Leo kuna mpya nyingine ya kushea nanyi kwa lengo la kujengana na kufundishana na kuonyana, but kabla ya mada ya leo, hebu tukumbushane kidogo na kupeana mrejesho wa mada zilizopita. Tuliangalia majina ya watoto, tukaangalia kuwaombea watoto wetu kwa kuwataja majina na kutoa sadaka for
each one of them, tukaona tena kupima afya za wasaidizi wetu wa kazi kule nyumbani, tukaona pia faida za kukaa na Mungu, kwamba tunakuwa salama, na kama kuna kitu hatarishi adui amekiandaa kwa ajili yetu, Mungu hututonya/ kutustua mapema ili tuwe salama, na pia tuliangalia "kupekenyua watoto" ili kujua tabia zao na kuweza kuwasaidia, tuliona jinsi gani mama/baba wadogo shangazi na wajomba wanavyobaka watoto wetu
kule majumbani, na kwamba tumekuwa bize sna kutafuta rizki lakini hatuna muda wa kukaa nao. Wapendwa, watoto wetu wana vitu vingi sana vya kutueleza, but hatuna muda nao, kuna vitu vinawakwaza sna pale nyumbani wanashindwa kutuambia. Tuliona kwamba kwa wale wenye watoto wadogo, wawe wanawaogesha siku za weekend na "kuwakagua kama wako salama". Dear friends, nilirusha mada hii pia kwenye Face book, na nikapata ushuhuda "live" toka kwa victim mmoja wapo. Mkiingia kwenye wall yangu mtaona pale, mdada mzuri sna sna sana, amejieleza kwa uwazi kabisa kwamba yeye alikuwa akibakwa na binamu wa baba yake mzazi waliyekuwa wanaishi naye pale nyumbani, na house girl wao ndo alikuwa akimwogesha baada ya huyo anko kumfanyia vitendo hivyo, halafu anamwambia, "Usimwabie mama'. Ameeleza alikuwa na umri wa miaka 4/5 yupo kwenye list hii, she will testify for herself, (Please Ndeshy share your testimony for others to benefit).
Huyu
Binamu alikuwa akimfanyia hicho kitendo kila mara mtoto, analia kwa maumivu makali sna, imagine binamu wa baba yake mzazi! Mtoto hakuweza kuwaeleza wazazi wake, kwa vitisho vya housegirl!mhh! May God have mercy on our children.
Niliahidi kuwaeleza habari nyingine iliyotokea majuzi hapo Kisarawe, familia ina katoto kamoja ka kike, kako darasa la kwanza, baba yake kaleta wadogo zake wa kike na wa kiume, yaani shangazi na baba mdogo wa mtoto huyu, wakawa wanamfanyia vitendo hivyo hivyo! samahani naogopa kueleza kwa details maana ni mambo ya "aibu", lakini bila shaka mmeshanielewa, baba mdogo alikuwa akimnajisi na shangazi kadhalika, "anamtenda mambo yasiyofaa" (Napunguza ukali wa maneno), lakini wazazi hawakuweza kugundua wakiamini kwamba, tukiishi na ndugu zetu, basi watoto wanakuwa salama zaidi, kumbe si ndugu wote walio wema kwa watoto wetu. Yale yale ya kuwa bize na kukosa muda wa kutoka na
watoto wetu, ni waalimu wa mtoto yule ndo waliogundua tatizo hili, baada ya kuona mtoto hana furaha darasani na afya yake inanyong'onyea kila iitwapo leo. Dear parents, hebu tuwe na muda private wa kukaa na watoto wetu na kuwasikiliza, wanayo mengi mioyoni mwao ya kutueleza. Halafu, tusiwe wakali mno kwao, wanatuogopa jamani.
Sasa leo, nina ujumbe kwa wale "WAREMBO" wenzangu.
Wadada/wamama/mawifi/mashangazi mlioko humu, na nimewaandikia na nyie wababa ili mkawaeleze wake zenu huko majumbani, waendapo kusuka nywele saluni kule mwenge na kinondoni na kwingineko, hebu wae wanasali kwanza.
Hii imetokea hapa mjini, wale tunaoendaga MWENGE kusuka "yeboyebo" n.k, kuna majini pale yanasuka watu. Kumbe wale wadada waliojazana kule Mwenye wanaosuka, sio wote ni wanadamu, jamani mengine ni majini. Imemtokea mrembo mwenzetu hapa majuzi, kaenda kusuka kule, kakaribishwa kwa
bashasha zote kama mjuavyo,akasukwa vizuri sna, but baada ya kumaliza, akaanza kuumwa na kichwa, basi kile kichwa ndo kikawa kichwaaaaaaaaaaaaaaa mpaka akazimia, mhh! wakamkimbiza kanisa la jirani kwa ajili ya maombezi, hee, mapepo yasilipuke? yakasema huyu katufata mwenyewe kuja kusuka kwetu, je, alitegemea nini? Kwa kifupi wandugu, kumbe dada yule alisukwa na JINI.Sasa basi, kutaka kulithibitisha hili, juzi Jmosi nikaenda namie kusuka pale pale MWenge, nikaulizia kama hizi habari ni za kweli au la, nikaambiwa ni za KWELI, na msusi yule alikufa ghafla wakati yale majini yanakemewa kule kanisani!
Wakanieleza kabisapia vice versa too is reality, hata wao wamekuwa "wakisuka majini",na huyagundua kwa vituko fulani, na wakishawagundua, yale majini hutoweka ghafla. mhh! wandugu, this world we're living in, is not fair with us!
Ninachotaka kuwashauri warembo wenzangu hapa, hebu tumweke
Mungu mbele jamani, uendapo kusuka Mwenge pale, Kinondoni na kwingineko kote, hebu wale wasusi tuwaombee, rasta tunazotumia, nazo pia tuziombee! Kuna mazaga zaga tele huko masaluni. Asomaye na afahamu.
Salamu hizi ziwafikie warembo wenzangu,na wababa muwafikishie wake zenu/ mabinti zenu/dada zenu na mama zenu huko nyumbani.
Wandugu, tukubali tukatae, zipo faida sana kutembea na uwepo wa Mungu. No bad thing will ever happen to you kama ukimfanya Mungu kuwa Msaada wako. Imagine, hata Musa, Nabii yule mkuu, alipotumwa na Mungu kwenda kuwakomboa Israel kule utumwani, aligoma, akamwambia Mungu, " Kama uwepo wako usipokwenda pamoja nasi HATUTOKI hapa", aligundua kabisa kwamba, bila Mungu hawataweza. Na Mungu being a Loving and caring father, akamjibu Musa akamwambia, " Uso wangu utakwenda pamoja nawe, nami nitakupa RAHA". Wandugu,ipo raha kutembea na ulinzi wa Mungu. (Exodus
33:14-15)
Nawatakia siku njema, kesho tutaona Clinic nako huwa kuna nini.
I love you all My dear friends, You mean a lot to me.
Stella Egidio.