NENO LA LEO

32 views
Skip to first unread message

eliezer.mwangosi

unread,
Mar 28, 2017, 2:37:14 AM3/28/17
to
NENO LA LEO - WEMA WA MUNGU HAUTAONDOKA KWAKO
Isaya 54:10 "Maana milima itaondoka, na vilima vitaondolewa; bali WEMA wangu HAUTAONDOKA kwako, wala AGANO langu la AMANI halitaondolewa; asema BWANA akurehemuye".

Rafiki;  bila kujali hali ya maisha unayoipitia, changamoto zisizoisha, huenda unaomba Maombi na Mungu anaonekana amekaa Kimya - Neno linasema WEMA wa Mungu HAUTAONDOKA KWAKO. Kumbuka maisha ya nyuma uliyopitia, ni hakika kuna wakati mgumu  ulikuwa mbele  yako ukiwa umekosa matumaini, lakini leo hii imebaki kuwa historia. Inua macho yako juu, tazama ahadi za Mungu wako - Naye atalitimiza Neno lake kwa wakati usioudhani. Songa mbele kwa IMANI isiyoyumba, naye ATATENDA.

NAKUTAKIA SIKU NJEMA YENYE BARAKA NA MAFANIKIO TELE

Na: Ev. Eliezer Mwangosi  - +255766992265




Sent from Samsung tablet
Reply all
Reply to author
Forward
0 new messages