3 views
Skip to first unread message

stella egidio

unread,
May 24, 2013, 5:03:19 AM5/24/13
to Vero James, veronica James, Zahara Amiri, Vivian Macha, Twitike Mwamundela, Tulibako Ulanga, Vicky Kamata, Tumsifu Elly, tutty mwankusye, Wende Caren Luvinga, yared dondo, vicky david, Tunu Mwiru, Tunu Mwiru, Wanagosheni, Upendo Mfalila, v_m...@yahoo.com, Zablon Mdeka, Tuwaha J. Mkunga, Veneranda N.. Lyimo, Victor Kimaro, Wolfgang E. Salia, Zawadi Nzota, vgamb...@yahoo.com, wvi...@yahoo.com, ve...@muvek.co.tz, vivia...@yahoo.com, viv...@yahoo.com, veronica...@yahoo.com, willso...@yahoo.com, zmas...@yahoo.co.uk, yoe...@yahoo.com, vk...@esrf.or.tz, waka...@state.gov, tunu...@yahoo.com, tuli...@yahoo.com, wema....@gmail.com, VS...@nhctz.com, veneran...@tra.go.tz, Veila Shoo
Wandugu, zipo faida kukaa na Mungu! Usalama wetu na familia zetu, furaha yetu na chanzo cha mafanikio yetu ni yeye tu!
Tumekuwa tukiangalia mambo mbali mbali "hatarishi' ambayo tunaweza kukumbana nayo katika familia zetu, ambayo adui anaweza kuwatumia vijana wetu wa kazi za ndani. Sasa leo tutaangalia sio hao tu but hata na ndugu zetu tuliowakaribisha kwenye familia zetu pia, wanaweza kuharibu uzao wetu.
Jana niliacha kibwagizo tu cha mdada ambaye alikuwa "hatarishi" kuliko Mchawi, maana mchawi anaweza kuamua kukutesa tu na asikuue, lakini huyu wa leo, mhh! Kama nilivyoanza na hicho kianzio changu kwamba, "Zipo faida kukaa na Mungu, wandugu ni kweli tupu. Ukimfanya Mungu kuwa msaada wako na kimbilio lako wakati wote si wakati wa hatari tu, na yeye atakuwa Baba mwema sana kwako. Yaani tusiwe na uhusiano na Mungu wakati tuna matatizo, basi ndo tunafunga na kuomba na kutoa sadaka ili yamkini MUngu atusaidie, No, but tuwe na mahusiano ya kudumu na Mungu wetu, though najua tupo watu wa Imani mbali mbali humu ndani.
Sasa , nina rafiki yangu tulikuwa tunaishi wote kule Tabata, of course also going in the same church, huyu dada, alikuwa na binti wa kazi ambaye ni mgeni tu alikuwa amekaa naye kama wiki tatu tu hivi. Siku moja akiwa kazini kwake pale Tanesco Ubungo, siku ya Ijumaa, akasikia wazo linamwambia, "House gelo wako, amepanga kuwaua kesho, wewe na familia yako yote! Mhh! wazo hili likarudia rudia sana moyoni mwake, lakini hakuamini kama ni Mungu anasema naye simply because, huyu binti alikuwa ni mgeni ana wiki tatu tu pale nyumbani, na wala hajawahi kuwa na dispute naye, since she is too new to her family. Wandugu, nasititiza tena, ZIPO FAIDA KUKAA NA MUNGU!
Kwakuwa huyu shosti wangu, hakuiamini sauti ya Mungu, na kwa kuwa Mungu ni mwingi wa rehema amejaa huruma, akaamua kumleta mgeni usiku ule ule kwa huyu shosti ili walau kwa kinywa cha mgeni, aweze kuamini ule ujumbe ,kwamba kesho Jumamosi, "Mtakufa". Mgeni huyu akafika pale akala na kunywa na kulala, but mgeni huyu naye aliijua "faida ya kuwa na Mungu", kwa hiyo aliamka usiku kufanya Ibada, while praying in the mid night, Mungu akamwambia amwambie mama mwenye nyumba ule ujumbe, kwamba house girl amepanga kuwaua wote. Hee, akasubiri mwenyeji wake aamke then wazungumze,jamani ndo huyu shosti wangu sasa kuamini kwamba mwee kumbe lile walo la jana pale ofisini, lilitoka kwa Mungu.
Kumbe huyu binti aliahidiwa na jirani kwamba atapewa shs. laki mbili, akifanikiwa kuiangamiza kwa sumu familia ile ya shosti wangu, kwa hiyo akampa na sumu kabisa, ya unga pakiti kadhaa na binti akaamka usiku wa ijumaa, akaweka kwenye maji ya kunywa, ya kuoga, kwenye sukari, kwenye mafuta ya kupikia, kwenye unga wa ugali mpaka kwenye mchele, kwahiyo wewe usiyekula ugali mchana, basi utakula wali usiku! Mpo mpaka hapo wandugu? basi,baada ya mgeni kutoa ujumbe kwa mwenyeji, wakaamua kujifungia c humbmani mwenyeji , mgeni na yule binti na kumwita Mungu kwa sala ili binti akiri na aweze kuwa muwazi zaidi ni nani na kwanini alitaka kufanya vile. Akasema, nimeahidiwa laki mbili, maskini yule binti yamkini zile laki mbili kwake aliona kama bilioni mbili, of which nina uhakika asingepewa hata senti tano zaidiya nauli ya kurudi kwao, maana mwenyeji ameshakufa kwa hiyo hangeweza kurudi kwao.
Sasa mmeona hapo wandugu? kilichomwokoa huyu shosti yangu na familia yake ni Uhusiano wake na Mungu. What if asingekuwa ni mchaji wa Mungu? Angeisikiaje sauti ya Mungu? Mpaka Mungu akaamua kumletea mgeni usiku ule ili ku-rescue familia yake?
Hebu tujifunze kwa familia hii, hawa watu tunaokaa kwenye familia zetu, jamani sio wote ambao " ni wa kwetu", yaani their not part of us, kwahiyo haoni hasara kukuangamiza, wee au mwanao.
Hivi unadhani wale majirani zako pale mtaani kwenu wanafurahi kukuona unatoka asubuhi na mumeo kwenda kazini na gari? Je, wanafurahi kuona kila jioni unaenda site na mafundi umebeba nondo sijui mabati na mifuko ya cement kumalizia "kibanda" chako? Je, wanafurahi kuona unafuatwa na kurudishwa na gari ya kazini, halafu wao wako pale mtaani wanapauka na kunyauka? Je, wanafurahi kuona yule mwanao Brian anamaliza chuo Kikuu, au kwamba kwako kuna send off ya yule binti yako aliyemaliza Mzumbe? Hawafurahi hata kidogo! wanapanga hila kukuangamiza wewe na familia yako, yamkini wanakwendaga nyumbani kwako wee ukiwa kazini kumrubuni kijana wako wa kazi atoe kopi ya funguo la gari lako ili waliibe usiku, kwa hiyo Let's be very careful na hawa watoto wa kazi tulio nao kule makwetu.
Hebu ngoja leo niishie hapa, halafu J3 ntamalizia na ndugu zetu nao, shemeji wale mawifi na vile vipeuo tunavyoishi navyo pale makwetu, are they good to our dear children? umeshawahi kuchunguza? Umeshawahi kuamka usiku ukenda kuchungulia kwa siri mwanao kalalaje na yule aunt ake au anko wake, au yaya anayemlea au unalala tu fofolifo mpaka asubuhi?
Leo aomba niwaachie hili swali wazazi na wale wazazi tarajiwa wenzangu, Je, mmeshawahi kujiuliza, ni kwanini wakati Yesu anakwenda Msalabani, akiwa anapigwa sna na kuteswa, aligeuka nyuma, maandiko yanatuambia, umati mkubwa wa watu ulikuwa ukimfuata unalia pmaoja naye, lakini yeye akawaambia, " enyi wanawake wa Yerusalemu, Msinililie mimi, bali jililieni ninyi na watoto wenu". Kwanini hakusema jililieni ninyi na waume zetu au hakusema, enyi wanafunzi wangu msinililie mimi , jililieni ninyi na wake zenu? Hebu tafakari, halafu chukua hatua ya kuanza leo kumlili Mungu kwa ajili ya watoto wako, wee baba na wee mama, bearing in mind that, We are custodians, but children belongs to God, God has entrusted us with them ,and we will be accountable on that day of Judgement, on how we raised them here on earth! Haya yesu mwenyewe litoa hesbu kabla hajaondoka, si mnakumbuka wandugu kwenye Yohana 17? Alisema," nami naja kwako Baba Mtakatifu, wote ulionipa, sikumpoteza hata mmoja wao".
Nawapenda wote, nawatakia mapumziko mema ya mwisho wa wiki.
Stella A. Egidio.
 
</body>
Reply all
Reply to author
Forward
0 new messages