re: TUNAENDELEA!

8 views
Skip to first unread message

stella egidio

unread,
Jun 5, 2013, 4:16:59 AM6/5/13
to SELELI EDWIN, Roselyne Massam, Sabina Nyoni, Ritha Semizigi, Rose Shirima, Rita Mandara, Sayuni Mariki, Shadrack Mrita, stella simkoko, Salome Magaya, Stella Jambo, rehi...@yahoo.com, shija msikula, Shija Msikula, stella...@yahoo.com, seme kennedy, Tausi Ingabire, samora macrice, smw...@gmail.com, Tecla Dominic, Shogo Mlozi, samb...@yahoo.co.uk, Rkyeli...@gmail.com, Rukia Adam, Rehema K. Shao, Straton Kimario, Sarah Seme, Sydney Mkamba, steve...@gmail.com, Rogers Fovo, Salum S. Yusufu, Richard Kerissa, suza...@yahoo.com, swafia....@tigo.co.tz, sos...@hotmail.com, solidarity...@gmail.com, rwandi...@yahoo.com, stanle...@yahoo.com, shidu...@yahoo.com, sweetm...@hotmail.com, smbo...@yahoo.co.uk, suzana...@yahoo.com, smz...@yahoo.com, sse...@yahoo.com, qutti...@yahoo.com, rmnd...@nhctz.com, Ray...@kings.co.tz, rose seth, Sarah Mwingira, ritchm...@gmail.com, Vero James, veronica James, Zahara Amiri, Vivian Macha, Twitike Mwamundela, Tina Geleja, Tulibako Ulanga, Vicky Kamata, Tumsifu Elly, tutty mwankusye, Wende Caren Luvinga, yared dondo, vicky david, Tunu Mwiru, Tunu Mwiru, Wanagosheni, Upendo Mfalila, v_m...@yahoo.com, Zablon Mdeka, Tuwaha J. Mkunga, Veneranda N.. Lyimo, Victor Kimaro, Wolfgang E. Salia, Zawadi Nzota, tple...@yahoo.com, vgamb...@yahoo.com, wvi...@yahoo.com, tengani...@yahoo.co.uk, ve...@muvek.co.tz, vivia...@yahoo.com, viv...@yahoo.com, veronica...@yahoo.com, willso...@yahoo.com, tubas...@yahoo.com, zmas...@yahoo.co.uk, yoe...@yahoo.com, vk...@esrf.or.tz, waka...@state.gov, tunu...@yahoo.com, tuli...@yahoo.com, wema....@gmail.com, VS...@nhctz.com, tito....@total.co.tz, veneran...@tra.go.tz, tumain...@mkono.com, Veila Shoo
Wandugu, tunaendelea kujifunza. Jana tuliona jinsi tulivyo kwenye dunia hatarishi, kwamba kila eneo shetani yupo ili tu kututaabisha na kutumiza. Tuliona kwa wasusi Mwenge,Kinondoni na kwingineko,jinsi nguvu za giza zilivyotawala na wasusi wakakiri kwamba hata wao pia wameshakumbana na "wateja wa kipepo" vile vile. Kuna msomaji ametuma ushuhuda wake jinsi mkasa kama huo ulivyomkuwa Mwenge pale, alienda kusuka "yebo yebo" lakini kila anavyosukwa, anajikuta anaishiwa nguvu, anaomba break kwa msusi ili apate fresh air,lakini akianza tena kusukwa, anaishiwa nguvu, ikawa ni mtindo huo mpaka amemaliza kusuka. Sasa akajaribu tena kwenda kwa msusi huyo huyo siku nyingine tena, yakamkuta hayo hayo, lakini akienda saluni nyingine, anakuwa kawaida tu, anasuka mpaka anamaliza bila kuishiwa nguvu, akagundua kwamba msusi yule " ana namna nyingine". Dada martha Please, if you won't mind, share your testimony. na mwingine amejibu kwenye FB kwamba, yeye alienda kusuka hapo MWenge, lakini alipomaliza kusuka akaumwa sna na kichwa, kumbe yule msusi alimkata nywele kinamna fulani, akanywa panadol kichwa hakikupona, usiku alipolala the same day, akamwota yule yule msusi anamkata nywele na kuondoka nazo, basi alipoamka haraka sna akawahi kwenye maombezi, anasema akaenda tena next time kwa msusi yule yule, lakini safari hii alipoenda, msusi yule " alimnunia" na hakuwa tayari kumsuka tena. Hivi vitu vipo wandugu. Hebu dada Emma Loth tafadhali shusha hapa huo ushuhuda for the people of God to learn from you.
 
Sasa leo, niliahidi kuangalia  kwenye "kiliniki" za kina mama na labour ward  nako kuna nini.Lakini kabla ya hapo, hebu tukumbushane tena jamani,hivi huu si ndo mwezi June huu? shule zimefungwa watoto wetu wamesharudi likizo, tunao majumbani, hebu zoezi la "kupekenyua" na lianze wazazi, eee? I'm conviced kabisa kwamba tuanze hili zoezi tukague vyumbani kwa watoto wetu, mabegi yao ya shule, simu zao na n.k wandugu, kuna wale wazazi/walezi wenzangu wanaosema kwamba, huko ni kumvunjia mtoto heshima, lakini naomba nikwambie hivi, mtoto kwa mzazi HAKUI,  kwa hiyo ni ruksa kumpekenyua binti yako au kijana wako, ni mpaka pale atakapoenda kwenye matrimonial Home yaani akioa au kuolewa hapo sasa inakuwa  sio "role" yako ya Kupekenyua, inahamia kwa Spouse wake. Wandugu, nasisitiza pekenyueni. Nina shosti yangu humuhumu, aliingia chumbani kwa binti yake, kutafuta sijui kitu gani, hee, si akakumbana na "njemba" imejificha kwenye kabati? Mhh! Kijana yule alitetemeka sna, hakuweza hata kujieleza, binti kuulizwa huyu nani kafikaje humu ndani kwangu, macho yamemtoka kama fundi saa, sasa wee unayesema unaogopa kumvunjia mwanao heshima, subiri akuvunjie wewe heshima kama hivyo!
Kuna huyu mzee fulani wa kule mbezi Beach, kwakweli huyu simwelewi mpaka leo, haya mambo ya kusema mtoto yuko above 18 kwahiyo ni mtu mzima, hayafai kabisa, sasa kama ni mtu mzima si akajitegemee? Yaani mzee, ana binti yake alikuwa anasoma chuo huko Ug, akija likizo binti anakuja na "boy friend" wake pale kwa wazazi wake, na analala naye chumbani kwake, mnapata picha wandugu? sasa kwa sababu ni wazazi wanaogopa kumkwaza mtoto, walichokuwa wanafanya ni baba yake binti usiku halali mle ndani, anakwend akulala nearby Hotel au guest house, anasema kwa kikabila chao, "Nimwiko mtoto kulala na boyfriend wake kwenye nyumba ya wazazi wake kama hawajafunga ndoa.Jamani wandugu, haya ni MALEZI BORA kweli, au kuvunjiana heshima? Yaani baba ndo ampishe binti ndani ya nyumba? Kisa nini? anaogopa kumkwaza! of which alipaswa kumwambia binti yake kwamba huyo mgeni afikie hotel, watakutana kwa wakati wao, au sio jamani? sasa huku ndo kulea gani? Ukiogopa kumkanya mtoto kwa kuogopa kumkwaza, subiri basi akukwaze wewe, kwa kumfungia kijana kabatini! Hata Biblia inasema, "Asiyetumia fimbo yake, HUMCHUKIA mtoto wake,", yani kwa lugha nyingine kama unampenda mtoto wako lazima utamwadhibu ili kumrekebisha! 
 
Sasa kule clinic jamani, wapo manesi pia ambao ni "mawakala wa ibilisi, na kwenye leba wodi nako pia wamejaa. Hujasikia story watuwanasema,hee, akiwa zamu nesi fulani, wamama wanakufa keli kweli jamani sijui ana mkosi gani? Au doctor fulani akikufanyia operation lazima tu utakufa,   hamjasikia haya wandugu? Nimeona kijana fulani Mhandisi menye masters yake, lakini kila akipata kazi anafukuzwa, ameoa lakini gharama hata za kulipa chumba kimoja cha kulala hawezi, analala kanisani. Yani alikuwa akitaabika sna na maisha, akaamua kumtafuta Mungu na kwenda kwenye "maombezi". kufika huko, pepo si likapanda bwana? Likasema huyu ni mali yetu tulikabidhiwa na tumemsajili kuzimu sike ile ile alipozaliwa, mh! mchungaji kuuliza, mali yenu kivipi au mlimpataje? yale mapepo yakasema, siku alipozaliwa, wakati mama yake anajifungua, nesi aliyekuwa anamzalisha ni wakala wetu, kwa hiyo baada ya kutoka tumboni mtoto alipolia tu, nesi "akampulizia pumzi mdomoni", mtoto yule akawa mali yetu. Simnakumbuka hata Mungu alipomuumba mwanadamu, tunaambiwa "akampulizia pumzi ya uhai puani mwake, na mwanadamu akawa NAFSI HAI? Mpo hapo wandugu? nimeona kwa macho yangu kabisa LIVE na wala sijasoma kwenye kitabu. Wandugu, kama ambavyo Mungu anao watumishi wake kila mahali, na shetani naye kadhalika anao ili kuharibu. kwa hiyo ushauri wangu kwa wakina mama "Kijacho" wote mlioko humu, mnapoenda kiliniki, hebu mwombeni Mungu kwanza, akutangulie, akuandalie daktari mzuri wa kukuhudumia, na siku ya kujifungua usali pia Mungu akuandalie wahudumu sahihi ili usije kuangukia kWenye mikono ya hawa "mawakala waharibifu". Sio siku ya kiliniki unachokumbuka wee ni kuchukua kadi tu na kuwahi namba kwa Dr. Shafiq au kwa Profesa Mgaya pale, halafu hukumbuki kumwomba Mungu.
 
Hebu nisiwachoke sana, kesho tutaangalia hawa omba omba au "beggars" wa mitaani nao ni kina nani na wametoka wapi.
 
Stay tuned!
 
Stella.
 






Charles Abihudi

unread,
Jun 5, 2013, 9:04:03 PM6/5/13
to wana-...@googlegroups.com
Dear Stella God has anointed you with special concern of social issues! First start to write books! Second you need to create a blog! You will reach many people/ universe/ Global in a second! With lots of Love! Friend Rev Abihudi! Blessings!!

Sent from my iPhone
--
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wana Goshen" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wana-goshen...@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 

stella egidio

unread,
Jun 6, 2013, 1:00:53 AM6/6/13
to wana-...@googlegroups.com
Thank you so much my darling pastor,
I will do the needful.
Stella.
Reply all
Reply to author
Forward
0 new messages