NENO LA LEO

20 views
Skip to first unread message

eliezer.mwangosi

unread,
Sep 29, 2016, 11:42:48 PM9/29/16
to
NENO LA LEO - NEEMA YA MUNGU NI ZAIDI YA CHANGAMOTO TUNAZOPITIA

Hebu tafakari kisa hiki:
Mwanzo 39:1-5 "Basi Yusufu akaletwa mpaka Misri naye Potifa, akida wa Farao, mkuu wa askari, mtu wa Misri, akamnunua mkononi mwa hao Waishmaeli waliomleta huko. Bwana akawa pamoja na Yusufu, naye akasitawi; naye alikuwa katika nyumba ya bwana wake, yule Mmisri. Bwana wake akaona ya kwamba Bwana yu pamoja naye, na ya kuwa Bwana anafanikisha mambo yote mkononi mwake. 
 Yusufu akaona neema machoni pake, akamtumikia. Naye akamweka awe msimamizi juu ya nyumba yake, na yote yaliyomo akayaweka mkononi mwake. Ikawa tokea wakati alipomweka awe msimamizi juu ya nyumba yake, na vyote vilivyomo, Bwana akabariki nyumba ya yule Mmisri kwa ajili ya Yusufu. Mbaraka wa Bwana ukawa juu ya vyote alivyokuwa navyo katika nyumba, na katika shamba. 

Ni hali ya kawaida kwa mwanadamu kuvunjika moyo na kukosa amani pale anapopitia changamoto zilizo juu ya uwezo wake. Na tumeshuhudia wengi wakibadilika tabia, na wengine kuamua kufanya uasi juu ya Mungu, hasa wakiwa katika harakati za kujikwamua na changamoto wanazopitia.

Ndipo utakuta mtu anakuwa mkali, wengine kwa waganga, wangine kurukia na kudaka waume au wake za watu, wengine kwenye ulevi, wengine ni hasira na visasi, wengine utapeli na uzushi, wengine huamua kupoteza maisha na wengine ni kuzidi kuzama kwenye dimbwi la Mawazo na misongo, wengine kuvuruga mahusiano ya wenzao n.k.. Hebu kila mmoja anapopitia changamoto na majeraha ya kuumizwa moyo anachukua hatua gani au ulichukua hatua gani? Kila mmoja ana majibu.

Sikiliza - Haijalishi unapitia changamoto kubwa kiasi gani, bila kujali moyo wako umejeruhiwa kiasi gani, kila mzigo ulioubeba na kukufanya uvunjike moyo au kukata tamaa; asubuhi ya leo tambua kuwa NEEMA YA MUNGU ipo kwa ajili yako na ni zaidi ya hayo unayoyapitia. Dumu kumtazama yeye na kumpatia haja ya moyo wako, kwa wakati usiotarajia, mambo yote yatabadilika kama yalivyokuwa kwa Yusufu.

NAWATAKIA SIKU NJEMA.

Na. Ev. Eliezer Mwangosi - 0767 210 299




Sent from Samsung tablet

James Mtoka

unread,
Sep 30, 2016, 12:02:53 AM9/30/16
to yourtr...@googlegroups.com
Amena  mtumishi WA mungu  tubarikiwe  wore. 

Reply all
Reply to author
Forward
0 new messages