NENO LA LEO - JINSI YA KUTUNZA UPONYAJI NA BARAKA ZA BWANA
Matendo 1:8 "Lakini mtapokea NGUVU, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa MASHAHIDI wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na samaria, na hata mwisho wa nchi".
Ndugu zangu; kila kukicha tunashuhudia watu wakiamka na misongo ya mawazo, hasa wanapoona changamoto kwao haziishi, kuna watu hadi wanajiita matatizo. Na jambo la kusikitisha ni kusikia Mkristo pia, analia juu ya kuonewa na Ibilisi, kwa kutupiwa Magonjwa, Kusumbuliwa na mapepo, Kuharibiwa biashara kwa Uchawi, kuvurugiwa Ndoa au Uchumba kwa dawa za waganga, mikosi ya familia, biashara, kazi, masomo n.k. Ndio maana vibao vya waganga wa mizimu vinazidi kila kona.
Na wengine usiku hawalali wakisumbuliwa na uchawi, na wengine wameolewa au kuoa mapepo, NGONO za kwenye ndoto wanafikiri ni starehe bila kujua ni majini mahaba. Kila kona siku hizi ni VILIO vya mikosi, laana, kuonewa, chuma ulete, hasira na ugonvi ni mtindo wa maisha, watu wanazunguka makanisa hadi makanisa, wakipata nafuu ya tatizo moja yanaibuka mengine. NI SHIDA SHIDA SHIDA.
Mpendwa SIRI YA USHINDI, ni kuunganishwa na Uweza wa Mungu, yesu aliwaambia wanafunzi wake kuwa "MTAPOKEA NGUVU" ndipo mtakuwa MASHAHIDI wangu. Walipovishwa uwezo kwa Njia ya Roho Mtakatifu; wakabadilika, mapepo yote ya Hasira, kupenda ukubwa au madaraka, wivu, chuki, ubinafsi, uongo, vijicho, umbeya, tamaa ya zinaa na mapepo ya kila tabia chafu yakahama. Shetani hakuwa na mamlaka juu yao Kabisa. HUO NDIO UKRISTO wenye maisha ya Ushindi.
Wito wa Mungu asubuhi ya leo ni: "STAY CONNECTED WITH GOD" Baki ukiwa umeunganishwa na Mungu, ili uonje maisha ya BARAKA za Bwana milele, achana na Ukristo Bandia, siku hizi kuna wokovu na kujazwa Roho feki, wokovu Bandia usiowaongoza watu kuacha dhambi, tamaa ya uzinifu, kugombania madaraka, wivu na uzushi havikomi, hizo ni Roho chafu haziwaongozi watu kumtii Mungu.
NAWATAKIA WOTE ASUBUHI TULIVU MKIZUGUKWA NA WEMA WA MUNGU
Na. Ev. E. Mwangosi - Tel. 0767210299. Email -
eliezer....@yahoo.com