WAVUMBUZI

Contact owners and managers
1–1 of 224
Ndugu Mvumbuzi/Mtafiti/Mwanamaarifa/Mwanazuoni/Mwanataaluma/Msomi/Mchambuzi/Mwanatafakuri/Mzamivu/Mmahiri/Mtambuzi/Mgunduzi/Mbunifu/Msonga et al.,


Karibu kwenye Mtandao wa kukusanya, kusambaza, kuhifadhi na kujadili maarifa tunayoyatafiti, masuala tunayoyavumbua, na matokeo ya tafiti kuhusu Tanzania.

Hiki ni kikundi ambacho kimejikita tu katika masuala hayo hapo juu, hivyo, mtandao huu hautatumika kupiga soga/ubuyu/chai na kusambaza mipasho ya kisiasa.

Mada zote - ziwe ni za kisiasa, kidini, kiitikadi n.k. - zinakaribishwa ila kama mawasilisho ya kitafiti na kivumbuzi ama hoja za kujadili dhana au masuala ya kitafiti.

Pia huu ni ulingo wa kujengeana uwezo wa kitafiti na kiuvumbuzi ambapo tunaweza kuleta rasimu au mawazo ya awali kwa ajili ya kupata maoni ya kuyaboresha.

WhatsApp nayo imeunganishwa na Mtandao huu, hivyo, kama ungependa kujiunga tuma ujumbe wa kuomba kuunganishwa kwenye namba hii: +255754771763. 

Wasalaam,

Chambi Chachage