Matamshi ya Ehud Barak -Waziri wa Ulizi wa Israel Yaleta Mgawanyiko na Hasira Tanzania

5 views
Skip to first unread message

Lemburis Kivuyo

unread,
Dec 31, 2011, 3:44:31 AM12/31/11
to wazalend...@googlegroups.com, kuhusu...@groups.facebook.com, tanzania...@groups.facebook.com
Matamshi aliyoyatoa waziri wa ulinzi wa Israel, Ehud Barak alipokuwa akihojiwa na mtangazaji Ayala Hasson wa Kituo cha redio cha
Israeli yaleta mgawanyiko na hasira Tanzania. Kimsingi yalimaanisha Tanzania "Haina umuhimu wowote kwa Israel. kama ilivyo Ujerumani, Ufaransa na Uingereza

Nukuu:  “Germany, France and England are not Tanzania, Mauritania or Tripolitania [jimbo mojawapo nchini Libya],”.... 

Alieleza Ehud na kuongezea “These are very important, very relevant countries and we don’t have an interest
in increasing tensions with them or making them bitter enemies.”


Mwitikio wa Tanzania
"Balozi wa heshima" wa Tanzania nchini Israel, Kasbian Nuriel Chirich alimwandikia barua Waziri wa Mambo ya Nje wa Israeli kulaani kauli hiyo ya Barak na kumualika kiongozi huyo kuitembelea Tanzania. Katika barua hiyo, "balozi" huyo pia alilaani kitendo cha Waziri Barak kuishusha hadhi Tanzania na kuilinganisha na nchi ambayo, kimsingi haipo hapa duniani (Tripolitania) ambalo ni jimbo tu nchini Libya!

Maoni ya Watanzania
Watu wengi wamejitokeza hapa Tanzania na kutoa maoni lukuki ya kulaani hiyo kauli ya Barak na kumtaka aifute na kuomba msamaha. Labda wako sahihi, lakini mimi naungana na wengi waliokuwa na maoni tofauti na hao wengine. Tanzania tangu enzi za Nyerere haikuwa na mahusiano mazuri na Israel, hata ubalozi wa nchi mbili husika haukuwepo. Matamshi mengi ya kidiplomasia ya Tanzania yamekuwa ni kuipinga Israel kwa sababu ya Wapalestina. Sasa unategemea Ehud Barak angesema nini kuhusu Tanzania? 

Feel free to ask any question and we will gladly try to help you

Cordially yours,  

Lembu
Technical Consultant - InfoCom Center
______________________________________________________________________________

Website and eMarketing Management Consultancy, Business and Community Projects Management Consultancy

Location:  Sokoine Rd, ACU Building, Opposite to Arusha Regional Library
Office Tel/Fax#:  +255 (0) 27 254 5430/ +255 (0) 73 297 8002, Cellphones: +255 654650100/+255 (0) 77 465 0100/+255 (0) 78 766 5050/+255 (0) 75 564 6470/
Website: www.infocomcenter.com, www.webstar5.net

Reply all
Reply to author
Forward
0 new messages