NENO LA LEO 28.11.2011 YESU MTULIZA DHORUBA

413 views
Skip to first unread message

Eliezer Mwangosi

unread,
Nov 27, 2011, 10:04:48 PM11/27/11
to

Salaam,

 

NENO LA LEO:  Mathayo 8:23-27

“Akapanda chomboni, wanafunzi wake wakamfuata. Kukawa na msukosuko mkuu baharini, hata chombo kikafunikizwa na mawimbi; naye alikuwa amelala usingizi. Wanafunzi wake wakamwendea, wakamwamsha, wakisema, Bwana, tuokoe, tunaangamia. Akawambia mbona mmekuwa waoga, enyi wa imani haba? Mara akaondoka, KAZIKEMEA PEPO NA BAHARI; KUKAWA SHWARI KUU”

TAFAKARI:

Kama kawaida ya Maisha ya Mwanadamu, katika ulimwengu huu wa dhambi, tunakumbana na dhoruba tusizozitegemea. Tunashuhudia waliokuwa na maisha mazuri hadi wanafikia kubeza wengine, hali zinageuka ghafla bila matarajio, wanakuwa na hali za kukatisha tamaa, hata asubuhi ya leo, kuna watu hawaoni raha ya maisha, na wengine usiku ulikuwa mrefu, hawajapata usingizi. Wapendwa ulimwengu huu hauna hauna mwenyewe, ni Mungu peke yake mwenye mamlaka, ni mara ngapi tunasikia watu wanasombwa na SUNAMI wakiwa kwenye maraha UFUKWENI?

Tafakari ya leo inatukumbusha kuwa; katikati ya DHORUBA kuu ya maisha, Yesu karibu nasi, ana uwezo wa kuliza kila namna ya tufani inayoweza kutusonga. Yeye hatishwi na tufani, wakati wanafunzi wanapiga yowe kwa hofu ya Dhoruba kuu, chombo kikifunikwa na Mawimbi, ndio kwanza Yesu alikuwa analala usingizi. Neno linasema; wakamwamsha wakisema, Bwana, TUOKOE, TUNAANGAMIA. Mara akazikemea pepo, zikatulia kukawa shwari. Rafiki, unachangamoto gani? Ni mazingira ya kazi magumu? Ni Biashara yako? Ni maisha magumu? Ni Ndoa yako inayopepesuka kama mlevi? Ni Uchumba uliosambalatika? Ni kuonewa au kutengwa? Ni Ugonjwa usio na tiba? Ni Upweke? N.k. hizo zote ni DHORUBA, karibu sana na wewe yupo Bwana wa Mabwana na Mfalme wa Wafalme, tamka maneno matatu tu kwa Imani “Bwana Niokoe Ninaangamia”. Utashangaa tatizo lako likiwekwa kwenye ushuhuda likiwa limekoma.
 

MUNGU ATUPATIE SIKU NJEMA YENYE AMANI ANA BARAKA TELE

 

Ev:  Eliezer Mwangosi.

Ukiona vema, wapelekee wengine ujumbe huu wa matumaini au nitumie E-addrees zao.

Maswali na Ushauri – vinaruhusiwa bila mashariti yoyote.


Eliezer Mwangosi

unread,
Nov 27, 2011, 10:21:20 PM11/27/11
to

Salaam,

 

NENO LA LEO:  Mathayo 8:23-27

“Akapanda chomboni, wanafunzi wake wakamfuata. Kukawa na msukosuko mkuu baharini, hata chombo kikafunikizwa na mawimbi; naye alikuwa amelala usingizi. Wanafunzi wake wakamwendea, wakamwamsha, wakisema, Bwana, tuokoe, tunaangamia. Akawambia mbona mmekuwa waoga, enyi wa imani haba? Mara akaondoka, AKAZIKEMEA PEPO NA BAHARI; KUKAWA SHWARI KUU”

TAFAKARI:

Kama kawaida ya Maisha ya Mwanadamu, katika ulimwengu huu wa dhambi, tunakumbana na dhoruba tusizozitegemea. Tunashuhudia waliokuwa na maisha mazuri hadi wanafikia kubeza wengine, ghafla hali zao zinageuka bila matarajio, wanakuwa na hali za kukatisha tamaa, hata asubuhi ya leo, kuna watu hawaoni raha ya maisha, na wengine usiku ulikuwa mrefu, hawajapata usingizi. Wapendwa ulimwengu huu mwenyewe, ni Mungu peke yake mwenye mamlaka, ni mara ngapi tunasikia watu wanasombwa na SUNAMI wakiwa kwenye maraha UFUKWENI?

Tafakari ya leo inatukumbusha kuwa; katikati ya DHORUBA kuu ya maisha, Yesu yupo karibu nasi, ana uwezo wa kutuliza kila namna ya tufani inayoweza kutusonga. Yeye hatishwi na tufani yoyote, wakati wanafunzi wanapiga yowe kwa hofu ya Dhoruba kuu, chombo kikifunikwa na Mawimbi, ndio kwanza Yesu alikuwa analala usingizi. Neno linasema; wakamwamsha wakisema, Bwana, TUOKOE, TUNAANGAMIA. Mara akazikemea pepo, zikatulia kukawa shwari. Rafiki, unachangamoto gani? Ni mazingira ya kazi magumu? Ni Biashara yako? Ni maisha magumu? Ni Ndoa yako inayopepesuka kama mlevi? Ni Uchumba uliosambalatika? Ni kuonewa au kutengwa? Ni Ugonjwa usio na tiba? Ni Upweke? N.k. zote hizo ni aina za DHORUBA,  Bwana wa Mabwana na Mfalme wa Wafalme, yupo karibu sana na wewe, anasubiri, utamke maneno matatu tu kwa Imani “Bwana Niokoe Ninaangamia”. Utashangaa tatizo lako likiwekwa kwenye ushuhuda likiwa limekoma.
Reply all
Reply to author
Forward
0 new messages