Bahati Mashimba
unread,Apr 25, 2017, 3:40:14 AM4/25/17Sign in to reply to author
Sign in to forward
You do not have permission to delete messages in this group
Either email addresses are anonymous for this group or you need the view member email addresses permission to view the original message
to YourTrueVine
NENO LA TAFAKARI: SIMAMA IMARA KATIKA WOKOVU
WAFILIPI 2:12 Basi wapendwa wangu kama vile mlivyotii sikuzote si
wakati mimi nilipokuwapo tu, bali sasa zaidi sana mimi nisipokuwapo,
UTIMIZENI WOKOVU WENU wenyewe kwa kuogopa na kutetemeka..
Wapendwa tunaishi nyakati zilizojaa changamoto mbalimbali za maisha,
wapo waliokosa furaha kwa sababu ya dhiki,magonjwa,uchumi kuyumba na
wengine wamekata tamaa kutokana na kukosa amani katika jamii
wanayoishi,ndoa, kazi, na hata katika hali ya umaskini ,kisiasa.
Lakini pia wapo wanaosumbukia maisha katika kutafuta kiasi kwamba
wameacha wokovu kwasababu zao za utafutaji.Haijalishi tunakazi zipi;
nilazima tutimize wokovu katika Kristo na kuwa na hofu ya Mungu si tu
tunapokuwa kwenye jamii inayotufahamu au watumishi wanaotujua bali
mahali popote tunapokuwa tuonakane tuna Yesu ndani yetu.
Mtume Paulo anatusihi Wakristo wote pamoja na Maaskofu ,Mashemasi ya
kuwa ni lazima tusimame imara katika wokovu uliowathamani sana bila
kujali changamoto za maisha tunazokutana nazo kwa kuwa tunaye Bwana
ambaye yeye ni kila kitu katika maisha yetu na tena ni furaha yetu
ambaye hututia nguvu na kutuwezesha katika mambo yote.
Ili tuweze Kusimama Imara katika Wokovu ni lazima:
1.Kujihadhari na mafundisho ya uongo Wafilipi 3:1-2
2.Kuacha kuutumainia mwili Wafilipi 3:3-7
3.Kuwa na shauku ya kumjua zaidi Yesu Wafilip 3:8-11
4.Kuwa na hamu ya kufikia lengo la imani Wafilipi 3:12-16
5.Kujiepusha na maadui wa msalaba Wafilipi 3:17-2
Bwana atubariki na neema yake iwe pamoja nasi sote,
MUNGU AZIDI KUTULINDA NA NGUVU ZAKE ILI TUSIACHE WOKOVU KWA SABABU YOYOTE ILE