Tuliangalia silaha kubwa tatu za kutusaidia kulea watoto wetu, tukaona ya kwanza ni Maombi ya mzazi, (sala), kwamba sala zako zinamgusa Mungu naye Mungu anawaponya watoto wako, tukaangalia silaha ya pili ni toba, yaani unatubu kwa ajili yao. Unajua kama tulivyoona hapo awali, watoto bwana, na siye pia wote tuliwa watoto, nasasa ni watu wazima, kwamba tunapokuwa na mzazi, basi weeeeeeee tuna adabu na nidhamu ya hali ya juu, lakini baba/mama/mlezi akitoka, tunaanza kugombana na kufanya mambo ya ajabu, kwahiyo hata sikumoja mzazi usiridhike na tabia za mtoto wako, kwamba she /he is an angel, je, akiwa kule shuleni, au chuoni anaishije? kwa hiyo huyu bwana Ayubu alitubu akisema,." yamkini wamemkosea Mungu mioyoni mwao, yaani kwa lugha ingine, hata kama mie sijaona uovu wa watoto wangu kwa macho,basi pengine hata ndani ya nafsi zao wamekengeuka, na mwisho tuliona ni SADAKA. Sadaka wapendwa, ni kitu cha tofauti, hasa
unapoitoa kwa kunuiza kitu fulani mbele za Mungu, tuliona Ayubu alivyotoa sadaka kwa ajili ya watoto wake, wote kwa idadi yao na kwa majina yao!
Sasa leo, nataka tumalizie kipengele cha pili cha hili somo letu, kwanini SADAKA? Au tuseme sadaka ina umuhimu gani mbele za Mungu? Just to mention the list, na mwingine atajazia.
(1) sadakani mumhimu sana mbele za mungu, kwa kuwa imeandikwa, Hazina yako ilipo, ndipo na moyo wako ulipo. Kwahivyo basi, wewe mzazi bila shaka umewabeba watoto wako moyoni mwako, kwa hiyo, ile sadaka yako inakuwa ni hazina iliyotoka kwenye moyo wako, walipo pale walipo watoto wako, Mungu anapoiangalia, ataangalia na hao watoto wako pia!
(2) Pia sadaka inaleta Kibali, yaani inatupa kukubaliwa na Mungu. Hapa tunamwangalia Abeli, mtoto wa kwanza wa Adamu na Hawa. neno la Mungu linatuambia kwamba, Abeli alipata kibali (upendeleo) mbele za Mungu, kwa sababu ya sadaka alizotoa! Hivyo basi unapompelekea Mungu sadaka yako, kwa ajili ya hao watoto wako, Mungu atawapa kibali, yaani watatembea katika Upendeleo wa Mungu. Utashangaa shule anayosoma mwanao, bweni limeungua, lakini mwanao hakuungua wala kuathirika, kumbe ni zile sadaka zako zilikumbukwa na Mungu, akasababisha ulinzi juu yake.
(3)Tatu, Umuhimu wa sadaka tunauona wakati wa gharika ya Nuhu, huyu bwana Nuhu baada ya gharika, maandiko yanasema, alimtolea Mungu sadaka nzuri ikamridhisha Mungu, naye Mungu akaapa, akasema tangu leo, sitaigharikisha tena dunia kwa gharika! akaweka upinde wa Mvua. Ndugu zanguni, ule upinde (rainbow) tunayoina sio sayansi wala Jiografia, ni Agano ambalo Mungu alilifanya, kwamba HATAGHARIKISHA tena dunia kwa maji, simply because, NUHU ALITOA SADAKA.
(4)Pia umuhimu wa sadaka tunauona tena kwa Cornelio. Tunaambiwa kwamba huyu bwana alikuwa akimcha Mungu, na kutoa sadaka nyingi. Siku ya shida yake,Mungu alituma malaika, "akamwambia cornelio, sala zako zimefika mbele za Mungu, na sadaka zako zimekuwa "ukumbusho". Mpendwa wangu unayenisoma, SADAKA ZAKO ZINAKUMBUKWA MBELE ZA MUNGU!
(5)Mwisho kabisa, tunaangalia umuhimu mwingine wa dadaka, kwa huyu mama anayeitwa Dorkasi. Maandiko yanasema kwamba, huyu bibi aliugua, akazidiwa mpaka akafa, lakini wakati wa uhai wake, alikuwa akitoa sadaka na kuwapa wajane, na aliwashonea hata masweta pia. sasa alipofariki, hawa wajane walikusanyika wakilia, wakamfuata mtume Petro,wakamuonyesha zile nguo walizopewa na huyu mama, wakalia sna, Petro akamwombea Dorkasi, akafufuka. Nini kilimfanya Mungu amfufue Dorkasi? Ni zile sadaka alizotoa kwa wajane, aliwashonea nguo na masweta , ile ilikuwa ni sadaka yake iliyokumbukwa mbele za Mungu,
Naomba leo niishie hapa, nikijua kabisa kwamba wazazi na walezi wenzangu tutajua umuhimu wa kuwaombea watoto wetu, tutatubu kwa ajili yao na kumtolea Mungu sadaka, kwa ajili yao, ili Mungu awalinde, awatunze na kuwapigania.
Wasalaam,
Stella Egidio.