Amen
Ubarikiwe kwa nyongeza,Niki post kwenye youtruevine ina reject, unanisaidiaje?Sent from Samsung tablet
-------- Original message --------
From: Bahati Mashimba
Date:29/06/2015 2:05 PM (GMT+03:00)
To: "eliezer.mwangosi" ,YourTrueVine
Cc: Mgedzi Deborah
Subject: Re: NENO LA LEO - USHOGA NI DHAMBIAmina.Wanadamu wanajinenea kuwa wenye hekima na kupumbazika. Mtume Paulo ameeliza vizuri katika Waroma1:21-27.Mungu amewaacha wafuate akili zao. Kama walivyokataa kuwa na Mungu katika fahamu zao ,Mungu aliwaacha wafuate akili zao zisizofaa, wayafanye yasiyowapasa.Waroma1:282015-06-29 4:02 GMT+01:00 eliezer.mwangosi <eliezer....@yahoo.com>:NENO LA LEO - USHOGA NI DHAMBI YA LAANA
Walawi 18:22-23 "Usilale na mwanamume mfano wa kulala na mwanamke; ni machukizo.
Wala usilale na mnyama ye yote, ili kujitia unajisi kwake; wala mwanamke asisimame mbele ya mnyama ili kulala naye; ni uchafuko".
Wakati dunia yetu inajazwa na Kelele zinazowafanya watoto, vijana na hata wazee wasisikie sauti ya Munu, ndivyo kizazi chetu kinaingia kwenye LAANA Kubwa na hatimae Mwisho wa mambo yote utafika.
Kile kilichofanyika kwa taifa kubwa la Marekani, kupitisha sheria ya Uhuru wa Ndoa za Jinsia moja, ni dalili mbaya za Ulimwengu kuelemewa na dhambi. Ukizingatia kuwa Marekani ni chimbuko la madhehebu mengi ya kikristo (wa Protestant), kutokana na misingi ya Uhuru wa dini iliyokuwa mejiwekea.
Asubuhi ya leo nasikia mwangwi wa sauti ikisema "......Mcheni Mungu, na kumtukuza, kwa maana saa ya hukumu yake imekuja, Msujudieni yeye aliyezifanya Mbingu na nchi na bahari na chemichemi za maji" Ufunuo 14:6-7. Kelele za Uovu zimekwenda kuziba hadi masikio ya viongozi wa dini wasisikie wala kuona sheria ya Bwana, na hatimaye kushia kusema, Tuko HURU chini ya Neema, wakimkana hata Kristo aliyewafia. Leo ndoa za mashoga, wasagaji na hata za wanyama zinakubalika na watu wa dini.
Taratibu lakini kwa uhakika, ndivyo kizazi hiki chote kinatiwa katika LAANA, vijana wengi na hata wazee wana practice vitendo hivi vichafu, na mbaya zaidi hata viongozi wa dini. Michezo yoyote ya Ngono kinyume na tendo halali la Ndoa, ni UCHAFU. Mashuleni na Vyuoni umejaa uchafu wa aina hii, Mabinti WANASAGANA na Vijana wa Kiume nao kulawiti wenzao, kwa kupenda au kulazimishwa.
Siku hizi Mapenzi kinyume na maumbile, ambayo wengine huita Mlango wa UANI, yanaonekana sio dhambi, vijana ndio michezo yao, na hata kwenye Ndoa au uchumba feki, hadi kwa wanaojiita watu wa Mungu, tunashuhudia kesi na malalamiko kwa akina mama wakitendewa haya. Hebu niwaulize, mumewahi kuona jogoo au Mbwa amekosea na kufanya kiyume? Mwanadamu AMEASI na amepotelewa na akili, zaidi ya mnyama.
Wito: Jiokoeni na kizazi hiki kiovu, wakati Neema kupitia kafara ya Yesu Kristo ingali ina NGUVU ya kuokoa kutoka katika kila Uchafu wa Dhambi (UASI WA MAAGIZO YA MUGU) kwa wote wanaoamini.
NAWATAKIA SIKU NJEMA YENYE AMANI YA MUNGU MIOYONI MWENU SASA NA HATA MILELE
Na: Eliezer Mwangosi - Simu 0767210299, Email - eliezer....@yahoo.com.Sent from Samsung tablet