Shirikisho la mpira wa kikapu Tanzania (TBF) linayo furaha kuwatangazia kuwa tunatarajia kushiriki mashindano mbalimbali ya kimataifa mwaka huu 2019.
Mashindano hayo ni kama ifuatavyo :
i. U16 Zone V Nations Cup (Boys & Girls) 10-15,Jume 2019, Rwanda
ii. Senior Zone V Nations Cup (Men & Women) 25 June - 1 July, 2019, Uganda
Washindi wa Mashindano hayo yote ya kanda watashiriki mashindano ya kutafuta bingwa wa Kikapu Afrika kwa timu za Taifa.
Nchi zitakazoshiriki mashindano hayo yote ni Tanzania, Uganda, Kenya, Ethiopia, Rwanda, Burundi, Somalia, Egypt, Eritrea, Sudan na South Sudan.
Makocha watakaosimamia timu hizi kwa Senior teams ni Ashraf Haroun na Suleiman Tasso na Pascal Nkuba, Agnella Semwaiko, Muhoja kwa wanawake na kwa upande wa U16 Makocha watakuwa Bahati Mgunda, Mohamed Mbwana, Peter Louis na Dennis Lipiki.
Walimu hawa wameshateua wachezaji watakaoingia kambini kuanza mazoezi kujiandaa na mashindano hayo kama ilivyo ambatanishwa.
Jumla ya fedha zinazohitajika kufanikisha ushiriki wetu katika mashindano haya yote ni Tshs. 100M.
Tunaomba Watanzania wote tuungane kifanikisha ushiriki wa Tanzania katika mashindano hayo na kuhakikisha tunashinda katika mashindano haya ya kanda ya tano ili tupate nafasi ya kushiriki mashindano ya kikapu ya Afrika na baadae ya dunia.
Tunakaribisha makampuni, taasisi za umma na za binafsi, na watu binafsi kila mmoja anakaribishwa kuchangia kwa hali na mali.
Phares Magesa
Rais,
Shirikisho la mpira wa kikapu Tanzania (TBF)
www.tbf.or.tz