RE: SUMMARY

10 views
Skip to first unread message

stella egidio

unread,
May 28, 2013, 3:23:25 AM5/28/13
to SELELI EDWIN, Roselyne Massam, Sabina Nyoni, Ritha Semizigi, Rose Shirima, Rita Mandara, Sayuni Mariki, Shadrack Mrita, Tina Geleja, stella simkoko, Rose Mkumbo, Salome Magaya, Stella Jambo, shija msikula, Shija Msikula, stella...@yahoo.com, seme kennedy, Tausi Ingabire, samora macrice, smw...@gmail.com, Tecla Dominic, Shogo Mlozi, samb...@yahoo.co.uk, Rkyeli...@gmail.com, Rukia Adam, Straton Kimario, Sarah Seme, Sydney Mkamba, steve...@gmail.com, Rogers Fovo, Salum S. Yusufu, tple...@yahoo.com, suza...@yahoo.com, swafia....@tigo.co.tz, tengani...@yahoo.co.uk, sos...@hotmail.com, solidarity...@gmail.com, rwandi...@yahoo.com, stanle...@yahoo.com, shidu...@yahoo.com, sweetm...@hotmail.com, smbo...@yahoo.co.uk, suzana...@yahoo.com, smz...@yahoo.com, sse...@yahoo.com, rmnd...@nhctz.com, tito....@total.co.tz, rose seth, Sarah Mwingira, ritchm...@gmail.com, Vero James, veronica James, Zahara Amiri, Vivian Macha, Twitike Mwamundela, Tulibako Ulanga, Vicky Kamata, Tumsifu Elly, tutty mwankusye, Wende Caren Luvinga, yared dondo, vicky david, Tunu Mwiru, Tunu Mwiru, Wanagosheni, Upendo Mfalila, v_m...@yahoo.com, Zablon Mdeka, Tuwaha J. Mkunga, Veneranda N.. Lyimo, Victor Kimaro, Wolfgang E. Salia, Zawadi Nzota, vgamb...@yahoo.com, wvi...@yahoo.com, ve...@muvek.co.tz, vivia...@yahoo.com, viv...@yahoo.com, veronica...@yahoo.com, willso...@yahoo.com, tubas...@yahoo.com, zmas...@yahoo.co.uk, yoe...@yahoo.com, vk...@esrf.or.tz, waka...@state.gov, tunu...@yahoo.com, tuli...@yahoo.com, wema....@gmail.com, VS...@nhctz.com, veneran...@tra.go.tz, Veila Shoo
 My darling friends, how have you been? It's my belief that you have been well kept Under the shadow of the most High. Stay there Always!
 
Sasa leo, hakuna mada but tuna kumbushana tu vitu muhimu ambavyo tumeshawahi kuviangalia hapo awali.
Tuliwahi kuangalia jinsi tulivyo bize sana hapa mjini, kiasi cha kukosa muda wa kukaa na watoto wetu na kuwasikiliza wana malalamiko gani pale nyumbani, pengine kuna vitu ambavyo wanetu hawaridhiki navyo pale makwetu, but kwakuwa tuko 'bize' sna hatuna muda wa kuwasikiliza kwahiyo wanaendelea kuharibikiwa. Na nyie wenye watoto wadogo, je, huwa mnapata muda wa kuwaogesha watoto wenu weekend? Je, unapomwogesha mwanao, "unampekua pekua " private parts' zake uone kama hakutendewa hiana? Sio mtoto mchanga peke yake, lakini watoto wako wote walio under twelve years of AGE, hivi vitu vipo jamani. Hivi wandugu, mnajua kwenye  "school buses" watoto huwa wanafanyiwa  vitu viovu na wale wanaowaita "maanko" yaani utingo au konda wa zile bus jamani? Mnaonaga jinsi watoto wanavyojazana kwenye school buses, wale watoto wakubwa huwa wanawafanyia vitu vibaya sna watoto wadogo, nimeona mwenyewe kwa macho yangu nikiwa kwenye foleni naelekea kazini, eti mtoto wa kike amepakatwa na mtoto wa kiume kwenye school bus, jamani, wale wengine tayari ni adolescent, hivi binti apakatwe kuanzia Gongo la Mboto mpaka Kule kawe Esacs Academy au Mbagala Sant MAry's, huyu mtoto atafika salama kweli? Nataka ufikiri kwa kina hapo mzazi, sio usome tu kama simulizi, Je, wale shangazi/ma.mdogo/ ba. mdogo kule nyumbani tunajua how they treat our dear children? Mara nyingi tukikaa na ndugu nyumbani,huwa tunaamini pengine watoto wako more safer, kumbe si mara zote. Nawapa angalizo la kufuatilia hili, na kesho nitawaletea simulizi fulani iliyotokea hapa mjini, jinsi baba mdogo na shangazi walivyomtenda mtoto wa kaka yao, aliyewatoa kijijini na kuwaleta hapa mjini,kuja kuwasomesha, lakini hawakuuona huo wema wa kaka na kuamua "kumfisadi" mtoto wa kaka yao!
 
Tuliwahi pia kuangalia jinsi ambavyo tunatingwa na kazi kiasi cha kushindwa kupekua vyumba vyao vya kulala, tukaona house girl wa rafiki yangu aliyejifungua akakaa na mtoto siku 3 mle ndani bila wenye nyumba kujua. Kagua masanduku yao ya nguo, utaona vidonge vya uzazi wa mpango tele humo, mabegi yao ya madaftari utakutana na salama condoms, sio tu unasema, "mie mwanangu hana tabia  mbaya', au mwanangu bado "mdogo", kumbe alishatoa hata mimba tatu!  CHukua simu ya mkononi ya mtoto wako siku moja, angalia anawasiliana na nani, utajua ni marafiki wa aina gani alionao, mie kuna siku nilisema hebu leo nichomoe line ya simu ya binti yangu, niweke kwenye simu yangu nione, itakuwaje! Mhh! wandugu Usiku huo wala sikulala kwa hizo simu za usiku wa manane na sms za ajabu zilizokuwa zinatumwa usiku kucha, cha ajabu nilipofanya uchunguzi, nikagundua wale wote waliomtafuta usiku wa manane, wala hawakuwa wasichana wenzie bali wote ni wavulana, though she is not my biological daughter but since she is under my custodian, ilibidi nilivalie njuga suala hili na kumkanya kwa bidii sana, why boys and not girls? Mpendwa, watoto wetu wanalindwa na Mungu ni kweli, but we have a big role to play! Na kule twisheni je anakokwenda? huwa unafatilia kujua kama nikweli anaenda tuition au? Mie mwenzio kuna siku nilimfatilia huyu huyu binti yangu,mhh! Kumbe kaenda kupanda treni na wenzie wameenda mjini, hakuwa tuition wala nini, aliporudi namwuliza habari za twisheni, anajibu nzuri,mmesoma nini? tumefanya test ya Physics, mhh!  kumbe hakujua kama nilienda kumfuatilia, kumkomalia sna na kumwambia kwamba nimetoka shuleni nimemkuta fulani na fulani ndo akakiri hakwenda shule. "sijawahi kupanda treni, kwahiyo nilitamani kupanda treni mpaka posta mpya nione inakuaje". Hebu watume malaika wa Mungu wamsindikize mtoto wako akienda twisheni. Na wale walimu wanaowafundisha pia jamani duu! nao pia huwa ni balaa, MZAZI FUATILIA, sio unasema mie wanangu wote ni wa kiume, wangekuwa wa kike ningefatilia, ndugu siku hizi hao wa kiume ndo wamekuwa "asusa" kwa mabazazi!
 
Tulishaangalia kuhusu kuombea watoto wetu kwa kuwataja majina yao mbele za Mungu na kutoa sadaka kwa ajili yao, ili Mungu awakumbuke na kuwalinda kule mashuleni walipo, vyuoni, kwenye familia zao n.k. Tuliona mfano wa Ayubu, alivyokuwa akifanya, mpaka shetani akaona wivu kwa ajili yake akamwabia Mungu, " wee si umemzungushia wigo wa ulinzi? wandugu, upo ulinzi wa Mungu ambao wewe huuoni kwa macho lakini kumbe adui anauona! Ombea watoto wako, wataje majina yao mbele za Mungu, tubu dhambi kwa ajili yao, yamkini huko vyuoni wanakosoma watoto wako ni hatarishi lakini wakija nyumbani likizo they pretend to be angels. Nakushukuru wewe fulani huko India uliyeguswa na somo hili, ukaamua kubadilika. Niliporusha hii mada ya kuwaombea watoto wetu na kutubu dhambi kwa niaba yao, na kutoa sadaka wa ajili yao,kuna wazazi humu ndani walinipa shuhuda kwa yale yaliyotokea kwa watoto wao, na wapo pia wanafunzi wa vyuo, waliokiri kwamba somo lile liliwagusa sana na wakaamua kubadilika. Walikiri kabisa kwamba wakiwa huko USA, UK, India, UDOm, SAUT, UDSM, n.k wanafanya mambo mabaya sana, lakini wakirudi likizo wanakuwa "wema sana" pale nyumbani. Jamani, nina ushuhuda niliouona kwa macho kabisa, mwanafunzi wa chuo fulani hapa Mjini, amejifungua mtoto wa kiume, mpaka hivi leo mtoto ana miaka zaidi ya 8 wazazi wake hawajui. Alitafuta ndugu wa kijana aliyempa mimba, kwa hiyo akirudi kwao likizo mtoto anabaki kule, akifungua chuo, anachukua mtoto wake. Sasa nawewe mzazi unayenisoma hapa unajuaje kama huja-jukuu kule India, au SAUT au UDOM? hebu jifunze kuombea watoto wako, uwe karibu nao, usiwe mkali sna kwao, hata wakashindwa kukwambia mambo yanayowasibu.
 
Tuliangalia pia ishu ya majina tuliowapa watoto wetu na kwamba si vizuri kuwapa majina ya bibi na babu zao, kwalengo la kuwa-enzi wazazi wetu wakati unajua kabisa kwamba yule mama yako au baba yako au shangazi yako aliishi maisha gani, ujue kabisa kwamba majina yana impact kubwa sna kawenye mustakabali wa watoto wetu. Pia tuliangalia nyie wazazi, "mliofoji au kughushi" majina huko makazini, mashuleni, na mkaja kuoa, mkawaita wake zenu kwa majina ya kufoji, watoto wenu pia mkawaita kwa majina ya kufoji. Mfano wee jina lako halisi ni Frank Shayo, ukafoji na kujiita Peter Shirima, mkeo akaitwa Janeth Shirima, na watoto wako Manka Shirima, au Brian Shirima,  tuliona kwamba familia hiyo wala sio yako, bali ni ya huyo Peter shirima uliyechukua jina lake, no wonder  huyo Peter shirima alishakufa, kwa hiyo familia yako imeolewa na mzimu wa peter, kwa kweli tengeneza mambo yako bado mapema!
 
Nawatakia upekenyuzi mwema huko makwenu!






Reply all
Reply to author
Forward
0 new messages