Sasa wao kupitisha muswada wakidhani Watanzania wengi wako nyuma yao,
ikija kuonekana kuwa Watanzania wengi wanachukuzwa na nyendoi hizo za
CCM watajifichia wapi?
Ndio maana baadhi ya watanzania waliochoka wameamua kuanza kuwatishia
viongozi wa serikali kwa kuwapa siku 100 kuondoka kwneye nyasifa zao
vinginevyo yatawapata.... Wao badala ya kujadili namna ya kubadili
tabia zao na jinsi wanavyoongoza nchi ili hasira za watanzania zipoe,
wanafikiri jeshi la polisi na ulinzi wataweza kuziba ufa
unaosababishwa na ufisadi wao.
Leo wanatishia, kesho vijana wataingia msituni na support kubwa ya
watanzania walichoka kila kitu.
Mimi hii nchi, serikali na CCM wananichosha sana
Ukimtupia raisi mawe ili kuonyesha hasira yako unaitwa mhuni
Mimba za wasichana mashuleni yanaongezeka kwa sababu ya umasikini
unaoongezeka wanaambiwa wamejitakia
Wanafunzi wakiandamana kwa sababu ya kunyanyaswa wanaambiwa wanatumiwa
na wanasiasa
Wazee wakiandamana kudai mafao yao wanaambiwa wanatumiwa na wanasiasa
Waalimu wakigoma kwa kudai masilahi yao, hadithi ni ile ile
Watanzania wakitaka kuandamana kuelezea hisia zao, yaleyale
Sasa watanzania wafanyeje?
Waendelee kuvumilia shida, na ukal;i wa maisha kama morani
anayetahiriwa
Tulidhani katiba mpya ndio itaondoa uozo huu wa chama kimoja kuwa
dikteta wa maisha yetu hata kama hatuwataki wameaza na huko
kuchakachuwa
Kazi ipo
Lembu