Katiba mpya tunayotaka Watanzania ni lazima iwe na sifa zifuatazo
1. Iondoe au kupunguza kwa kiwango kikubwa tofauti za muungano mfano
tunahitaji serikali moja au tatu, kama ni mbili basi iwe ni ya
Zanzibar na Tanganyika
2. Itofautishe wajibu wa mihimili mitatu ya dola, Mahakama, Bunge na
Serikali
3. Iweke wazi umiliki na ugawanyaji wa rasilimali kama ardhi, madini,
mafuta nk
4. Iweke wazi sera za nchi katika mahusiano na nchi za nje
5. Iweke sera na mfumo mmoja wa maendeleo ili nchi iwe na dira badala
ya dira za vyama vya kisiasa
6. Katiba mpya iwape wanachi mamlaka zaidi katika kuwachagua viongozi
na pia kuwarudi
7. Kamati ya uchaguzi iwe huru na isisimamiwe na serikali.
Michango zaidi inatakiwa