Ni vyepesi sana tunapoongelea
mambo yanayoweza kumkasirisha Mungu vibaya sana, tukataja haraka dhambi kama
uzinzi, uuwaji,uchawi, makufuru nk, maovu
ambayo ni kweli Mungu hafurahishwi nayo hata nukta lakini pia kuna Kutomwamini,
Kutotii na Manung’uniko.Ni nia ya somo ili kuzumgumzia Kutomwamini
Mungu ilivyo dhambi mbaya kweli kuliko tunavyochukulia au kuzoelea. Nilishangaa
kweli Roho Mtakatifu alivyo ninunurishia nikang’amua ivyo katika baadhi ya
maandiko nitakayoyatumia.
Kutoamini
ni nini kwa mantiki ya kawaida ya maisha haya?
Mfano kama Wazazi watamwambia mtoto kua asiwe na wasiwasi watamsomesha tu, au
Mume akamwambia Mke kua atamnunulia gari/dressing table birth day party ijayo
kisha Mtoto au Mke asiamini maneno ya Wazazi au Mume, maana yake nini? Majibu
ya swali hilo yatakupa picha kwa nini Mungu ali-react alivyo-react dhidi ya
Wana Israel ndiposa tutaelewa tabia ya Kutomwamini Mungu ni issue kubwa mno mbele
za Bwana, tusiichukulie kirahisi hata kidogo. Ikiwa Wazazi kwa kujiamini kabisa
wamemwambia mtoto wao kua watamsomesha au Mume kwa confidence zote kamwambia
Mkewe atamnunulia gari, perfume halafu wasiaminiwe,itakua na maana ya kutiliwa shaka, kupuuzwa,kutojaliwa,kua na wasiwasi
nao, kuwachukulia wao ni ndumila kuwili, waongo-waongo ivi ,hawa aaminiki kwa
njia yoyote, ni hatari kuweka tumaini kwao, niku-risk status/personality yako
kwa kua any time utavuna aibu maana hawatatimiza ilihali kwa furaha yako
umeshawaambia rafiki zako( shuhudia). Pia Kutowaamini ni kujiuliza-uliza
maswali negative dhidi ya yao, kisitasita,kuogopa, kutilia shaka mpaka uwezo wa
Mzazi na Mume, ni kusema kua hapa nimeahidiwa lakini hamna lolote huyu bwanaa.
Kwa upande mwingine wa Mhusika( Wazazi/Mume) watakapokua hawaaminiwa inapelekea
kujisikia vibaya, kudharauliwa, kushushwa
hadhi, kutoheshimiwa,kujisikia wao ni matapeli, kua hawana kauli thabiti ya
kuaminika,watajikia huzuni kwa kweli na wakati mwingine hasira na ghadhabu(Imagine
Mke hasiye mwamimi Mume au Wachumba wasio aminiana,Wazee wa Kanisa na Mchungaji
Kiongozi wanaotiliana mashaka,Kwaya Master na wenzake)
Kwanini
Asiye aminiwa ajisikie vibaya, hasira na ghadhabu?
Ni kwa kua anajua ana uwezo kufanya alichoahidi, pia ameahidi kwa upendo
wa dhati, anajisikia na anajua kua anahusikia kabisa na maisha ya mtendewaji, ni raha kwakwe kumuona
mtendewaji anajisikia kupendwa na kua na amani na kufurahia maisha sasa na uko
mbele. Pia atajisikia vibaya sana asipoaminiwa kwa kua ni nyakati nyingi yeye
huamua bila kuombwa kutenda mambo kadhaa na kua pale alipomwambia mtendewaji
kua atamfanyia jambo fulani, ilikua tu kutoa taarifa ya maamuzi ya furaha ya moyo
wake kumtendea jambo. Zaidi sana atajisikia hasira kweli kwa kua upo ushahidi
mzito uko nyuma kua alishatenda sana na zaidi ya kutenda yale aliyoahidi
mwenywe kwa nafsi yake na hata yale aliyoombwa kutenda na beneficiary. Kwa
mantiki izo, kutoaminiwa sharti liwe ni jambo baya sana, lenye maudhi kweli
kweli na kutia hasira isiyo na utani hata kidogo.
Ukiangalia andiko
hili Hesabu-14:1-39 hasa
mistari ya 11 na 22, utashangaa kufahamu jinsi Mungu, asipoaminiwa, uchukizwa
kuliko kawaida.. ’’Bwana akamwuliza Musa, Je! Watu hawa watanidharau hata lini? Wasiniamini
hata lini? Nijapokuwa nimefanya ishara hizo zote kati yao nakwa sababu watu
hawa wote, ambao wameuona utukufu wangu na ishara zangu, nilizozitenda huko
Misri, na huko jangwani, pamoja na haya wamenijaribu
mara hizi kumi, wala hawakuisikiza sauti yangu’’’. Unajua kwa sababu ya kutoamini kwao, Mungu alifanya
MAAMUZI MAGUMU…aliapa ingawa alishawaapia watairidhi Nchi, alifuta mpango huo
na akahakikisha wanakufa jangwani wote..mistari 22-23. Si ivyo tu, wale
wapepelezi 10 walioleta habari mbaya kinyume na kuongea maneno ya Kumwamini Mungu
kwa kua alishawaapia kua watairidhi Nchi kwa hakika hata kama kuna upinzani,
wakasababisha kundi kulalamika na kumtilia shaka Mungu, walipigwa wakafa mara
moja..mistari 36-37.
Katika Kutoka.32 na 33 pia Kumbu.9:11-20,
Uko mwanzoni walishamvuruga Mungu na ilikua awafute toka ktk uso wa dunia Wana
Israel,Taifa lake Teule kabisa na wala hakua anatania maana waga hatanii,wakapona-pona
kwa kua walikua na Mchungaji aina ya Musa ambaye hata kama kundi lilikua
linamvuruga sana yeye pia si Mungu tu bado kwa upendo wa kulea kondoo, no
matter what mpaka wafike mbinguni, ndio uliomsukuma kuwatetea kwa kujenga hoja
nzito sana mbele za Mungu( bila shaka wajua Mungu hupenda watu wamuendee kwa
hoja( Isaya.43:26..let us contend together, state your case…).
Pamoja na miujiza isiyo ya kupapasa na wala siyo ya kuona kiroho-roho bali live
Mungu aliyotenda katikati yao, pamoja na kua ni Mungu mwenyewe kwa mapenzi yake
kuamua kuleta ukombozi wao na kuwaahidia ahadi nyingi bila kusukumwa na kutiwa
msukosuko na mtu Kutoka.3:1-22, lakini kila walipopata changamoto kama
kukosa maji-Hesabu.20:1-5,nyama au walipofuatiliwa na majeshi ya Farao,
walinung’unika na kuongea mambo mabaya sana kinyume na Musa na Mungu, matamko
yaku-question or ku-query uwezo wa Mola.Walipoteza kabisa imani na Yehova
Mkombozi wao na kufikia hatua ya kutengeneza sanamu ya ndama na kuisujudia
kisha kuipa sifa na utukufu kua ndiye mungu aliye waookoa toka Misri!!!!! Mungu
akashindwa kuvumulia kudharauliwa, kutoaminiwa na kushushwa hadhi kiasi icho
akataka kuwafutilia mbali.
Pia Waebrania.11:6, Pasipo Imani
Haiwezekani kumpendeza Mungu! ingekua pasipo utakatifu haiwezekani kumpendeza
Mungu, hiyo ni mara moja rahisi kuelewa hata bila kujipatia muda wa kutakafari.
Hata ivyo wakati ktk kitabu icho icho 12:14 kuhusu utakatifu imeandikwa..
tafuteni….na huo Utakatifu ambao hakuna atakaye muona Bwana bila kua nao, kuhusu
Imani imeandikwa haitawezekana
kumpendeza.Ili Mungu apendezwe,ajue kua anaheshimika,ashawishike kua anafahamika
na uweza wake usiotia shaka na moyo wake wa kupenda kuwasaidia beneficiaries, ni lazima
aone kwa hakika na dhati kabisa kua anaaminiwa na anajulikana yupo.
Kuhusu Bwana Yesu
katika Mathayo.13:58, imeandikwa,
hakutenda miujiza mingi huku kwa kutomwamni kwao! Can you imagine that? Yesu
Mungu mwenye uweza wote na kwakwe hakuna lisilowezekana yet akaacha kutenda kwa
kua hawakumwami yaani nguvu na kuonekana kwa Mungu dhahiri ktk miasha yao kukaathiriwa
vibaya kwa kutoaamini kwao. Kwa maneno mengine, kama wangemwamini, leo tungekua
na orodha ya miujiza mingine aliyotenda but itoke wapi wakati hawakumwamini?
Kitabu cha Waebrania. 11:7-40 kuna shuhuda za
Wapendwa ambao walimwamini Mungu hata kama wengine hawakua watakatifu sana
lakini kwa imani yao kwa Mungu, wakahesabiwa haki(God did qualify( count) them righteous only after
they believed). Thus, kama kuamini au kua na imani kwa/na Mungu inamfanya Mungu
kum-transfer mtu toka stage ya chini kwenda ya juu/bora/ya baraka ie kuhesabiwa
haki basi kumwamini Mungu ni serious thing to miss.
Hatimaye ktk Yohana.14:1-3 Bwana Yesu ilibidi
asisitize kwa namna ya pekee Yeye pia kuaminiwa kwa mambo aliyowahi kusema na
aliyokua anawaambia wakati anatoa picha ya kuelekea kumaliza kazi aliyotumwa
kuifanya na nini destiny ya wanafunzi wake. Aliwachagiza kua kwa kua
wanamwamini Mungu basi na wamwamini na Yeye kwa habari ya mahali anapokwenda na
kua wasitie shaka kwa kua kwa Baba kuna makao mengi na anaenda kuwaandalia
makao,na kwamba kungekua hamna kitu, angekua sincere tu kuwaambia.
Kwakua mategemeo ya
Mungu kuaminiwa na madhara ya Yeye kutokuaminiwa na makubwa kiasi icho, basi
twapaswa kumwanimi Mungu ktk hali zote mfano: Wakati mambo hayaendi sawia,
mambo magumu safarini, ktk majaribu( tests/trials) za aina zote, mambo
yamekawia. Kwakua pasipo imani , haitawezekana kumpendeza na kutokumwamini ni
sawa sawa na kama alivyosema mwenyewe ktk Hesabu 14:11 kua ni kumdharau au
kumkataa, ni heri Tukamwamini, tukaendelea kumwamini na kama tulishuka imani
juu yake na mambo yake-(Ahadi ktk Neno lake au lile alilokuambia binafsi moyoni),
basin a tuinue/tufanye upya imani yetu kwakwe leo. Kama mwanadamu aweza jisikia
vibaya na kukasirika kweli hakidharauliwa, kwa Mungu inaweza kua serious case.
Press on believing in God, trusting in Him fully, no matter what!
Edwin Seleli