Wanataaluma,
Habari za siku ndugu zangu Wazalendo !
Nadhani kila mmoja ameona ambavyo thamani ya fedha yetu ilivyoshuka thamani katika historia ya nchi yetu tangu tupate uhuru.
Kushuka kwa thamani ya fedha ya nchi yoyote haina maana ya kuonyesha moja kwa moja kuwa uchumi wa nchi husika umeshuka au umeathirika, hivyo basi kushuka au kupanda kwa thamani ya fedha kuna faida na hasara kulingana na mfumo na mpangilio wa kiuchumi wa nchi husika. Ziko nchi hufaidika kwa kushusha thamani ya fedha zake makusudi kwa malengo ya kupandisha kiwango cha mauzo ya nje na kuuza zaidi.
Mengi yanasemwa kuhusu sababu za kushuka kwa thmani ya fedha yetu dhidi ya dola ya Marekenai sasa nikaribishe michango kama kuna mdau yoyote ndani ya jukwaa hili anaweza kutuelimisha zaidi.
Noamba tuchangie mada hii kwa lengo la kuelimishana sababu, faida na hasara na nini kifanyike, labda kupitia jukwaa hili kuna mambo yanaweza yakachukuliwa na watunga sera wetu ambao baadhi yao ni wanchama wa mtandao huu ili kusaidia kujenga uchumi wetu.
Maana taarifa muhimu wananchi wasipoelimishwa vizuri kwa kupewa taarifa sahihi na kwa wakati sahihi inaweza ikasababisha wananchi kupaniki na kuleta athari zaidi kwenye uchumi , mfano ni jinsi uchumi wa dunia ulivyoyumba miaka ya 2008/2009 sababu moja ilichangiwa na wananchi wa Marekani na Uingereza kutopata taarifa sahihi kwa wakati sahihi na ikapelekea wengi wao kufanya maamuzi yasiyo sahihi ya kiuwekezaji/kifedha yaliyosababisha kuyumba kwa uchumi wote wa dunia.
Hivyo basi naomba nitoe wito kwa wote tuwe huru kutumia jukwaa hili na majukwaa mengine kwa lengo la kuelimishana na kupashana habari mbali mbali zilizo sahihi kwa faida yetu wote.
Wasalaamu.
B.Sc,PGDSE,MBA, IEng.,MIET
----------------------------
Mtaalamu na Mshauri wa TEHAMA, Menejimenti na Uongozi
Rais - Mtandao wa Wanataaluma Tanzania (TPN)
Cell: +255 (0784/0713/0767) 618320
E-mail: mag...@tanzaniaports.com
Mrema,
Umeongea kiasi fulani ila sababu za kushuka kwa Tzs. dhidi ya dola ya kimarekani ni hizi zifuatazo:-
1. Kuvuja kwa uchumi (economc leakage)/matumizi holela ya dola kwenye mzunguko wa ndani ya nchi wa fedha. Duniani kote, kuendesha uchumi imara kunahitaji mikakati na taasisi imara za kusimamia sera, sheria na kanuni za fedha. Nchini Ufaransa, kwa mfano, hairuhusiwi kubadilisha/kununua Euro taslim zenye thamani ya zaidi ya dola 1000! Afrika ya Kusini hairuhusiwi kutumia dola/euro isipokuwa rand tu unaponunua mali au huduma yoyote (hotelini, ticket za ndage n.k). Hapa nchini kwetu hali ni shaghala baghala – mamlaka zinazopaswa kusimamia uchumi wa nchi hazifanyi chochote; bureaux de change zinahamisha mauzo ya kila siku ya madukani kwenda nje ya nchi.
2. Watu, hasa mafisadi, kutorosha/kuhodhi dola nje ya nchi kutokana na hofu ya uchuguzi mkuu. Hali hii inasababisha uhaba wa dola hivyo kutengeneza artificial appreciation ya dola kutokana na msingi mkuu wa uchumi wa demand vs. supply.
3. Tanzania kutokuwa na dhahabu ya kuuza nje ya nchi (dhahabu inayochimbwa siyo ya kwetu bali ni ya makampuni yanayochimba (wawekezaji) na zaidi ya 90% ya mauzo ya dhahabu na madini mengine nje ya nchi hairudishwi nchini bali yanabaki huko (clauses za MDAs zinatoa fursa hizo kwa makampuniya madini) nyumbani kwao na wawekezaji. Kwa kifupi Tanzania siyo gold mining country bali ni source of gold, hivyo haimiliki madini yanayochimbwa nchini kwake bali madini husika humilikiwa na nchi mama wa makampuni ya wawekezaji.
4. Kuwa na weak manufacturing, construction and professional services industries hivyo nchi kutegemea imports zaidi kuliko uwezo wa kuuza huduma na bidhaa nje ya nchi. Aidha mauzo ya mazao ya kahawa, pamba, katani na chai nje ya nchi yamepungua kufikia negligible value. Nchi isipouza bidhaa na huduma za kutosha nje ya nchi haiwezi kuwa na akiba ya kutosha ya fedha ya kigeni. Na kwa mukhtadha huu, thamani ya fedha ya nchi haiwezi kuimarishwa na pesa ya misaada au mikopo kutoka kwa wafadhali au mashirika ya Bretton Woods.
5. Impact ya wizi wa pesa ya akaunti ya Tegeta Escrow (wafadhili kuzuia pesa ya misaada ya kibajeti). Zipo sababu nyingine pia zinazoathiri uchumi wa nchi (kuwa wa hovyo) kama Tanzania ambazo watu wake wengi bado hawategemei maarifa na ujuzi, bali ardhi na bidhaa, hususan kutokana na tasnia ya uziduaji.
Najua MNEC-CCM Magesa anatafuta hoja za ku-pacify hali mbaya inayokikabili chama chake ila ukweli ndio huo (free consultancy).
Kaiza
--
You received this message because you are subscribed to the Google Groups
"Wanataaluma wa Tanzania" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email
to wanataaluma...@googlegroups.com.
It is my opinion that this frightening devaluation of Tanzania Shillings has little, if anything, to do with
donor funds, or any other factors that might be causing the devaluation with complex social consequences
upon the poor masses of the nation. The result would be even more frightening !
Our failure to safeguard our currency is due to our absolute or complete lack seriousness in handling
the abuses we inflict upon our economy.
Past and recent financial scandals (some in newspapers and some in the ……. can provide some glimpse of
the problems.
Mohamed Sumar.
-------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------
Hello tujadili uchumi wa Tanzania na namna ya kuuokoa badala ya kuishia kulinganisha tu na mafanikio ya kiuchumi ya nchi nyingine. Ni vizuri wachumi wakachukua nafasi yao maana hisia na mipasho ya kisiasa haitatusaidia. Let’s talk openly.
Kwa taarifa ya wengine, uchumi wa Kenya umejengewa katika msingi imara wa a strong manufacturing and professional services industries. Kenya ni nchi ya tatu kwa Africa kuwa na a very strong manufacturing industry baada ya Africa Kusini na Egypt. Bajeti za kila mwaka za Serikali ya Kenya hutokana na/hutegemea kodi (hasa kutoka tasnia ya usindikaji na kilimo) na other internal pubic financing strategies such as monetary instruments kwa asilimia 95. Serikali ya Kenya huachia mashirika ya nje (BWs) kuchangia asilimia 5 tu ya bajeti na hii ni baada ya BWs kuomba kuchangia bajeti ya Serikali ili wasiwe useless/irrelevant.
Nakumbuka wakati wa Kibaki BWs walitaka kuleta mambo ya GBS ya hapa kwetu, kujadili michango yao ya ku-finance bajeti ya Serikali hadharani, Kibaki aliwaeleza kuwa Serikali yake haijadili mambo ya budget financing hadharani, kwamba siyo utamaduni wa Kenya na iwapo BWs wangeshindwa kuvumilia utamaduni huo wa Kenya, Serikali ilikuwa radhi kutopokea hiyo asilimia 5 yao ya nyongeza katika bajeti ya Serikali ya Kenya. BWs waliufyata mpaka leo.
Lakini pia sekta ya fedha ya Kenya inasimamiwa vilivyo siyo holela kama hapa kwetu. Huwezi kuona wananchi waki-transact kwa kutumia dola au euro bali Ksh. Export component ya Kenya ni kubwa na nchi ina comprehensive strategy ya uchumi, mfano tujiulize kiasi cha dola kinachoingizwa nchini humo kutokana na travel service export ya KQ. Tujiulize maduka kama ya NAKUMATI, Mabenki, manunuzi yanayofanywa na Ofisi za Umoja wa Mataifa (Giligili?) na kadhalika, yanayouza bidhaa na/au huduma nje ya Kenya yanaingiza dola/euro kiasi gani nchini humo. Kenya ina mkakati mkubwa unaotekelezwa na kila Mkenya kuhakikisha uchumi wa nchi unabaki imara.
Salam kwa MNEC Magesa.
Kaiza
..... mwaka 2008 Serikali ya Zambia ilifuta mikataba (MDAs) yote ya uchimbaji madini iliyokuwepo baada ya kuona nchi yao hainufaiki na mauzo ya shaba nje ya nchi. Sheria mpya ya madini ilitungwa na kuachana na mambo ya MDAs (ushauri wa BWs). Kampuni zinazotaka kuwekeza nchini Zambia hufuata taratibu za kisheria za kupewa/kununua leseni za uchimbaji na kuingia kazini. Hakuna misamaa ya kodi wala ruzuku kwa makampuni ya wawekezaji kama Tanzania inavyofanya. Zambia inadhibiti mauzo yote ya shaba nje ya nchi. Leo hii nilipokwenda kununua ZKwacha hapa Lusaka nimekuta Kwacha 7 zinanunuliwa kwa dola 1.
Tunachojifunza kutoka Zambia ni kuwa Serikali ikifanya maamuzi sahihi na kuweka sera sahihi, uchumi wetu unaweza tena kurudi kwenye reli; hata shilling 5 kununua dola moja ya Marekani kama ilivyokuwa mwanzoni mwa miaka ya 1980.
Salamu kwa MNEC Magesa.
Kaiza
--
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanataaluma wa Tanzania" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanataaluma...@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
Habari zenu?
Mimi naona shilingi inaporomoka kwasababu tuna Viongozi wenye mamlaka ya kuleta mabadiliko lakini HAWAJITAMBUI na KUTEKELEZA wajibu wao. Tuna wataaluma waliosoma lakini HAWAJITAMBUI na KUTEKELEZA wajibu wao.
Nchi ni kama familia haina tofauti na Mzazi anaezaa tu watoto alafu ANAZEMBEA kutimiza wajibu wake kama Baba au Mama.
Nchi ni kama kuendelea gari highway na inaendeshwa na dereva mwenye DHARAU MJUAJI HASHAURIKI lazima utaokotwa korongoni tuu.
Hata uwe na team nzuri kiasi gani kama HUTOI FURSA watu kufanya mambo ya kisomi na wewe kiongozi UKAYASIMAMIA kwa maendeleo ya taifa you are doomed.
Kiongozi MBINAFSI lazima ataua uchumi kwasababu anawaza TUMBO lake tuuuu wakati kiongozi anatakiwa KUJIKANA NAFSI YAKE na KUSIMAMIA MASLAHI YA UMMA.
Kinachoendelea kwenye uchumi wetu hakijitaji rocket science Hali ya uchumi au shilingi itaimarika sio kwaajili ya kwenda seminar na makongamano bali kwa MIMI na WEWE kuacha UBINAFSI na kutenda na kusimamia HAKI na UWAJIBIKAJI kwa manufaa ya Watanzania.
Wasalaam
Salome
Mwalimu alisema, "It can be done, play your part".
Nakubaliana na mtaalam Salome..
Tuko wote jamani?
Tuokoe Shillingi yetu kwa namna mbali mbali....kuanzia hapo mtu ulipo..
Shukrani.
Yassin
--
Mwalimu alisema, "It can be done, play your part".
Nakubaliana na mtaalam Salome..
Tuko wote jamani?
Tuokoe Shillingi yetu kwa namna mbali mbali....kuanzia hapo mtu ulipo..
Shukrani.
Yassin
On 30 Apr 2015 19:41, "Salome Mallamia" <salomem...@gmail.com> wrote:
Habari zenu?
Mimi naona shilingi inaporomoka kwasababu tuna Viongozi wenye mamlaka ya kuleta mabadiliko lakini HAWAJITAMBUI na KUTEKELEZA wajibu wao. Tuna wataaluma waliosoma lakini HAWAJITAMBUI na KUTEKELEZA wajibu wao.
Nchi ni kama familia haina tofauti na Mzazi anaezaa tu watoto alafu ANAZEMBEA kutimiza wajibu wake kama Baba au Mama.
Nchi ni kama kuendelea gari highway na inaendeshwa na dereva mwenye DHARAU MJUAJI HASHAURIKI lazima utaokotwa korongoni tuu.
Hata uwe na team nzuri kiasi gani kama HUTOI FURSA watu kufanya mambo ya kisomi na wewe kiongozi UKAYASIMAMIA kwa maendeleo ya taifa you are doomed.
Kiongozi MBINAFSI lazima ataua uchumi kwasababu anawaza TUMBO lake tuuuu wakati kiongozi anatakiwa KUJIKANA NAFSI YAKE na KUSIMAMIA MASLAHI YA UMMA.
Kinachoendelea kwenye uchumi wetu hakijitaji rocket science Hali ya uchumi au shilingi itaimarika sio kwaajili ya kwenda seminar na makongamano bali kwa MIMI na WEWE kuacha UBINAFSI na kutenda na kusimamia HAKI na UWAJIBIKAJI kwa manufaa ya Watanzania.
Wasalaam
Salome
On 30 Apr 2015 18:43, "mwitondi via Wanataaluma wa Tanzania" <wanat...@googlegroups.com> wrote:
I was just about to make an online remittance to Tanzania only to realise that our currency is not listed. Anyone knows why?
Sent from my iPhone
On 29 Apr 2015, at 20:53, Bubelwa E. Kaiza <bubelw...@fordia.org> wrote:
Mrema,
Umeongea kiasi fulani ila sababu zakushuka kwa Tzs. dhidi ya dola yakimarekani ni hizi zifuatazo:-
1. Kuvuja kwa uchumi (economcleakage)/matumizi holela ya dolakwenye mzunguko wa ndani ya nchiwa fedha. Duniani kote, kuendeshauchumi imara kunahitaji mikakati nataasisi imara za kusimamia sera,sheria na kanuni za fedha. NchiniUfaransa, kwa mfano, hairuhusiwikubadilisha/kununua Euro taslimzenye thamani ya zaidi ya dola1000! Afrika ya Kusini hairuhusiwikutumia dola/euro isipokuwa randtu unaponunua mali au hudumayoyote (hotelini, ticket za ndagen.k). Hapa nchini kwetu hali nishaghala baghala – mamlakazinazopaswa kusimamia uchumi wanchi hazifanyi chochote; bureaux de change zinahamisha mauzo ya kilasiku ya madukani kwenda nje yanchi.
2. Watu, hasa mafisadi, kutorosha/kuhodhi dola nje ya nchikutokana na hofu ya uchuguzimkuu. Hali hii inasababisha uhabawa dola hivyo kutengeneza artificial appreciation ya dola kutokana namsingi mkuu wa uchumi wademand vs. supply.
3. Tanzania kutokuwa na dhahabuya kuuza nje ya nchi (dhahabuinayochimbwa siyo ya kwetu bali niya makampuni yanayochimba(wawekezaji) na zaidi ya 90% yamauzo ya dhahabu na madinimengine nje ya nchi hairudishwinchini bali yanabaki huko (clauses za MDAs zinatoa fursa hizo kwamakampuniya madini) nyumbanikwao na wawekezaji. Kwa kifupiTanzania siyo gold mining countrybali ni source of gold, hivyo haimilikimadini yanayochimbwa nchinikwake bali madini husika humilikiwana nchi mama wa makampuni yawawekezaji.
4. Kuwa na weak manufacturing, construction and professional services industries hivyo nchikutegemea imports zaidi kulikouwezo wa kuuza huduma na bidhaanje ya nchi. Aidha mauzo ya mazaoya kahawa, pamba, katani na chainje ya nchi yamepungua kufikianegligible value. Nchi isipouzabidhaa na huduma za kutosha njeya nchi haiwezi kuwa na akiba yakutosha ya fedha ya kigeni. Na kwamukhtadha huu, thamani ya fedhaya nchi haiwezi kuimarishwa napesa ya misaada au mikopo kutokakwa wafadhali au mashirika yaBretton Woods.
5. Impact ya wizi wa pesa yaakaunti ya Tegeta Escrow (wafadhilikuzuia pesa ya misaada ya kibajeti). Zipo sababu nyingine piazinazoathiri uchumi wa nchi (kuwawa hovyo) kama Tanzania ambazowatu wake wengi badohawategemei maarifa na ujuzi, baliardhi na bidhaa, hususan kutokanana tasnia ya uziduaji.
Najua MNEC-CCM Magesaanatafuta hoja za ku-pacify halimbaya inayokikabili chama chakeila ukweli ndio huo (free consultancy).
wanabidii+...@googlegroups.comUtapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Phares,
Asante sana kwa kuanzisha mjadala mzuri na pia shukrani kwa wataalam waliotufungua macho. Nadhani sasa tinahitaji kuweka mkazo kwenye nini kifanyike. Kama walivyoeleza wataalamu kila mmoja wetu anapaswa kuchukua hatua pale alipo. Pia nimefurahi hakuna ushabiki wa kisiasa wa waziwazi.
Nashauri wewe Phares ukiwa kama "moderator" wa mjadala au uchague mmoja mwenye ujuzi wa masuala haya ili atusaidie kukokotoa maoni yaliyotolewa na kuandaa andiko (paper) ambayo itaisaidia serikali na sisi wote. Kuna mmoja alisema "free consultancy" mimi naita mchango wa wataalam kwa nchi yao.
Kwa mfano, mimi ni mpenzi wa kahawa ya kupikwa kwa mashine (brewed coffee) na juzi nilipita kununua paketi yangu ya kila mwezi. Nikashangaa imeongezeka bei kwa sh elfu mbili. Nikauliza kwa nini imepanda bei maana haihusiki na dola ya marekani. Kahawa ni ya Rift Valey Mbeya na Zanzibar. Nikaambiwa mwenye duka la kahawa (Coffee Shop) ni mtu wa nje hivyo bei inategemea dola. Ila sidhani bei itapungua shilingi ikiimarika.
Swali: hapo mimi kama mlaji nitachukua hatua gani? Je ni nani anapaswa kulinda walaji kutokana na wafanya biashara nyemelezi (opportunists) kama hawa. Nadhani mifano mingi ipo ya kitaalam kwa wachumi au ki muma kama niliotoa mimi.
Hilo andiko ninalopendekeza liainishe hatua za kila mtu na kila taasisi za kuchukukua ili kuinusuru shilingi yetu. Na baada ya miezi mitatu tufanye mjadala kama huu kuangalia kama mapendekezo yetu yatakuwa yamefanyiwa kazi.
Naomba kuwasilisha,
Ipuge
------------------
Dr. Yahya A. Ipuge M.D., MMed.
Senior Health Specialist
Wazo Hill,Tegeta
P.O. Box 66764
14130 Dar es Salaam
...............lakini ili mapendekezo haya yaweze kutekelezeka, kila mmoja wetu ajiangalie na kujitathmini juu ya mahali alipo na majukumu yake, halafu ajiulize, Je, nimefikia hapa nilipo kwa professional competence merit na kwa kupitia a due process?
Ni wale tu watakojijibu, NDIYO tunaoweza kutekeleza au kuwawajibisha wahusika kutekeleza mapendekezo yaliyainishwa hapa chini.
Kaiza
From: wanat...@googlegroups.com [mailto:wanat...@googlegroups.com] On Behalf Of Janet Mbene
Sent: 01 May 2015 01:09
To: wanat...@googlegroups.com
Phares,
Asante sana kwa kuanzisha mjadala mzuri na pia shukrani kwa wataalam waliotufungua macho. Nadhani sasa tinahitaji kuweka mkazo kwenye nini kifanyike. Kama walivyoeleza wataalamu kila mmoja wetu anapaswa kuchukua hatua pale alipo. Pia nimefurahi hakuna ushabiki wa kisiasa wa waziwazi.
Nashauri wewe Phares ukiwa kama "moderator" wa mjadala au uchague mmoja mwenye ujuzi wa masuala haya ili atusaidie kukokotoa maoni yaliyotolewa na kuandaa andiko (paper) ambayo itaisaidia serikali na sisi wote. Kuna mmoja alisema "free consultancy" mimi naita mchango wa wataalam kwa nchi yao.
Kwa mfano, mimi ni mpenzi wa kahawa ya kupikwa kwa mashine (brewed coffee) na juzi nilipita kununua paketi yangu ya kila mwezi. Nikashangaa imeongezeka bei kwa sh elfu mbili. Nikauliza kwa nini imepanda bei maana haihusiki na dola ya marekani. Kahawa ni ya Rift Valey Mbeya na Zanzibar. Nikaambiwa mwenye duka la kahawa (Coffee Shop) ni mtu wa nje hivyo bei inategemea dola. Ila sidhani bei itapungua shilingi ikiimarika.
Swali: hapo mimi kama mlaji nitachukua hatua gani? Je ni nani anapaswa kulinda walaji kutokana na wafanya biashara nyemelezi (opportunists) kama hawa. Nadhani mifano mingi ipo ya kitaalam kwa wachumi au ki muma kama niliotoa mimi.
Hilo andiko ninalopendekeza liainishe hatua za kila mtu na kila taasisi za kuchukukua ili kuinusuru shilingi yetu. Na baada ya miezi mitatu tufanye mjadala kama huu kuangalia kama mapendekezo yetu yatakuwa yamefanyiwa kazi.
Naomba kuwasilisha,
Ipuge
------------------
Dr. Yahya A. Ipuge M.D., MMed.
Senior Health Specialist
Wazo Hill,Tegeta
P.O. Box 66764
14130 Dar es Salaam
---------- Forwarded message ----------
From: Janet Mbene <maor...@gmail.com>
Date: Friday, May 1, 2015
Kuna rafiki yangu alichaguliwa Uwaziri nikamuuliza je kuna fanicha yeyote ndani ya wizara yenu made in Tanzania? Akanijibu kuwa mostly zote ni imported. Two months ago nikamuuliza swali lile lile, akanijibu kuwa kashindwa kupambana na 10% za procurement. Tuendelee kupiga soga tu labda Mungu atatusikia atusaidie!t.
Sent from my iTochi powered by UhuruOneWapendwa wapenda maendeleo wenzangu.Naona tumelifungumzia na kulizungusha hili janga vya kutosha. Sasa tuingie mitamboni tufanye kazi zetu kwa bidii kama alivyoshauri NW Janet Mbene....Ni sawa lakini sijapata kusoma taarifa rasmi kwamba, hili janga lilitokeaje kwa ghafla? Na kuna viona mbali vya namna gani vipo au vitawekwa ili kuepusha kugonga mwamba tena?Ndio Tsh itatulia baada ya mikopo...lakini, hiyo itakua kama kutuliza maumivu tu. Inabidi kuwe na mbinu tofauti zilizokuwepo hapo zamani....Tufufue Sector ya uzalishaji ...yaani ni kuanzia shughuli za SIDO vijijini hado vikubwa kama NECO badala ya kuwa na Showrooms along Nyerere Road kwa Dar na miji mingine. Kwa fani yangu ya uhandisi naumiza kuona wahitimu wakibakia jufura vifaa vumbi kwenye showrooms ambavyo angeviteneza laiti angeajiriwa kiwandani...nk. Tumegeuka soko kirahisi by 100%....Eti kwa sababu bidhaa zetu hazifikii kiwango cha soko la kimataifa? Tutavitumia wenyewe kwani tuna TBS yetu ya kuangalia Ubora na Viwango.....Kama dada Mbene alivyoshauri, ....."Tujitambue" ...Tusonge mbeleYassinSent from Samsung Mobile
--
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanataaluma wa Tanzania" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanataaluma...@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
--
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanataaluma wa Tanzania" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanataaluma...@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
?
Sent from my Xperia™ S
Phares,
Naona hadidu za rejea ziko tayari. Mimi ni mtaalam wa afya hivyo itakuwa vigumu kuandika vizuri andiko la kiuchumi. Ñashauri wenzangu waanze mimi ntakuwa mmoja kati ya wapitiaji (reviewer )wenye ''layman's lens".
Nashauri Buberwa Kaiza atusaidie rasimu ya kwanza kutumia hizo hadidu za rejea
Ipuge
------------------
At May 5, 2015, 9:19:07 AM, Phares Magesa<'pma...@gmail.com'> wrote:Wenye maoni yoyote kuhusu suala hili sasa wapeleke kwa kamati ndogo tuliyopendekeza ili yaunganishwe katika andiko ambalo tumewaomba wenzetu watusaidie kuliandika ili lije litolewe rasmi kwa umma kama kauli yetu wote. |
|
|
Mr President naomba usajili wa email yangu ubadilike kwenda kwenye email ya pmasa...@gmail.com Asante |