NENO LA LEO

42 views
Skip to first unread message

eliezer.mwangosi

unread,
Aug 8, 2016, 5:51:31 PM8/8/16
to
NENO LA LEO - VITABU VILIVYOCHANIKA.

Hebu tafakari muundo wa kitabu imara, utakuta kuna "Hard Covers" juu na chini, na zimeungana huwezi ona maungio. Halafu karatasi za ndani zenyewe ni laini, lakini nazo zimeshikiliwa na hizo hard cover kwa kutumia Gundi isiyobanduka. Ikitokea, cover (jarada) moja limechanika, utakuta kitabu kizima kinasambaratika, makaratasi yanaanza kutoka hata kwa upepo.

Mfano huo wa kitabu ni sawa na Ndoa inayounda familia. Baba na Mama ni Majarada (Hard Cover), na watoto ni sawa na Makaratasi ya Ndani ya Kitabu. Mungu anafanya kazi kama GUNDI ambayo ndiyo inaunganisha Majarada na kuyafanya yawe Imara na hatimaye kuyashikiria makaratasi. Mungu anapokosekana kati wa wanandoa, makusudi ya Mungu juu ya Ndoa yanapotea. Yesu alisema maneno Haya.

Marko 10:7-9 "Kwa sababu hiyo mtu atamwacha babaye na mamaye, ataambatana na mkewe; na hao wawili watakuwa mwili mmoja; hata wamekuwa si wawili tena, bali mwili mmoja. Basi alichokiunganisha Mungu, mwanadamu asikitenganishe.

Mishale mingi yenye sumu za kujeruhi na hata kuua inaelekezwa katika Ndoa na hatimaye familia. Na muasisi wa mashambulizi hayo ni Adui mkuu Shetani, ambaye anapinga mpango wa Mungu aliyeasisi Ndoa pale edeni, na kuifanya sehemu ya kuudhihirisha Upendo wake, ni sehemu yenye usalama, ni sehemu ya furaha na Amani. Kwa bahati mbaya sana Ndoa nyingi zimegeuka kuwa sehemu za kujeruhiwa mioyo.

Ndoa nyingi zimebeba sura za vitabu vilivyochanika, vingine vibaki na jarada moja, na makaratasi ya ndani (watoto), yamechanika na kupeperushwa na kila upepo, kama ilivyo kwa kitabu Gundi ikitoka, ndivyo ilivyo kwa Ndoa Mungu asipokuwa kati yao. Shetani atarusha kila aina ya mishale na kuhakikisha amesambaratisha na kuleta MAJERAHA.

Neno la leo, linamkumbusha kila mmoja anayeanzisha mahusiano, kuunganishwa na Mungu, kama unapenda mahusiano yenu yadumu, omba sana kila mmoja wenu aunganishwe na Mungu, HUU NI WAJIBU WA KILA MMOJA, Kwani mmoja akiachia Kitabu, mahusiano yamesambaratika.

Je kitabu chako kina sura gani? Kama kimeshachanika, usikate tamaa, unganisha moyo wako na Mungu, utakuwa salaama hata kama uko peke yako. Kama majarada au makaratasi ya kitabu yamechakaa, kila mmoja ana wajibu wa kuunganishwa upya na Mungu, ataimarisha mahusiano kama mwanzo.

KUUNA FAMILIA BILA MUNGU NI SAWA NA KITABU KILICHOCHANIKA.

NAWATAKIA SIKU NJEMA YENYE MIANZO MIPYA YA MAFANIKIO.

Na Ev. Eliezer Mwangosi - 0767 210 299




Sent from Samsung tablet

Safari Daudi Buganda

unread,
Aug 9, 2016, 8:03:36 AM8/9/16
to yourtr...@googlegroups.com

Aksante kwa ujumbe mzuri ambao utasaidia kuponya ndoa zetu.Mungu akubariki sana.


______________________________________________________________________
This email has been scanned by the Symantec Email Security.cloud service.
For more information please visit http://www.symanteccloud.com
______________________________________________________________________

--
Mimi ni mzabibu ninyi ni matawi, akaaye ndani yangu nami ndani yake, huyo huzaa sana; maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya neno lolote.Yohana 15:5
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "YourTrueVine" group.
To post to this group, send email to yourtr...@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.


CONFIDENTIAL NOTE:
The information in this E-mail and any attachments transmitted are originated by SABMiller or any of its subsidiaries companies, is intended to be privileged and/or confidential and only for use of the individual, entity or company to whom it is addressed. If you have received this e-mail in error please destroy it and contact the sender. If you are not the addressee you may not disclose, copy, distribute or take any action based on the contents hereof. Any total o partial unauthorized retention, dissemination, distribution or copying of this message is strictly prohibited and sanctioned by law

eliezer.mwangosi

unread,
Aug 10, 2016, 5:27:59 PM8/10/16
to
NENO LA LEO - NYUFA ZINAZOBOMOA NYUMBA NYINGI

Mwanzo 2:24 "Kwa hiyo mwanamume atamwacha baba yake na mama yake naye ataambatana na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja."

Ndoa nyingi zimeathirika kama sio kuvunjika kabisa kutokana na kutotilia maanani fungu hili la maandiko. Leo tutaangalia kwa ufupi mambo mawili makubwa, yanayotoa fulsa kwa Shetani kutupa mishale na kujeruhi Ndoa.

1. KUWAACHA BABA NA MAMA.
Ndoa nyingi zinasambaratika kwa sababu wanandoa hawaachi wazazi wao. Na wazazi nao hawaachi watoto wao waanzishe familia zao. Akina mama wengi wanaingilia ndoa za watoto wao, wao ndio watoa amri, na Kijana asipokuwa makini atakuta Nyumba inaendeshwa na Mama au Baba.

Vilevile hata watoto wa- kike, wengi utakuta wazazi ndio wanaongoza nyumba, bila kusahau mawifi. Wanandoa wanapaswa kuwa huru kabisa, wakianza kujenga nyumba yao, bila kuingiliwa. Pia wanandoa wanapaswa kukaa mbali na wazazi wao, labda kuwe na sababu za msingi.

Sikilizeni: Huyo mke sio mke wa familia, mwenye amri naye ni mume wake anayejua uthamani wake. Hebu kila mtu amlinde mpenzi wake kutokana na maneno ya uchonganishi.

2. KUTENGANA
Ndoa ina siri ya muungano wa watu wawili kuwa mwili mmoja, ukiwatenganisha, kila mmoja anajisikia mpweke, katika hali hiyo ya kukosa mwenzi Shetani anapata nafasi ya kuleta njia mbadala kukidhi hitaji la upweke.

Asilimia kubwa ya wanaume, wanajikuta wamesaliti ndoa zao wanapokuwa mbali na familia kwa siku kadhaa. Wengi wananaswa na wapenzi wa mpito, hatimaye hukata mawasiliano wake zao. Vilevile inatokea kwa akina mama kusaliti ndoa zao wanapokuwa mbali na wapenzi wao.

Kutokana na ugumu wa kupata wenzi wa maisha, wanawake wakipata BUZI lililoacha mke, huenda kwa waganga na kuwatilia kila namna ya uchawi, ili wasikumbuke tena wake zao, au wawaone kama vinyago. Ndoa nyingi zinapitia machungu ya mafarakano kwa sababu ya kutengana.

Nimeshuhudia pia, wasichana wengi walioanzisha mahusiano ya Mapenzi wakiwa vyuoni, wanapomaliza vyuo na kutengana, wengi wanaporwa wapenzi wao kwa sababu ya kuishi mbali, vilio vya kuporana wachumba vinasikika kila kona, na kuwaacha mabinti wakiwa majeruhi wasio na msaada.

USHAURI:
1. Kwa wanandoa, msifanye ujinga wa kutengana bila sababu ya msingi. Kamwe msikubali kuishi mbalimbali, mmoja Mbeya na mwingine moshi, kuonana likizo. Huo sio mpango wa Mungu.

2. Wakati wote ni salaama kuishi chini ya Mamlaka ya Mungu. Ikitokea mnaishi mbalimbali kwa sababu za Msingi ... mfano masomoni, au KAZI ... Wote mkiishi maisha ya Ucha Mungu, mtakuwa salama, vinginevyo ni lazima majanga yatokee, kwa sababu kazi ya Shetani ni kuharibu na kuua.

Ni wajibu wa kila mmoja aliye katika mahusiano kusalimisha maisha yake mikononi mwa Mungu, ili awalinde na HILA za Shetani. Kama umepitia au uko katika dhoruba ya kuhujumiwa mpenzi wako .... Rudi miguuni pa Mungu, yeye ana uwezo wa kubomoa kila ngome alizoweka shetani juu yako na mwenzi wako.

KWA MUNGU YOTE YANAWEZEKANA.

NAWATAKIA SIKU NJEMA YENYE MAFANIKIO NA BARAKA TELE.

Na: Ev. Eliezer Mwangosi  - 0767 210 299.




Sent from Samsung tablet

eliezer.mwangosi

unread,
Aug 17, 2016, 11:28:59 PM8/17/16
to
NENO LA LEO - DHAMBI ISIYOSAMEHEKA

Mathayo 12:31 "Kwa sababu hiyo nawaambia, Kila dhambi na kila neno la kufuru watasamehewa wanadamu, ila kwa kumkufuru Roho hawatasamehewa."

Neno KUFURU lina maana ya; Tukana, kudhihaki, kudharau, kunena mabaya juu ya Wema, kupuuza n.k. Yesu aliwaambia mafarisayo maneno hayo, kutokana na msimamo wao wa Kiroho, wa kukataa makusudi kuamini kazi ya Yesu Kristo.

Kumkufuru Roho mtakatifu ni kitendo cha kumkataa Roho mtakatifu na Kazi yake. Roho mtakatifu ndiye anafanya kazi ya Kutufunulia Nuru au Kweli ya Mungu, anatuvuta tuiamini Kweli, anatushawishi tutubu dhambi na anatuongoza tutende Mapenzi ya Mungu.

Kitendo cha kumkataa Roho mtakatifu na kumdharau, ni kujifungia mlango wa kutoifikia TOBA, na kuendelea katika Dhambi hadi mauti. Mafarisayo walifikia kiwango hicho cha kufanya Uadui na Roho mtakatifu, walikaza mioyo hadi wakamsulubisha Mwana wa Mungu.

Mtume Paulo anasema    "Maana, kama tukifanya dhambi kusudi baada ya kuupokea ujuzi wa Ile Kweli, haibaki tena dhabihu kwa ajili ya dhambi; bali kuna kuitazamia hukumu yenye kutisha, na ukali wa moto ulio tayari kuwala wao WAPINGAO. Waebrania 10:26-27, pia soma; Waebrania 6:4-6. Hivyo kufanya Dhambi kusudi, na kukataa ushawishi wa Roho mtakatifu wa kuiachilia dhambi hiyo ni KUMKUFURU ROHO MTAKATIFU.

Hatua ya Mwisho baada ya makufuru, ni Roho mtakatifu kuacha kukushawishi, anakuwa amezimishwa, hofu ya Dhambi inapotea, Dhambi inakuwa kitu cha kawaida, inakuwa ni kitu cha kawaida ... Uzinifu, kuishi na mume au mke wa mtu, masengenyo, uongo, visasi, wizi, ulevi, upendeleo, wivu n.k. inakuwa ni sehemu ya maisha. Roho mtakatifu anakuwa amezimishwa - 1Wakorintho 5:19.

Dalili za juu za kumkufuru Roho mtakatifu ni, kuuchukia ukweli na kutopenda kuusikia ukweli, na  kutafuta kila njia za kubaki katika Dhambi fulani bila kiwa na mpango wa kuiacha. Mafarisayo walifikia hapo ... wakaanza kutunga njama za kumuua Masihi, na kumwita ana Pepo wa Beelzeburi, na hatimaye kumsulubisha. Kwa namna mbalimbali, wengi leo ni Makristo kwa Jina, lakini ndai yao wanampinga Kristo na Kumsukumia mbali Roho mtakatifu, anapowashawishi waache DHAMBI.

Wito: Kabla kengele za mauti hazijagonga, Mungu anatualika tena kupitia somo hili, kusiwe na mtu atakaye mkufuru Roho mtakatifu na kupotea milele. Neema ya Yesu yatosha kumtoa kila mmoja katika Dhambi na kumuweka huru.

NAWATAKIA SIKU NJEMA YENYE BARAKA TELE

Na: Ev. Eliezer Mwangosi  - 0767 211 299.

Utabarikiwa ikiwapelekea wengine ujumbe huu.




Sent from Samsung tablet

mtokajbc

unread,
Aug 24, 2016, 11:03:30 AM8/24/16
to yourtruevine

Amen  barikiwa  nyote

--

eliezer.mwangosi

unread,
Aug 24, 2016, 10:54:45 PM8/24/16
to
NENO LA LEO – NDOA NA IHESHIMIWE 
Waebrania 13:4 “Ndoa na iheshimiwe na watu wote, na malazi yawe safi; kwa maana waasherati na wazinzi  Mungu atawahukumia adhabu."

TAFAKARI:
Kama kuna bidhaa adimu katika maisha ya siku hizi, ni HESHIMA KATIKA NDOA. Wana ndoa asilimia kubwa hawaheshimiani, lakini pia hata watu wa nje hawaheshimu Ndoa za wenzao.

Utasikia matusi ya nguoni yakirushwa kati ya wanandoa mbele za watoto, magomvi ya usiku yasiyokoma, kunyanyasana, dharau, maneno ya mikato, kununiana n.k. yote hayo ni kukosa heshima katika ndoa.

Mawifi, mashemeji, akina mama mkwe n.k. tunashuhudia wakianzisha tafrani katika ndoa za ndugu zao. Bila kuwasahau wanaowasha mapenzi kwa waume au wake za watu. Hayo yote ni kuvunja heshima ya ndoa. Mithali 5:15 inasema “Unywe maji ya Birika lako Mwenyewe”. Uliona wapi watu wanapokezana vijiko wakati wa kula? Hata walevi nao siku hizi wamestaarabika, wameacha kupokezana chombo kimoja kuywea pombe, kila mtu anatumia kifaa chake.

Sehemu nyingine inayopaswa heshima ni chumbani, sehemu pekee ya kupumzisha akili na kupata furaha na kuwa na wakati wa faragha. Wapendwa, leo kuna kesi nyingi na matatizo mengi ya wanandoa, hata magonjwa mengi, yanatokana na KARAHA za hapo chumbani. Wengi vyumba vyao vimegeuka kuwa sehemu za gwaride, ni amri kama jeshini, sikiliza; huo sio uwanja wa masumbwi, wala uwanja wa Kwata, ni sehemu ya starehe na kuiburudisha nafsi.

Madereva wa magari wanalazimika kwenda Shule ili wajue kuendesha vizuri, wajue sheria za barabarani, na kujua jinsi ya kutunza gari, hata ndoa zina sheria zake, angalia madereva taxi wengi ambao wako “very rough” gari zao hazidumu, zinakongoroka hovyo, ndivyo zilivyo ndoa nyingi leo, zimajaa majeruhi wa vipigo kama sio moyo kukosa Amani. 

Pia sharti wanandoa wakumbuke kuwa kila kiungo cha mwili kiliumbwa kwa kazi maalumu, siku hizi mambo yamegeuka, wanadamu wanazidiwa akili na wanyama, umewahi kuona wanyama wamekosea wanafanya ngono kinyume na maumbile? lakini wanadamu bila aibu wanadai ni haki, tena kisheria. Wanadamu wamefikia kumkosoa muumba wao, na ndio maana laana inazidi kuifunika dunia.

Huu ni wakati wa wenye hekima, kumrudia Mungu na kuruhusu Roho mtakatifu atawale, ndoa ili UPENDO, AMANI na FURAHA vidumu katika familia na kuifanya nyumba iwe uwanja wa FARAGHA badala ya KARAHA.

NAWATAKIA SIKU NJEMA YENYE AMANI NA MAFANIKIO TELE

Na: Ev. Eliezer Mwangosi - 0767 210 299

Wapelekee wegine ujumbe huu - utabarikiwa.




Sent from Samsung tablet

bmashimba

unread,
Aug 26, 2016, 2:32:36 AM8/26/16
to YourTrueVine

Amina ubarikiwe  mtumishi wa Bwana

--

eliezer.mwangosi

unread,
Aug 30, 2016, 10:35:19 PM8/30/16
to
NENO LA LEO - NJIA ZA MAUTI KWA VIJANA WA LEO
Mithali 14:12 "Iko njia ionekanayo kuwa sawa machoni pa mtu, lakini mwisho wake ni njia za MAUTI"

Kizazi chetu kinazidi kukosa vijana waadilifu na wacha Mungu, ambao wangefaa kuendeleza kizazi chenye maisha yenye furaha na amani wakimtumaini Mungu. Bahati mbaya sana, vijana wengi sana, japo sio wote, wamenasa katika mitego, na kuziendea njia ambazo ni za MAUTI, tayari wametobolewa macho ya Kiroho, hawawezi kuona hatari zilizo mbele yao.

Neno la Mungu linasema "Mtu aziniye na Mwanamke hana akili kabisa; Afanya jambo litakalomwangamiza nafsi yake." Mithali 6:32. Japo Kila dhambi inamtenga mtu na Mungu na kuleta madhara kwa Jamii, Zinaa na Uasherati ni kati ya Mshale unaojeruhi vijana wengi, na kuwaachia vidonda visivyopona.

Mara nyingi dhambi ya Zinaa huzaa dhambi zingine. Ni mara ngapi akina dada wanashiriki mauaji ya kutisha, wakikata viungo vya watoto na kuwanyofoa kutoka katika matumbo yao? Ni mara ngapi wanaua watoto matumboni kwa kunywa Dawa, huku wakijisifiwa na kusema; namshukuru Mungu NIMETOA MIMBA SALAMA.

Na wanaume vijana kwa wazee, na hata wazazi wanaoshiriki kwa namna yoyote ile, kufanikisha zoezi la kutoa Mimba ni WAUAJI. Laana hiyo haipiti bure, wengi wanakuja kutafuta watoto baadaye katika Ndoa, hawapati, huku haki za damu za watoto waliowaua zikibaki zinawadai.

Dhambi ya Uuaji na Utesaji inaenda hadi kwa wanaume wanaume wanaotelekeza watoto bila kuwatunza. Kizazi chetu kinazidi kuwa na watoto yatima wa kutelekezwa, vijana wengi wa kiume ni matapeli wa mapenzi, wanajua kustarehe, ukifika wakati wa kulea wanakimbia futi mia, Dhambi hiyo ya kutelekeza watoto ni TANZI ya mauti.

Japo shetani anaipaka marashi dhambi hii ya Ngono kabla ya Ndoa na nje ya Ndoa; bado ni TANZI ya mauti. Watu wanadai ujana ni maji ya moto, eti hawawezi kuishi bila Ngono - huo ni utapeli wa Shetani, kuna akina Daniel na Yusufu wa leo tena ni wengi, bado kuna mabinti wengi na wavulana ambao huingia katika ndoa na ubikra wao. Kwa uwezo wa Mungu inawezekana, fanya maagano upya na Mungu, muamini Yesu, mpatie maisha yako.

Ni wakati wa kurudi nyumbani na kutafakari njia zetu, ni wakati wa kufanya uamuzi na kuanza upya, upendo wa Mungu na Neema yake kupitia kifo cha Yesu msalabani vinatosha kutuweka HURU na TANZI YA MAUTI.

NAWATAKIA SIKU NJEMA YENYE BARAKA TELE.

Na Ev. Eliezer Mwangosi - 0767 210 299.

Utabarikiwa ukimpelekea mwingine ujumbe huu.



Sent from Samsung tablet

Bahati Mashimba

unread,
Sep 1, 2016, 7:40:12 AM9/1/16
to eliezer. mwangosi, YourTrueVine

Amen

Reply all
Reply to author
Forward
0 new messages