NANO LA LEO 01.02.2012 KUTEMBEA JUU YA MOTO BILA KUUNGUA

14 views
Skip to first unread message

Eliezer Mwangosi

unread,
Jan 31, 2012, 9:23:06 PM1/31/12
to

Salaam,

 Ukiona vema mtumie mwingine ujumbe huu - au nitumie email address yake niwe namtumia

NENO LA LEO:  Danieli 3:24-25

“Ndipo Nebukadreza akastaajabu, akainuka kwa haraka; akanena, akawaambia mawaziri wake, Je! Hatukutupa watu watatu, hali wamefungwa, katikati ya Moto? Wakajibu, wakamwambia mfalme, Kweli, ee mfalme. Akajibu, akasema, Tazama, mimi naona watu wanne nao wamefunguliwa, wanatembea katikati ya Moto hali hawana dhara; na Sura yake yule wa nne ni mfano wa mwana wa Miungu”

tAFAKARI:

Bila kujali hali ya Mtu aliyonayo, awe tajiri sana au maskini, awe mzuri sana au mbaya, awe mweupe au mweusi, awe mrefu au mfupi, haijarishi una hali gani na jamii inakuonaje, maisha yanaweza kubadilika hadi ukajisikia uko katika Tanuri la Moto la Majaribu au Changamoto fulani. Unaweza ukamkuta Mwanaume Tajiri ana kila kitu, na anacheo kikubwa kazini, anaweza kuwa hata Raisi, ambaye anauwezo wa kufanya analotaka. Lakini utashangaa siku moja anaongea peke yake barabarani au ofisini, macho yamekuwa mekundu, ni mkali kwa kila mtu, mambo yamegeuka, mbele anaona Giza, Ukiuliza kulikoni? utakuta nyumbani hali ya hewa imeharibika, nyumba haikaliki – anatafuta jinsi ya kujinasua na Ndoa ambayo ni ngumu badala ya Furaha ni Karaha tupu. Changamoto za maisha ziko nyingi, inaweza kuwa Ugonjwa, UKATA wa fedha, kuachwa na Mchumba, kukosa Kazi, kudhulumiwa, kuonewa, Pango la Nyumba, Tabia za watoto zimeharibika, ni manyanyaso ya ndugu?  n.k.

 Maisha siyo kama tunavyoyaona, ni zaidi ya hapo, Vijana watatu wa kiebrania walipitia changamoto ya kujaribiwa Imani yao, wakilazimishwa kuisujudia sanamu ya mfalme wa Babeli badala ya Mungu wao. Adhabu kwa wasio tii ilikuwa ni kutupwa katika tanuri la Moto, Vijana wale waliamua kumtii Mungu kuliko mwanadamu na Waliamini juu ya ahadi ya Mungu kuwa atawaokoa. Mwisho wa yote wakafungwa na kutupwa katika moto, Mungu aliingilia kati – Neno linasema “alionekana Mtu wa nne aliyemfano wa Mwana wa Miungu” huyo si mwingine ila ni Mwana wa Mungu mwenyewe alishuka akauamuru MOTO usifanye kazi ya kuunguza, na ikawa hivyo, walipoitwa kutoka katika Moto, huyo mtu wa nne akatoweka.

 Rafiki yangu Mpendwa inawezekana unapitia changamoto fulani ambayo tayari ni kama uko kwenye Moto, Kumbuka ahadi ya Mungu inasema “….Uendapo katika Moto hautateketea, wala mwali wa moto hautakuunguza” Isaya 43:2. Mtazame Yesu mwana wa Mungu yuko karibu sana na wewe, ana uwezo wa kugeuza shida yako ikawa Baraka. Kwa wale ambao mambo yao yako Shwari, wanaishi kama wako peponi, kumbuka maisha ni Mlima – Ni salama kuwa na Mungu sasa ili awasaidie wakati wa kukosa matumaini.

NAWATAKIA SIKU NJEMA YENYE AMANI, FURAHA NA BARAKA TELE

 

Ev:  Eliezer Mwangosi.

0755808077 & 0652571733

Kwa masomo zaidi fungua mitandao ifuatayo:   http://emwangosi.blogspot.com/ (VIJANA) http://kayanafamilia.blogspot.com/ (NDOA) http://matengenezo.blogspot.com/ (UKWELI ULIOFICHIKA NA KUUKULIA WOKOVU)


Reply all
Reply to author
Forward
0 new messages