NENO LA LEO

75 views
Skip to first unread message

eliezer.mwangosi

unread,
May 9, 2018, 10:35:57 PM5/9/18
to aak...@hq.bot-tz.org, ester...@yahoo.com, Yohana Mtoni, annie...@yahoo.com, cella...@yahoo.co.uk, emie...@yahoo.com, Arusha Reception, bmas...@gmail.com, elijahc...@yahoo.com, bngan...@yahoo.com, evam...@yahoo.co.uk, devon...@yahoo.com, ckiiz...@yahoo.com, emmy...@yahoo.com, Andyni...@yahoo.com, benson...@yahoo.com, emba...@yahoo.com, damar...@ymail.com, epiphania...@yahoo.com, bmt...@gmail.com, elig...@yahoo.co.uk, Erick...@hotmail.com, Dat...@scitz.com, Buhatwa Ladislaus, berna...@gmail.com, weddym...@gmail.com, csend...@yahoo.com, Emmyk...@gmail.com, answ...@yahoo.co.uk, alfredb...@yahoo.com, annas...@yahoo.com, ana...@hotmail.co.uk, debok...@yahoo.com, emap...@yahoo.co.uk, chec...@yahoo.co.uk, dai...@diamondtrust.co.tz, yourtr...@googlegroups.com, deri...@yahoo.com, anne...@hotmail.com, deoma...@yahoo.com, ant...@gmail.com, elyta...@yahoo.com, Edesia Kahyarara, apbw...@yahoo.co.uk, Evel...@gmail.com, bar...@yahoo.com, cjk...@yahoo.co.uk, Dorah....@tigo.co.tz, zaina...@yahoo.com, ema...@serena.co.tz
NENO LA LEO - JIAMINI NA KUJITHAMINI

1Wakorintho 7:23 "Mlinunuliwa kwa thamani; msiwe watumwa wa wanadamu."

Siku moja nilikutana na kijana mmoja ambaye alionekana kuchanganyikiwa, nilipomuuliza kulikoni? akajibu kwa ufupi "acha mtumishi, sioni tena haja kuishi", maneno kama haya hata kama hayasikiki sana yakisemwa, lakini yamejaa kwenye mioyo ya wengi, wakiwemo mabinti, akina mama na wababa, wanaopitia kuumizwa na wenzi wao.

Katika ulimwengu huu uliojaa uovu, ni jambo la kwaida kukutana na nafsi zilizojeruhiwa na kuumizwa na watu wengine. Watu wengi wanafikia kupoteza mwelekeo wa maisha na wengine kuchanganyikiwa, wanapokutana na hali wasiyoitarajia hasa katika mahusiano ambako waliwekeza nafsi zao na kuona wamefika. 

Neno la leo linatuonya tusisalimishe nafsi zetu kwa wanadamu wenzetu, na kuwekeza huko, wanadamu hugeuka kama upepo, mahusiano yoyote yanaweza kuvunjika wakati wowote na kujeruhi nafsi, usalama wetu ni kusalimisha nafsi zetu kwa Mungu. Yeye anatupenda na alintoa Yesu afe kwa yetu, tunapaswa kujisalimisha kwake.

Mtume Paulo aliwaambia wakorintho "Mlinunuliwa kwa thamani, msiwe watumwa wa wanadamu", Je umeachwa na mchumba? Mshukuru Mungu, huyo hakuwa wako, kama Mungu ameruhusu ana makusudi mema nawe. Je ni ndoa inayumba? Salimisha nafsi yako kwa Mungu utapita katika dhoruba hiyo salama. Je umedhurumiwa au kuonewa? Mungu yupo atakutetea, jiamini tu hayo nayo yatapita. Je kuna maumivi yoyote unayapitia? Salimisha nafsi yako kwa Mungu.

Sikiliza; Wewe ni wa thamani machoni pa Mungu, jiamini, peke yako unaweza kuishi bila ya huyo mwenzi. Hebu angalia ahadi hizi za Mungu; "Atawakomboa nafsi zao na kuonewa na udhalimu, Na damu yao ina thamani machoni pake." Zaburi 72:14. 

Mfalme Daudi anazidi kusema, wenye hakima machoni pa Mungu wana thamani kuliko marijani, wala hakuna cha kulinganisha. Zaburi 3:15 "Yeye ana thamani kuliko marijani, Wala vyote uvitamanivyo havilingani naye." Huu ni wakati wa KUSHINDA katika yeye Mungu muweza wa yote.

NAWATAKIA SIKU NJEMA YENYE KUFUNIKWA NA WEMA WA MUNGU.

Na: Ev. Eliezer Mwangosi
Simu: 0767210299




Sent from my Samsung Galaxy smartphone.

Bahati Mashimba

unread,
May 10, 2018, 10:04:15 AM5/10/18
to eliezer.mwangosi, aak...@hq.bot-tz.org, ester...@yahoo.com, Yohana Mtoni, annie...@yahoo.com, cella...@yahoo.co.uk, emie...@yahoo.com, Arusha Reception, elijahc...@yahoo.com, bngan...@yahoo.com, evam...@yahoo.co.uk, devon...@yahoo.com, ckiiz...@yahoo.com, emmy...@yahoo.com, Andyni...@yahoo.com, benson...@yahoo.com, emba...@yahoo.com, damar...@ymail.com, epiphania...@yahoo.com, bmt...@gmail.com, elig...@yahoo.co.uk, Erick...@hotmail.com, Dat...@scitz.com, Buhatwa Ladislaus, berna...@gmail.com, weddym...@gmail.com, csend...@yahoo.com, Emmyk...@gmail.com, answ...@yahoo.co.uk, alfredb...@yahoo.com, annas...@yahoo.com, ana...@hotmail.co.uk, debok...@yahoo.com, emap...@yahoo.co.uk, chec...@yahoo.co.uk, dai...@diamondtrust.co.tz, yourtr...@googlegroups.com, deri...@yahoo.com, anne...@hotmail.com, deoma...@yahoo.com, ant...@gmail.com, elyta...@yahoo.com, Edesia Kahyarara, apbw...@yahoo.co.uk, Evel...@gmail.com, bar...@yahoo.com, cjk...@yahoo.co.uk, Dorah....@tigo.co.tz, zaina...@yahoo.com, ema...@serena.co.tz
Amen, Bwana akubariki kwa neno la uzima
> Na: Ev. Eliezer MwangosiSimu: 0767210299
Reply all
Reply to author
Forward
0 new messages