisri."

Hebu tutafakari kisa hiki, Yusufu alichukiwa na ndugu zake kwa sababu ya HAKI, wakaamua kumtupa shimoni ili afe, baadaye akauzwa kwa wafanyabiashara, nao wakamuuza Misri kwa Potifa, baadaye akasingiziwa kubaka mke wa Potifa akatupwa gerezani. Mwanzo 37:21-28, 39:1-23.

Mwisho tunaona Bwana akiwa na Yusufu gerezani, akamtumia kuitafsiri ya ndoto mfalme farao, ndipo farao akaamua kumpatia cheo cha kuwa juu ya misri yote, akawa ndiye mtawala wa pili kwa farao. Mwanzo 41:41-44.

Ni kawaida kukuta watu wanapanga njama za hila ili kumuonea na kumharibia maisha mwenzao, wanapenda asifanikiwe, kwa sababu ya wivu, kwa midomo ya uongo huzusha maneno, huchonganisha, wako tayari wamchafue ili wamharibie maendeleo yake.

Rafiki; ukiona hali hiyo inatokea, iwe ni katika maisha ya kawaida au kwemye kazi ya Mungu, mshukuru Mungu, jua hiyo ni kazi ya shetani, zidi kumtazama Mungu na kuwaombea. Hata wakutupe kwenye shimo la taka kwa namna yoyote ile, Bwana atakupandisha kutoka kilele hadi kilele cha mafanikio.

Mwanadamu anapopanga kukuangusha, kukukanyaga, kukudhalilisha, kukukatisha tamaa, kukuvunja moyo, Mungu yeye anapanga KUKUPANDISHA VILELENI na wao kuwashusha chini, endelea kuwa mwaminifu kwa Mungu siku zote, naye hatakuacha.

WEMA WA BWANA UKAZIDI KUWAFUNIKA SIKU HADI SIKU

Na: Ev. Eliezer Mwangosi
Simu: 0767210299
Tovuti: evmwangosi.blogspot.com.
FB: Ev Eliezer Mwangosi.

eliezer.mwangosi

unread,
Mar 20, 2018, 11:27:25 PM3/20/18
to aak...@hq.bot-tz.org, ester...@yahoo.com, annie...@yahoo.com, cella...@yahoo.co.uk, emie...@yahoo.com, Arusha Reception, bmas...@gmail.com, elijahc...@yahoo.com, bngan...@yahoo.com, evam...@yahoo.co.uk, devon...@yahoo.com, ckiiz...@yahoo.com, emmy...@yahoo.com, Andyni...@yahoo.com, benson...@yahoo.com, emba...@yahoo.com, damar...@ymail.com, epiphania...@yahoo.com, bmt...@gmail.com, elig...@yahoo.co.uk, Erick...@hotmail.com, Dat...@scitz.com, Buhatwa Ladislaus, berna...@gmail.com, weddym...@gmail.com, csend...@yahoo.com, Emmyk...@gmail.com, answ...@yahoo.co.uk, alfredb...@yahoo.com, annas...@yahoo.com, ana...@hotmail.co.uk, debok...@yahoo.com, emap...@yahoo.co.uk, chec...@yahoo.co.uk, dai...@diamondtrust.co.tz, yourtr...@googlegroups.com, deri...@yahoo.com, anne...@hotmail.com, deoma...@yahoo.com, ant...@gmail.com, elyta...@yahoo.com, Edesia Kahyarara, apbw...@yahoo.co.uk, Evel...@gmail.com, bar...@yahoo.com, cjk...@yahoo.co.uk, Dorah....@tigo.co.tz, zaina...@yahoo.com, ema...@serena.co.tz, ymt...@hotmail.com
NENO LA LEO - YUKO WAPI YUSUFU WA LEO?

Mwanzo 29:7-9 "Ikawa baada ya mambo hayo, mke wa bwana wake akamtamani Yusufu, akamwambia, Lala nami. Lakini akakataa, akamwambia mke wa bwana wake, Tazama;..... Nifanyeje ubaya huu mkubwa nikamkose Mungu?"

10-12 "Akawa akizidi kusema na Yusufu siku baada ya siku, lakini hakumsikia alale naye, wala aongee naye. Ikawa, siku moja, akaingia nyumbani atende kazi yake, wala hapakuwa na mtu katika watu wa nyumbani humo ndani; huyo mwanamke akamshika nguo zake, akisema, Lala nami. Yusufu akaiacha nguo yake mkononi mwake, akakimbia, akatoka nje."

Kama kuna sehemu ambayo shetani ameshatangaza ushindi kwa Vijana, na hata wazee, ni hii hapa ya UZINZI na UASHERATI. Ingelikuwa ni TV tungesema Dish limecheza ni chenga tupu, ingelikuwa ni umeme tungesema fuse imekata au imeungua na ingekuwa ni mtandao tungesema network imekata hakuna mawasiliano.

Vijana wengi network zao na Mungu zilishakata, mishipa ya fahamu ya kuhisi au kutambua kuwa zinaa ni dhambi, ilisha kufa ganzi au ilishakatika. Ndio maana anaweza kuimba "Nimekombolewa na Yesu, na sasa nimefurahi, kwa bei ya mauti yake, mimi mtoto wake", baada ya hapo anawasha data na anaanza kurusha sms za mapenzi na kupanga miadi na akina switiiii.

Mungu anatafuta akina Yusufu wa leo, ambao antena zao bado zinashika mawasiliano na mbingu ili awatumie, anaambulia chenga. Hata kama wengine hawafanyi Ngono live, kwa sababu yoyote ile, wengi wameharibu akili zao kwa picha na message chafu za mitandaoni, hizo zote ni zinaa.

Wengi katika kizazi hiki wanamkimbilia Mungu baada ya kujeruhiwa na ADUI, japo Mungu anawakubali, wanakuwa tayari wameathirika na wanabaki kujutia. Bado kuna uwezekano wa kuwapata vijana wanaoweza kusimama kama Yusufu, wasio kubali kabisa kuchafuliwa, na Mungu anawatafuta vijana kama hao.

Huu ni wakati wa kusema HAPANA kama Yusufu, inawezekana, kwa kudumu kumtazama na kumwamini Mungu. Kwa waliojeruhiwa na adui, bado lipo tumaini, Yesu alikufa ili wadhambi waokolewe na kupewa HAKI ya kuwa watoto wa Mungu. Huu ni wakati uliokubalika  ... IKIMBIENI ZINAA, Bwana hatawaacha daima.

NAWATAKIA MAISHA YENYE MAFANIKIO NA BARAKA TELE.

%%% Tafadhali, wapelekee na wengine ujimbee huu, Mungu atakubariki %%%

Na: Ev. Eliezer Mwangosi
Simu: 0767210299
Tovuti: evmwangosi.blogspot.com
FB: Ev Eliezer Mwangosi.

eliezer.mwangosi

unread,
Mar 26, 2018, 11:30:52 PM3/26/18
to aak...@hq.bot-tz.org, ester...@yahoo.com, annie...@yahoo.com, cella...@yahoo.co.uk, emie...@yahoo.com, Arusha Reception, bmas...@gmail.com, elijahc...@yahoo.com, bngan...@yahoo.com, evam...@yahoo.co.uk, devon...@yahoo.com, ckiiz...@yahoo.com, emmy...@yahoo.com, Andyni...@yahoo.com, benson...@yahoo.com, emba...@yahoo.com, damar...@ymail.com, epiphania...@yahoo.com, bmt...@gmail.com, elig...@yahoo.co.uk, Erick...@hotmail.com, Dat...@scitz.com, Buhatwa Ladislaus, berna...@gmail.com, weddym...@gmail.com, csend...@yahoo.com, Emmyk...@gmail.com, answ...@yahoo.co.uk, alfredb...@yahoo.com, annas...@yahoo.com, ana...@hotmail.co.uk, debok...@yahoo.com, emap...@yahoo.co.uk, chec...@yahoo.co.uk, dai...@diamondtrust.co.tz, yourtr...@googlegroups.com, deri...@yahoo.com, anne...@hotmail.com, deoma...@yahoo.com, ant...@gmail.com, elyta...@yahoo.com, Edesia Kahyarara, apbw...@yahoo.co.uk, Evel...@gmail.com, bar...@yahoo.com, cjk...@yahoo.co.uk, Dorah....@tigo.co.tz, zaina...@yahoo.com, ema...@serena.co.tz, ymt...@hotmail.com
NENO LA LEO: KUANGAMIA KWA KUKOSA MAARIFA

Hosea 4:6 "Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa; kwa kuwa wewe umeyakataa maarifa, mimi nami nitakukataa wewe, usiwe kuhani kwangu mimi; kwa kuwa umeisahau sheria ya Mungu wako, mimi nami nitawasahau watoto wako."

Kwa kuzaliwa, watu wote wanapenda maisha mazuri, maisha ya kufanikiwa, maisha yenye furaha, amani na upendo; hayo ndiyo yalikuwa makusudi ya Mungu kwa mwanadamu. Bahati mbaya sana shetani aliingilia kati, akamtenganisha mwanadamu na Mungu, kwa kumshawishi afanye dhambi (Kuasi juu ya maagizo ya Mungu). Hapo ndipo ulikuwa mwanzo wa maisha yaliyojaa uchungu na kukosa matumaini.

Hata hivyo, Mungu alifanya kila njia kumrejesha mwanadamu katika makusudi yake ya mwanzo, hapo ndipo kazi kubwa inatakiwa, hapo ndipo pambano kuu lilipo, shetani hakubali kirahisi watu waokolewe, anafanya kila njia kuwapotosha njia wasirudi kwa Baba yao. Mungu ametupatia NENO lake kama taa na Yesu Kristo akatumwa kuja kulifunua, na kutuweka HURU tukiwa kwenye NURU halisi.

Kadri tunavyoelekia mwisho, shetani anafanya kila njia kuwakosesha watu wa Mungu wasiijue kweli, mafundisho potofu na falsafa zilizo nje ya misingi ya kweli, zinajaa kwenye akili za wasafiri. Siku hizi AMRI za Mungu zimekuwa kitu kigeni, somo la Neema kimekuwa kichaka cha watumishi wengi kuhalalisha uovu na kila namna ya utapeli wa kiroho.

TABIA ya Ucha Mungu kwa wengi inabaki ya midomoni tu, ukristo wa nadharia unazidi kushamiri, japo wengi wanakimbilia makanisani au kwenye majumba ya ibada, lakini bado mishale ya yule adui haiwaachi. Siku hizi miujiza na ishara ndiyo chambo cha manabii na mitume kunasa wengi, na wengi wanaishia kufanyiwa mambo ya aibu, na kuzidi kuziunguza dhamiri zao.

Neno la leo linatoa wito mkuu wa kumrudia Mungu, kwa Imani katika Kristo na kulitii neno lake na amri zake, hakuna aliyechelewa, mlango wa rehema bado uko wazi, tunapaswa kufanya matengenezo na kutakaswa kwa neno .. Yohana 17:17. Utakatifu wetu unapimwa kwa Imani ya Yesu inayotuongoza kutii neno la Mungu ... Ufunuo 14:12. Shetani anafanya vita ya mwisho juu ya wanaoshika Amri za Mungu na Ushuhuda wa Yesu ... Ufunuo 12:17, 1Yohana 2:4, Mathayo 5:17-19.

Siku nyingine nitatoa ufafanuzi wa tofauti kati ya sheria zilizoishia msalabani (Ambazo mtume Pulo ameziita sheria za torati) na Amri au sheria za maadili, zinazoonyesha mapenzi ya Mungu, zinazodumu milele, ukiziasi unaitwa mtenda dhambi.

NAWATAKAIA SIKU NJEMA YENYE BARAKA TELE.

¥¥¥ Utazidi kubarikiwa ukiwasambazia wengine ujumbe huu ¥¥¥

Na: Ev. Eliezer Mwangosi

Simu: 0767 210 299

Tovuti: evmwangosi.blogspot.com

FB: Ev Eliezer Mwangosi.

eliezer.mwangosi

unread,
Apr 3, 2018, 11:37:50 PM4/3/18
to aak...@hq.bot-tz.org, ester...@yahoo.com, annie...@yahoo.com, cella...@yahoo.co.uk, emie...@yahoo.com, Arusha Reception, bmas...@gmail.com, elijahc...@yahoo.com, bngan...@yahoo.com, evam...@yahoo.co.uk, devon...@yahoo.com, ckiiz...@yahoo.com, emmy...@yahoo.com, Andyni...@yahoo.com, benson...@yahoo.com, emba...@yahoo.com, damar...@ymail.com, epiphania...@yahoo.com, bmt...@gmail.com, elig...@yahoo.co.uk, Erick...@hotmail.com, Dat...@scitz.com, Buhatwa Ladislaus, berna...@gmail.com, weddym...@gmail.com, csend...@yahoo.com, Emmyk...@gmail.com, answ...@yahoo.co.uk, alfredb...@yahoo.com, annas...@yahoo.com, ana...@hotmail.co.uk, debok...@yahoo.com, emap...@yahoo.co.uk, chec...@yahoo.co.uk, dai...@diamondtrust.co.tz, yourtr...@googlegroups.com, deri...@yahoo.com, anne...@hotmail.com, deoma...@yahoo.com, ant...@gmail.com, elyta...@yahoo.com, Edesia Kahyarara, apbw...@yahoo.co.uk, Evel...@gmail.com, bar...@yahoo.com, cjk...@yahoo.co.uk, Dorah....@tigo.co.tz, zaina...@yahoo.com, ema...@serena.co.tz, ymt...@hotmail.com
TAFAKARI BAADA YA SIKUKUU YA PASAKA

Mathayo 26:27-28 “Akakitwaa kikombe, akashukuru, akawapa, akisema, Nyweni nyote katika hiki; kwa maana hii ndiyo damu yangu ya agano, imwagikayo kwa ajili ya wengi kwa ondoleo la dhambi”.

Kama kuna mambo ya kushangaza; basi na hili ni moja wapo, siku ya Jumapili (Siku ya kwanza Juma), ambayo asilimia kubwa ya wakristo, wanaamini Yesu kristo alifufuka kutoka kaburini, ndiyo siku niliyoshuhudia Makundi ya Vijana kwa Watu wazima, WAKIVINJALI katika kila namna ya starehe.

Kama ni pombe zilinyweka, kama muziki ulichezwa, maholi ya Disco yalifurika, na sehemu zingine nikasikia disco toto ni marufuku siku ya Pasaka, na jambo la kushangaza zaidi ni kusikia hata nyumba za kulala wageni (Guest house) zilijaa. Ukipita ufukweni kwa wanaokaa pwani, unajionea kila aina ya vituko, lakini ndiyo siku ambayo ndoa za masaa zilishamiri.

Wapendwa sikilizeni, kuna wengi ambao kwa kutokujua au kwa kudanganywa na adui, wamejiona wameifaidi sikukuu kwa mtindo huo wa kutenda maouvu, kumbe wamejipatia HATIA ya mwili na damu ya Bwana wao. Mtume Paulo anasema “Basi kila aulaye mkate huo, au kukinywea kikombe hicho cha Bwana isivyostahili, atakuwa amejipatia hatia ya mwili na damu ya Bwana.” 1Wakoritho 11:27.

Japo agizo la kuadhimisha Pasaka kwa Neno la Kristo, ni kushiriki huduma ya Meaza ya Bwana au Chakula cha Bwana, wala sio sherehe kama inavyofanywa siku hizi, neno linasema ..

1Wakorinrho 11:23-26 “Kwa maana mimi nalipokea kwa Bwana niliyowapa nanyi, ya kuwa Bwana Yesu usiku ule aliotolewa alitwaa mkate, naye akiisha kushukuru akaumega, akasema, Huu ndio mwili wangu ulio kwa ajili yenu; fanyeni hivi kwa ukumbusho wangu. Na vivi hivi baada ya kula akakitwaa kikombe, akisema, Kikombe hiki ni agano jipya katika damu yangu; fanyeni hivi kila mnywapo, kwa ukumbusho wangu. Maana kila mwulapo mkate huu na kukinywea kikombe hiki, mwaitangaza mauti ya Bwana hata ajapo.”

Japo sio agizo la Kristo kuadhimisha pasaka kwa sherehe kama hizi, bado wale wanaoamini na kusherekea wanapaswa kujua kinachotakiwa kufanywa katika adhimisho, ili wasije wakata HATIA badala ya BARAKA itokanayo na UTAKASO au ONDOLEO la Dhambi. Watu wanao endelea kufanya dhambi, baada ya kushiriki huduma hii ya pasaka, “WANAMSULUBISHA mwana wa Mungu mara ya pili, na KUMFEDHEHI kwa dhahili” Waebrania 6:5-6.

Bado nafasi ingalipo ya kila mmoja kujitathmini, ameitumiaje sikukuu hii ya pasaka? Ameondoka na nini mbele za Mungu? Hatia au Baraka? Huu ni wakati wa kufanya matengenezo.

MUNGU AMBARIKI KILA MMOJA ANAPOTAFAKARI SOMO HILI

Na: Ev. Eliezer Mwangosi.

eliezer.mwangosi

unread,
Apr 8, 2018, 11:11:00 PM4/8/18
to aak...@hq.bot-tz.org, ester...@yahoo.com, annie...@yahoo.com, cella...@yahoo.co.uk, emie...@yahoo.com, Arusha Reception, bmas...@gmail.com, elijahc...@yahoo.com, bngan...@yahoo.com, evam...@yahoo.co.uk, devon...@yahoo.com, ckiiz...@yahoo.com, emmy...@yahoo.com, Andyni...@yahoo.com, benson...@yahoo.com, emba...@yahoo.com, damar...@ymail.com, epiphania...@yahoo.com, bmt...@gmail.com, elig...@yahoo.co.uk, Erick...@hotmail.com, Dat...@scitz.com, Buhatwa Ladislaus, berna...@gmail.com, weddym...@gmail.com, csend...@yahoo.com, Emmyk...@gmail.com, answ...@yahoo.co.uk, alfredb...@yahoo.com, annas...@yahoo.com, ana...@hotmail.co.uk, debok...@yahoo.com, emap...@yahoo.co.uk, chec...@yahoo.co.uk, dai...@diamondtrust.co.tz, yourtr...@googlegroups.com, deri...@yahoo.com, anne...@hotmail.com, deoma...@yahoo.com, ant...@gmail.com, elyta...@yahoo.com, Edesia Kahyarara, apbw...@yahoo.co.uk, Evel...@gmail.com, bar...@yahoo.com, cjk...@yahoo.co.uk, Dorah....@tigo.co.tz, zaina...@yahoo.com, ema...@serena.co.tz, ymt...@hotmail.com
NENO LA LEO - PASIPO YEYE HATUWEZI LOLOTE

Yohana 15:5 "Mimi ni mzabibu; ninyi ni matawi, akaaye ndani yangu nami ndani yake, huyo huzaa sana; maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya neno lo lote."

Katika safari ya maisha yetu ya kila siku, tunakumbana na changamoto za hapa na pale na aina mbalimbali, ndipo tunashuhudia wengi wakikiri kushindwa, na wengine kukata tamaa na wengine kufanya maamuzi hatarishi.

Kupitia neno la leo, Yesu anathibitisha kuwa, peke yetu hatuwezi, ni kwa njia ya sisi kusalimisha maisha yetu kwake ili atushindie, ni dhahiri asubuhi ya leo, wengi wanakiri kushindwa sehemu fulani, inawezekana kuna dhambi fulani imeshindikana kuachwa, au ni hitaji fulani ambalo sasa ni mzigo mzito unaohitaji msaada.

Ikiwa ni asabuhi tulivu ya Jumatatu, kuna mwangwi wa sauti yenye suluhisho ya kila changamoto na mapito, kutoka kwa Yesu Kristo anayejua shida zetu kabla hazijatokea, inatusihi tumtazame yeye na kusalimisha maisha yetu kwake, ili atupatie ushindi.

NAKUTAKIA JUMATATU YENYE MIANZO MIPYA KWA KILA JAMBO KATIKA YEYE.

Na: Ev. Eliezer Mwangosi
Simu: 0767 210 299

eliezer.mwangosi

unread,
Apr 10, 2018, 11:15:53 PM4/10/18
to aak...@hq.bot-tz.org, ester...@yahoo.com, annie...@yahoo.com, cella...@yahoo.co.uk, emie...@yahoo.com, Arusha Reception, bmas...@gmail.com, elijahc...@yahoo.com, bngan...@yahoo.com, evam...@yahoo.co.uk, devon...@yahoo.com, ckiiz...@yahoo.com, emmy...@yahoo.com, Andyni...@yahoo.com, benson...@yahoo.com, emba...@yahoo.com, damar...@ymail.com, epiphania...@yahoo.com, bmt...@gmail.com, elig...@yahoo.co.uk, Erick...@hotmail.com, Dat...@scitz.com, Buhatwa Ladislaus, berna...@gmail.com, weddym...@gmail.com, csend...@yahoo.com, Emmyk...@gmail.com, answ...@yahoo.co.uk, alfredb...@yahoo.com, annas...@yahoo.com, ana...@hotmail.co.uk, debok...@yahoo.com, emap...@yahoo.co.uk, chec...@yahoo.co.uk, dai...@diamondtrust.co.tz, yourtr...@googlegroups.com, deri...@yahoo.com, anne...@hotmail.com, deoma...@yahoo.com, ant...@gmail.com, elyta...@yahoo.com, Edesia Kahyarara, apbw...@yahoo.co.uk, Evel...@gmail.com, bar...@yahoo.com, cjk...@yahoo.co.uk, Dorah....@tigo.co.tz, zaina...@yahoo.com, ema...@serena.co.tz, ymt...@hotmail.com
NENO LA LEO - NJIA ILIYOJERUHI WENGI

Tafadhali soma ujumbe huu hadi mwisho na wapelekee wengine ...

Mithali 14:12 "Iko njia ionekanayo kuwa sawa machoni pa mtu, Lakini mwisho wake ni njia za mauti."

Nilikuwa nafuatilia tukio la wito wa mkuu wa mkoa wa D'salaam la wanawake na watoto waliotelekezwa na wanaume zao, nimeshangaa kuona umati mkubwa wa wamama na watoto wakiwa wamejaa, wenye machungu mioyoni. Na hao ni kiasi cha waliojitokeza, kwa mkoa huu mmoja.

Ukifuatilia kwa undani, asilimia kubwa ya matatizo hayo ni matokeo ya kufanya starehe ya ngono nje ya ndoa halali, yaani Uzinifu na Uasherati. Hapo kuna walioiba waume za watu, kuna waliozalishwa kwa kudanganywa kuwa watawaoa, kuna waliorubuni wanaume ili wapate watoto kwa hiari yao, lakini pia kuna waliokuwa katika ndoa waume zao wakaporwa na viruka njia.

Kuna mithali isemayo, MAJUTO NI MJUKUU, yaani kila jambo linalotendwa nje ya utaratibu wa Mungu, lina matokeo hasi baadaye, wakati vidumu na vibanda hasara vinalia kwa kutelekezwa, wapo wamama waliojeruhiwa na wanapitia machungu katika ndoa zao kwa sababu ya waume zao kuporwa.

Dhambi ya zinaa na uasherati ni pango kubwa ambalo wengi wanatumbukia, na kuambulia majeraha na wengine mauti, wakati akina mama wanahaha, akina Baba nao matumbo moto, wengi walijifanya waaminifu kwa wake zao, sasa wakati umefika wa kuanikwa hadharani, yale maraha yote ya kuitwa BABY huku wakipepewa kama watoto mdogo, sasa yamegeuka KARAHA kama sio miiba.

Wanaume na wanawake, sikilizeni, neno linasema; "Afichaye dhambi zake hatafanikiwa; Bali yeye aziungamaye na kuziacha atapata rehema." Mithali 28:13. Bila kujali matokeo, huu ni wakati wa kuungama dhambi hii, na kuwekwa huru.

Ushauri kwa wanaume vijana na wazee; Mungu anasema; "Mtu aziniye na mwanamke hana akili kabisa; Afanya jambo litakalomwangamiza nafsi yake. Mithali 6:32. Wewe unayejirusha nje ya ndoa, wewe unayekopa tendo la ndoa, (Unayeishi kwenye advance ya ndoa), na wewe unaye onja onja na kutelekeza baada ya kuharibu, Mungu anasema, ni sawa na kichaa anayegusa nyaya za umeme wa transfoma bila kujua matokeo yake.

Na mwisho; bila kujali ulitelekeza mke au mtoto kwa sababu yoyote ile, kwa usalama wako, TUBU na anza kutunza watoto, bila kujali lolote linaloweza kutokea, TUNZA WATOTO, tunza FAMILIA ili uwe salama. Mungu anasema "Lakini mtu ye yote asiyewatunza walio wake, yaani, wale wa nyumbani mwake hasa, ameikana Imani, tena ni mbaya kuliko mtu asiyeamini." 1Timotheo 5:8.

Ujumbe huu usaidie wote kujua athari ya ngono nje ya ndoa, wale waliojeruhiwa na wakora wa mapenzi, bado Mungu yupo wakimtumaini atawafanyia njia pasipo njia, wale wasio ingia katika dhambi hii wasiingie hadi ndoa, wale wanaoendelea kuvinjali nje ya ndoa waache haraka kabla ya maumivu.

NAWATAKIA SIKU NJEMA YENYE BARAKA TELE.

+++ UTABARIKIWA ZAIDI UKIWASAMBAZIA WENGINE UJUMBE HUU +++

Na: Ev. Eliezer Mwangosi
Simu: 0767 210 299
Tovuti: evmwangosi.blogspot.com
FB: Ev Eliezer Mwangosi.
Reply all
Reply to author
Forward
0 new messages