Mpendwa salaam katika jina la Yesu.
Tumeandaa semina ya wajane ambayo imepangwa kufanyika tarehe 20 February 2016 pale Palm Beach katika ukumbi uliopo St. Columba's Presbyterian Church. Semina itaanza saa mbili asubuhi mpaka saa kumi jioni.
Tutakuwa na watumishi wa Mungu watakao wezesha masomo yafuatayo; 1. Neema ya kuongoza familia na Mungu 2. Thamani ya uwajibikaji na huduma ya mjane.
Pia kutakuwa na Kipindi cha kuinuana kwa shuhuda na maombi. Uandikishwaji ni baada ya uhakiki wa uwepo hivyo tunaomba kama unamfahamu mjane yoyote utusaidie namba yake ili tuwasiliane naye kuconfirm.
Chakula, viburudisho na makabrasha vimeandaliwa Bure kwa ajili ya watakaoshiriki. Tafadhali tuma namba ya mshiriki wako pamoja na jina lake kwa uongozi wa Spatula Performance Initiatives (Stephen Samson Mkoloma 0713/0754 761341 na Ellyjalia Mabiki Stephen 0754638386) ili apigiwe simu na kuandikishwa. Tuna nafasi hamsini tu. Uandikishwaji utasitishwa idadi hiyo itakapotimia. Tafadhali wajulishe na wengine.
Mungu akubariki sana.
| Reply via web post | • | Reply to sender | • | Reply to group | • | Start a New Topic | • | Messages in this topic (1) |