eliezer.mwangosi
unread,Feb 13, 2018, 1:45:41 AM2/13/18Sign in to reply to author
Sign in to forward
You do not have permission to delete messages in this group
Either email addresses are anonymous for this group or you need the view member email addresses permission to view the original message
to aak...@hq.bot-tz.org, ester...@yahoo.com, annie...@yahoo.com, cella...@yahoo.co.uk, emie...@yahoo.com, Arusha Reception, bmas...@gmail.com, elijahc...@yahoo.com, bngan...@yahoo.com, evam...@yahoo.co.uk, devon...@yahoo.com, ckiiz...@yahoo.com, emmy...@yahoo.com, Andyni...@yahoo.com, benson...@yahoo.com, emba...@yahoo.com, damar...@ymail.com, epiphania...@yahoo.com, bmt...@gmail.com, elig...@yahoo.co.uk, Erick...@hotmail.com, Dat...@scitz.com, Buhatwa Ladislaus, berna...@gmail.com, weddym...@gmail.com, csend...@yahoo.com, Emmyk...@gmail.com, answ...@yahoo.co.uk, alfredb...@yahoo.com, annas...@yahoo.com, ana...@hotmail.co.uk, debok...@yahoo.com, emap...@yahoo.co.uk, chec...@yahoo.co.uk, dai...@diamondtrust.co.tz, yourtr...@googlegroups.com, deri...@yahoo.com, anne...@hotmail.com, deoma...@yahoo.com, ant...@gmail.com, elyta...@yahoo.com, Edesia Kahyarara, apbw...@yahoo.co.uk, Evel...@gmail.com, bar...@yahoo.com, cjk...@yahoo.co.uk, Dorah....@tigo.co.tz, zaina...@yahoo.com, ema...@serena.co.tz, ymt...@hotmail.com
NENO LA LEO - BIDHAA ADIMU KATIKA JAMII
1 yohana 2:29 "Kama mkijua ya kuwa yeye ni mwenye haki, jueni ya kuwa kila atendaye haki amezaliwa na yeye."
Kama kuna bidhaa inayozidi kuadimika siku hadi siku katika kizazi hiki ni KUTENDA HAKI. Wakati mwingine hili neno HAKI linakuwa kama halieleweki vizuri, lakini kwa maneno rahisi neno HAKI ni mtu kutendewa anachostahiri, kulingana na utaratibu uliowekwa.
Kwa wanaosikiliza vyombo vya habari, tumeshuhudia umati wa watu uliofurika, walioitikia mwaliko wa Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, kusikiliza kero za DHULUMA za viwanja, kwa kweli ni hali ya kushangaza, na hiyo ni sekta ya ardhi peke yake, lakini kila kona ya maisha ya jamii kuna mwangwi mkubwa wa vitendo vya UONEVU na DHURUMA.
Sikiliza, kila tendo analotenda mtu juu ya mwingine kinyume na sheria au utaratibu ulio wekwa sio HAKI, Upendeleo, Uonevu, Hila, Unafiki, Vijicho, Undumila kuwili, Uzushi, Uongo, Ubinafsi, Mioyo ya Chuki, mawazo mabaya, visasi na tabia zinazofanana na hizi, ni matunda ya UOVU, yasiyo ya HAKI.
Neno la leo, linatukumbusha kuwa kila atendaye HAKI amezaliwa na Mungu, asiyetenda HAKI ni uzao wa adui. Hebu kila mmoja, iwe katika Familia, Iwe kwenye mahusiano, Iwe Maofisini, Iwe Makanisani, Iwe Misikitini, Iwe kwenye ngazi yoyote Serikalini, Iwe popote pale, tunapaswa KUTENDA HAKI.
Neno la Mungu linasema, Kutotenda HAKI, ni tendo la AIBU ni UOVU, bali HAKI huleta mafanikio, huleta AMANI na Furaha katika Jamii, na Mungu anakuwa kati yetu. Mithali 14:34 "Haki huinua taifa; Bali dhambi ni aibu ya watu wo wote."
NAWATAKIA SIKU NJEMA YENYE MAFANIKIO NA BARAKA TELE
Na: Ev. Eliezer Mwangosi
Simu: 0767 210 299
Sent from my Samsung Galaxy smartphone.