|
Bali, zingatieni kwanza Ufalme wa Mungu na matakwa yake, na hayo mengine yote mtapewa kwa ziada. Mathayo 6:33 Yesu aliwaambia wanafunzi wake wasiwe na wasiwasi juu ya
mahitaji ya miili yao ya kwamba wale nini,wanywe nini,wavae nini. Mungu
anajua kabisa kwamba tunahitaji kuvaa, kula, kusoma,kuoa na kuolewa, nyumba, pesa, kuponywa magonjwa, ulinzi.Hayo
yote na meningine Mungu anayajua na hutupa nguvu na njia ya
kuyapata. Ndiyo maana watu wengi wanasumbuliwa sana na mioyo yao kutosheka,na hawaridhiki.Kile wanachopata kila siku kwao hakitoshi. Ukiomba upate ubunge moyo utataka upate na uwaziri,
ukiomba upate kazi yenye pesa nzuri, ukiipata kazi hiyo moyo utataka kazi
nyingine yenye pesa zaidi. Hitaji la moyo wa mtu asiyezaliwa mara ya pili huwa halitosheki siku zote. Kama
mkristo hajampa Mungu nafasi ya kwanza katika maisha yake tatizo hili lazima limsumbue.Tunaona taifa letu watu
wachache walio wakristo na wasiomjua Kristo wenye nafasi serikalini wanavyojilimbikizia mali kwa njia isiyo
halali kwa sababu mioyo yao inatafuta kile ambacho hakiwezi kukidhi haja za utajiri, ndiyo maana hawatosheki na wanachokipata. |
--
Mkikaa ndani yangu na maneno yangu yakikaa ndani yenu basi ombeni chochote mtakacho nanyi mtapewa.Yohana15:7