Salaam,
NENO LA LEO: ZABURI 46:1-2“Mungu kwetu sisi ni kimbilio na Nguvu, Msaada utakaoonekana tele wakati wa mateso. Kwa hiyo hatutaogopa ijapobadilika nchi, ijapotetemeka milima moyoni mwa bahari. Maji yake yajapovuma na kuumuka, ijapopepesuka milima kwa kiburi chake”TAFAKARI:Sitasahau kisa cha mama mmoja aliyejulikana kama mcha Mungu, lakini siku moja alishikwa uchawi, baada ya kukutwa makaburini usiku akiwa uchi. Baadaye iligundulika huyo mama hakuwa mchawi, ila alienda makaburini usiku kwa mashariti ya Mganga wa Kienyeji ili kuondoa Mikosi inayofanya Ndoa yake isambaratike na kuwa kama Jela ndogo, Ndoa imegeuka kuwa Ndoano. Siku ya tukio alilia kwa uchungu, akidai Ndoa yao ni Changa, lakini haina AMANI wala Furaha.Mtumishi wa Mungu Daudi ana ujumbe wa matumaini, pamoja na Dhambi yake ya Uzinzi na mauwaji ya kutisha katika familia ya Uria, alipomwendea Mungu kwa TOBA ya Dhati, alisamehewa dhambi zake na kila mara aliokolewa na Mungu kutoka katika Mikono ya Watesi.Rafiki! japo dhoruba iliyomfano wa sumani ipite katika – Ndoa yako, Biashara yako, Kazi yako, Afya yako, Mashamba yako, au maisha yako kwa Ujumla. Usifadhaike, Mungu yupo kwa ajili yetu daima ni MSAADA NA KIMBILIO LETU, KWAKE HAKUNA LISILO WEZEKANA.KATIKA JINA LA YESU KRISTO KILA MISHALE IKAVUNJIKE – AMANI, UPENDO NA FURAHA VIKATAWALE SAWASAWA NA AHADI ZA BWANA.BARAKA ZA BWANA ZIAMBATANE NANYI DAIMA, NA KUWA NA SIKU NJEMA.Na: Eliezer Mwangosi
Important Notice:
The National Bank of Commerce Limited is a registered Commercial Bank in the United Republic of Tanzania.
This e-mail and any files transmitted with it are confidential and intended for the use of the individual or entity to whom they are addressed.
Please note that there are terms and conditions and some important restrictions, qualifications and disclaimers ("the Disclaimer") that apply to this email. To read this click on the following address or copy into your Internet browser:
http://www.nbctz.com/disclaimer/email
The Disclaimer forms part of the content of this email.