Fw: USHUHUDA MPYA WA GEREZA WATOTO!

6 views
Skip to first unread message

stella egidio

unread,
Nov 22, 2012, 1:22:20 AM11/22/12
to Eliasifu Mlay, SELELI EDWIN, Roselyne Massam, Sabina Nyoni, Henrick Sanga, Ritha Semizigi, Rose Shirima, Vero James, veronica James, Alice Gomba, Zahara Amiri, Rita Mandara, Twitike Mwamundela, Sayuni Mariki, Ndemanisho Edith, Noela Lugera, Paula Mugeye, Tulibako Ulanga, Vicky Kamata, Ntuli, stella simkoko, Harold Sungusia, Rose Mkumbo, Tumsifu Elly, scholastica mhando, tutty mwankusye, Wende Caren Luvinga, Salome Magaya, Pablo Kaisi, Nakimo Mwakatundu, Stella Jambo, Rehema, shija msikula, Shija Msikula, Stella Mngodo, seme kennedy, vicky david, Tausi Ingabire, samora macrice, Nancy Mukoyogo, Samwel Mwiru, Tunu Mwiru, Tunu Mwiru, Shogo Mlozi, Paulo1, ruth kyeli, Justin Kaleb, Dr. Turuka, Wanagosheni, Oliver Njunwa, Prosper Goima, Pamella Salehe, Patrick Kisaka, Patrick Mugoya, Rukia Adam, Rehema K. Shao, Straton Kimario, Sarah Seme, Sydney Mkamba, steve...@gmail.com, Upendo Mfalila, v_m...@yahoo.com, Zablon Mdeka, Neema Mrema, Nicholas Nyonyo, Patience Minga, Rogers Fovo, Salum S. Yusufu, Tuwaha J. Mkunga, Veneranda N.. Lyimo, Victor Kimaro, Wolfgang E. Salia, Zawadi Nzota, Paul Shalua, Richard Kerissa, Atupele Edward, Veronika Gambares, Tra Noelia, Sis Vinna, suzan otieno, swafia....@tigo.co.tz, peter mitimingi, tengani...@yahoo.co.uk, Joyce Nampesya David, rose seth, Sarah Mwingira, Richard Mbuthia, Veila Shoo
Dear friends of Mine in this family!
 
Nawashukuru sna nyie wote mliokwenda pamoja nami kule gereza la watoto kuwaombea au kusema nao neno la Mungu na kuwaombea pia.
 
Jana jioni wakati najiandaa kutoka ofisini, nipigiwa simu kwamba nishuke chini kuna watoto wamekuja kunitafuta, nikaenda kuwaona, aisee, kumbe ni wale watoto wa kule gereza la watoto!
 
Wakanipa ushuhuda huu kwamba, "siku ile ya idd ulipokuja kutuombea na kutuletea zawadi, kesho yake tuliitwa mahakamani, tukaambiwa kwamba kesi zetu zimeisha, yaani tumefutiwa mashitaka. Glory be to God in the Highest! wamenieleza kwamba wametoka karibu watoto kumi, kwa hiyo wamebakia watoto saba. Nawashukuru kwa maombi yenu kwa ajili ya wale watoto, Mungu amewarehemu, na kesi zao zimefutwa!
 
 Katika hao saba waliobaki, ni pamoja na kale kabinti ketu, ka Hawa. Nategemea kesho kupita tena pale niweze kuzungumza na mkuu wa gereza ili nijue kama zimepatikana contacts za yule mama mlalamikaji, ili tuweze kuzungumza naye kwamba, tupo tayari kumlipa pesa yake ili yule mtoto atokea gerezani. Asanteni kwa huduma yenu, kwa maombi yenu na kwa michango yenu pia.
 
Ushuhuda mwingine wa watoto, ni hawa wanaoosha vioo vya magari yetu kule njiani, nakumbuka niliwakusanya kwenye kile kijiwe chao cha pale kwa Bakhresa kwenye ule mti pale, walikuwa kama watoto 24, nikazungumza nao kwanini wako pale, na madhara ya kutoroka nyumbani na kwamba hizo peza wanazopata shilingi mbili tatu za kuosha magari, wanaweza wakaanza kufanya kitu fulani cha faida zaidi, nikawapa wazo la kuanza kuuza chewing gum, jamani naomba kuwashuhudia kwamba watoto wale sasa hivi niwafanya biashara za pipi na biscuit kwenye foleni, kila nikipita asubuhi, nawaona wanatuuzia, na sio tena kuwa omba omba wala kuosha magari, na mwingie huyu ndo kaniacha hoi kabisa, hapa karibu na ofisini kwetu kuna kanafasi fulani, kaamua kulima bustani ya mboga, anavuna na kila jioni anazipanga pale tazara, juzi nimekula mboga zake, kwa kweli wazazi, nimekubali kwamba Tanzania bila watoto wa Mitaani, INAWEZEKANA. Kama kila mmoja wetu akiamua kuongea na mtoto mmoja tu huku njiani na kumsaidia, kweli we can make a difference in this generation!
 
Mungu awabariki sana wazazi wenzangu, tusichoke kusaidia watoto wa mitaani na wenye shida, kwa kufanya hivyo tunapanda mbegu mbele za Mungu kwa ajili ya watoto wetu, ili walindwe na Mungu.
 
Stella Egidio.




Reply all
Reply to author
Forward
0 new messages