Sasa leo ndo tunahitimisha ile mada yetu ya MAJINA YA WATOTO, tuliona juzi na jana athari za kurithisha watoto majina ya bibi au babu zao, na pia kwa wale waliofoji vyeti pia tuliwaangalia kwa jicho kali zaidi kwanini umwite mkeo, au watoto
wako kwa jina la yule unayetumia cheti chake kazini au shuleni wakati pengine yule mtu alishakufa siku nyingi! sasa leo tuangalie kwa wale "ladies", walioolewa halafu kwa sababu moja ama nyingine hawataki KUKUBALI kutumia majina ya waume zao, au tuseme, wanaendeela kutumia maiden names for some reasons hawataki au hawapendi kutumia
marital names.
Ikumbukwe kwamba, unapoolewa na huyo bwana, Mungu wake anakuwa Mungu wako, watu wake wanakuwa watu wako, yaani kwa kifupi your husband owns you. Hebu kwa kuanzia tuangalie Mwanzo 5:1, pale ambapo Mungu alianzisha ndoa ya kwanza, "Hiki ndicho kizazi cha Adam, siku ile Mungu alipoumba mtu, kwa sura ya Mungu alimfanya, MWANAMUME NA MWANAMKE aliwaumba, AKAWABARIKI, akawaitwa JINA LAO ADAM, siku ile alipowaumba".
Hivi sijui umeelewa hapo msomaji wangu? aliwaumba wawili yaani mwanamke na mwanaume, lakini AKAWAITA JINA LAO, Adam. Bila shaka ushanielewa hapo, kwamba siku ile ulipofunga ndoa, wewe Flora Egidio, uliitwa Benjamin, au wewe mary uliitwa Steve.
Kitu ninachotaka tuangalie hapa, ni lile jina la baba yako , yaani Egidio, ndo mwisho wake pale, mpaka siku ya kufa ndo msalaba wako sasa ule utaitwa tena R.I.P FLORA EGIDIO au death certificate yao itandikwa jina lako na mzazi wako sio jina la mumeo tena. Wote tunajua kabisa kwamba kinachotenganisha ndoa ni KIFO, kwa hiyo HAPO SASA HATUTASEMA MAREHEMU FLORA BENJAMIN MAIRA, TUTASEMA MAREHEMU FLORA EGIDIO. Nakumbuka hata mama yangu alipofariki majuzi, hatukuandika kwenye msalaba wake marehemu Cecilia Egidio, tuliandika marehemu, CECILIA PHILIPO BINYARUKA. Yaani kabisa kwamba kifo ndo kimeuondoa ule umiliki wa jina la baba yangu. Mpo hapo wandugu? Wote tunajua kwabsia kwamba, kuna kusoma then tunaanza kazi kabla hatujaolewa, kwa hiyo nitaliachaje jina la baba yangu? nenda kwa afisa utumishi wako, mpe nakala ya cheti chako cha ndoa, basi utabadilisha, mbona kwenye kadi ya Bima ya
afya tunapeleka vyeti vya ndoa jamani, na waume zetu tunawaweka kwenye orodha ili watibiwe? sas ahapo tunashindwaje? utasema umesomea jina lako flora egidio, mpaka ukaajiriwa kwa jina hilo sasa itakuwaje? unachaotakiwa kufanya unaliondoa tu lile jina la kwanza ba baba yako jina la ukoo wako unaweka initial tu, then unalijaza hilo la mumeo, kama ni Alex Kakakuuoana, au JOhn Kalikumtima, au Steve Byakugira utajua mwenyewe. Mfano, wewe unaitwa Flora Aloyce Egido, unafuta Aloyce, unaweka Flora E.Maira, mpo hapo wadada? Huo ni mfano tu, huyo flora ni immediate sister angu, wa kuzaliwa kwa hiyo kutumia mfano wako, isiwatishe!
Sasa tuangalie unakosa nini wewe shosti yangu, unapo "ng'ang'ania" kwamba hutaki kuitwa jina La Frank Shayo au, au Benjamin Maira? Kumbuka "Mungu AKAWABARIKIA, akawaambia
zaeni mkaongezeke, mkaijaze nchi na kuitiisha, mkatawale samaki wa baharini na ndege wa angani, na kila KIUMBE CHENYE UHAI KIENDACHO JUU YA NCHI" Mwanzo 1:18. Kwa hiyo ujue kabisa unakosa vitu vifuatavyo: (1) unakosa zile baraka alizotamka Mungu juu ya ndoa yako (2) Unakosa haki ya kutawala viumbe hai vikiwemo hata kuku unaofuga kwenye banda lako, ndo maana hawaishi kukufia kwa mdodndo bandani hapo.
(3) Kuijaza nchi na kuitiisha. Shosti unakosa haki ya kuitiisha nchi, ndo maana hata ukipanda mchicha pengine hata hauoti, ukipanda maua hayachipui, unashindwa hata kuitamkia ardhi ikutii, maana hutaki kutumia jina la mumeo ambalo kwa hilo ndo umepewa kibali au ruhusa na Mungu ya kutawala vitu na kuvitiisha, usidhani mzaha shosti angu! Mende ndani kwako hawakauki, mbu kibao, panya nao ndo kabisa kama vile ni family members wako, maana huwezi kuwatiisha na kuwatamkia kwamba waondoke nyumbani kwao! ahaaaa! jamani, It sounds funny but that's the
reality.
Kuna dada mmoja alitupa ushuhuda wake , alikuwa kwenye ndoa kwa miaka kadhaa, lakini akasema yeye hataki kusikia anaitwa Mrs. fulani, yaani jina fulani la Kihaya ambalo halitamkiki vizuri mdomoni, jamani, hakujua impact yake kwenye ulimwengu wa roho ikoje, guess what! yule mdada alikosa mtoto, kafanyiwa vipimo na vipimo vyote vya kitaalamu hakukutwa na tatizo lolote, akaamua
kurudi kwa Mungu na kuuliza, Mungu akamwambia, sasa wewe utapataje mtoto wakati hujaolewa? akamwambia Mungu unamaana gani? Mungu akamwambia wewe ushasema "Utabaki kuitwa Joyce Robert (mfano tu wa jina la kwao), lakini hutaki kuitwa Mrs. Rose Robert Masawe, na baraka za kuzaa na kuongezeka ni kwa WALE TU WALIOOANA. Mbona jasho lilimtoka? kwa hiyo wandugu, hivi vitu vina impact sna kwenye maisha yetu.
Lakini pia vile ukumbuke kwamba hata wewe uliyeoa, Neno linasema, " Apataye mke apata kitu chema, naye AJIPATIA KIBALI kwa Mungu. Ina maana kwamba, wewe kijana "bachela" huna
kibali machoni pa mMungu, ni mpaka pale unapooa! Ndo maana una-struggle na vitu vingine ambavyo pengine wala hukuhitaji kutumia nguvu, simply because, " huna kibali machoni pa Mungu.Sasa fanya hima, ukaoe ili upate kibali cha Mungu kwenye maisha
yako.
Wandugu ngoja kwa leo nishie hapa. Kama kuna mwenye mchango wa mawazo, basi unaporusha comment yako, basi utu-copy wote, ili nasie tuweze kunufaika na masomo haya.
Love you all,
Stella Egidio.