On Thu Jul 14th, 2011 5:45 AM PDT Bahati Mashimba wrote:
>
>Ndoa ni mpango wa Mungu tangu alipomuumba Eva kwa ajili ya Adamu.Ndiyo maana mwanamume humwacha baba yake na mama yake akambatana na mkewe nao wawili huwa mwili mmoja.Mwanzo2:24.
>
>Ndoa nyingi za kikristo zimekuwa na matatizo mengi kwa sababu hazikujengwa kwenye msingi mzuri wa neno la Mungu.Na mara nyingi tatizo linalonekana ni masuala ya pesa na mambo mengine ya kinyumba.Kwa mfano yawezekana uko kwenye ndoa, ni kweli wewe ni mwanamume mwenye uwezo wa fedha, wengine wanawanunulia magari au kuwafanyia mambo mazuri wake zao lakini wewe humfanyii hivyo mke wako. Hata kwa wanawake pia, wapo ambao wamekuwa wakiwafanyia yaliyo mazuri waume zao hasa kwa kuwapa fedha na kadhalika, lakini wanashindwa kufahamu kuwa suala la kula vizuri au fedha sicho hasa muhimu kwa wanandoa.
>
>La muhimu katika ndoa ni kuishi kwa upendo na amani na pia kuangalia pande zote, kwa mfano kama ni kweli uko sawa kwenye suala la fedha, unapaswa kuangalia pia katika suala la mahusiano na mahaba kwa ujumla, je, kama mwanamume, una uwezo wa kushughulika kama ambavyo mwanamume anapaswa vilevile na mwanamke ana uwezo wa kushughulika kama ambavyo mwanamke anapaswa.
>
>Jambo la msingi kwa wanandoa kupenda kuwa na mazungumzo ya wazi huku mkiwa na shina imara katika Neno la Mungu. Eeh hata nyumbani, utakuta mara nyingi wanawake wanapika vitu kwa mazoea, kwamba aaah mume wangu huwa anapenda wali au ugali. Lakini ni vizuri wakati fulani kumuuliza unaonaje nikakupikia tambi na kadhalika.Pia wanaume utakuta wanaenda matembezi bila kumjulisha mke wake na akirudi akiulizwa ulikuwa wapi eehe anakuwa mkali.Mme naye anaweza kumfanyia jambo mkewe litakalo onyesha upendo mfano anaweza kumsifia hata kwa mapishi yake na chakula anachopika yeye ni kitamu kuliko maelezo.
>
>
>Mara nyingi wana ndoa wamejikuta kila mtu anafanya mambo yake bila kumshirikisha mwenzake kwa kukosa uaminifu kati yao.Unaweza kufanya kitu ukafikiri unatengeneza, kumbe unaharibu.
>Mpendwa Mkristo tuzifanye ndoa zetu kuwa zenye upendo na amani tele.
>
>Mtume Paulo aliandika barua kwa Wakorintho na kwetu sisi Wakristo juu ya kuoa.Tunasoma kwenye waraka wake wa kwanza kwa Wakorintho.''
>Kila mwanamume na awe na mke wake mwenyewe, na kila mwanamke awe na mume wake mwenyewe.Mume atimize wajibu alio nao kwa mkewe, naye mke atimize wajibu alio nao kwa mumewe.Mke hana mamlaka juu ya mwili wake, bali mumewe anayo hali kadhalika naye mume hana mamlaka juu ya mwili wake,bali mkewe anayo''.1Korintho7:2-4
>Na pia aliaandika amri ya wanandoa ambayo ni ya BWANA''Kwa wale waliooa ninayo amri tena si yangu ila ni ya Bwana, mke asiachane na mumewe, lakini kama akiachana naye basi abaki bila kuolewa ama la apatanishwe na mume wake.Mume naye asimpe talaka mkewe''1Korintho7:10-11
>
>Kitu muhimu kwenye ndoa ni kuwa na upendo wa agape.Mara nyingi watu wana pokuwa kwenye hatua ya uchumba huwa wana upendo usiokuwa na kifani lakini wengi wanashindwa kuendelea kuutuza upendo huo pindi wana poanza maisha ya ndoa.Paulo aliandika juu ya upendo katika barua yake ya kwanza kwa wakorintho akisema ''Mwenye upendo huvumilia,hufadhili, mwenye upendo hana wivu,hajidai,wala hajivuni.Mwenye upendo hakosi adabu,hatafuti faida yake binafsi,wala hana wepesi wa hasira,haweki kumbukumbu ya mabaya,hafurahii uovu, bali hurahia ukweli.Mwenye upendo huvumilia yote,huamini yote na hustahimili yote.Upendo hauna kikomo kamwe.1Korintho13:4-8
>
>Katika hali ya kawaida ni vigumu kushika matokeo haya ya upendo lakini kwa Wakristo ambao mienendo yao inaongozwa na Roho, matokeo hayo yanawezekana kabisa.Neno la Mungu linasema katika Wagalatia ‘Lakini matokeo ya kuongozwa na Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu,wema,fadhili,uaminifu,upole na kiasi.Hakuna sheria inayoweza kupinga mambo hayo’.Wagalatia5:22-23.
>
>Tukiishi kwa msaada wa Roho na tuuufate mwongozo wake .Basi tusijivune, tusichokozane wala kuoneana wivu: Wagalatia5:25-26
>
>Pia biblia inaendelea kutuambia wanandoa ‘Wake wawatii waume zao kama kumtii Bwana. Kama vile kanisa linavyomtii Kristo,vivyo hivyo wake wawatii waume zao katika mambo yote’ Waefeso 5:22,24
>
>‘Nanyi waume wapendeni wake zenu kama Kristo alivyolipenda
>kanisa, akajitoa mwenyewe sadaka kwa ajili yake’.Waefeso5:25
>
>Kila mume lazima ampende mkewe kama nafsi yake mwenyewe naye mke anapaswa kumstahi muweweWaefeso5:33
>
>Kuna baraka katika maisha ya ndoa kama wanandoa wakiishi pamoja kwa upendo kama ndugu na mwili mmoja. Kwa mwanamke anayemtii mume wake anaweza kubadili mwenendo wa mumewe kama mwanamuwe huyo hajaamini neno la Mungu kwa kuona mwenendo wa mkewe ukiwa safi.1Petro3:1-5
> Na kwa wanaume wanaowatendea wake zao kwa heshima watapokea zawadi ya uhai anaowapeni Mungu na pia sala zao hazitatiliwa kizuizi. 1Petro3:8
>
>
>
>
>
> Humble yourselves in the sight of the Lord and he shall lift you up James4:10
>
>--
>Usikubali kushindwa na ubaya bali ushinde ubaya kwa wema.Waroma12:21
Ujumbe mzuri sana. --- On Thu, 7/14/11, ambokile erasto <amb...@yahoo.com> wrote: |