RE: JE! OMBA OMBA NAO? (BEGGERS)

14 views
Skip to first unread message

stella egidio

unread,
Jun 7, 2013, 6:18:36 AM6/7/13
to Vero James, veronica James, Zahara Amiri, Vivian Macha, Twitike Mwamundela, Tina Geleja, Tulibako Ulanga, Vicky Kamata, Tumsifu Elly, tutty mwankusye, Wende Caren Luvinga, yared dondo, vicky david, Tausi Ingabire, Tunu Mwiru, Tunu Mwiru, Tecla Dominic, Wanagosheni, Sydney Mkamba, Upendo Mfalila, v_m...@yahoo.com, Zablon Mdeka, Tuwaha J. Mkunga, Veneranda N.. Lyimo, Victor Kimaro, Wolfgang E. Salia, Zawadi Nzota, tple...@yahoo.com, vgamb...@yahoo.com, wvi...@yahoo.com, suza...@yahoo.com, swafia....@tigo.co.tz, tengani...@yahoo.co.uk, ve...@muvek.co.tz, vivia...@yahoo.com, viv...@yahoo.com, veronica...@yahoo.com, willso...@yahoo.com, tubas...@yahoo.com, sweetm...@hotmail.com, zmas...@yahoo.co.uk, yoe...@yahoo.com, vk...@esrf.or.tz, waka...@state.gov, tunu...@yahoo.com, tuli...@yahoo.com, wema....@gmail.com, VS...@nhctz.com, tito....@total.co.tz, veneran...@tra.go.tz, tumain...@mkono.com, Veila Shoo
Dear Precious people of God, jana niliahidi kwamba tungezungumzia suala la hawa Omba omba mitaani, yaani (beggers), ili tujue wametoka wapi, na wana misheni gani labda katika hii Jamii yetu.
Tuliangalia kuhusu masaluni na kwa wasusi jinsi ambavyo nguvu za giza zimetawala mpaka kuna wasusi majini na wateja wengine ni majini wanasukwa pale MWenge.
 
Tukumbuke ya kwamba, hawa beggers, hawakuanza leo ndugu zangu, wala hawapo hapa Tanzania tu, hata mataifa tajiri duniani, kama US, Uk, na kwingine pia wapo.Kumbe nikaja kugundua ni Mungu alimwambia nabii Musa maneno haya kwenye kitabu cha Leviticus,, " Muda nchi idumupo, maskini hawatakoma kati kati yenu). Kwanini alisema hivi, ni ili kutuwajibisha sisi kwa sisi kuhurumiana na kusaidiana, kwa mfano tukisoma hapa kwenye Walawi 23:22, imeandika hivi, "Nanyi mtakapovuna mavuno yenu, usivune kabisa kabisa pembe za shamba lako, wala msiyakusanye masazo ya mavuno yako,  utayaacha kwa ajili ya huyo masikini na mgeni, Mimi ndimi Bwana".
 
Kwa hiyo wandugu hawa masikini, wana sehemu katika mavuno ya mashambani mwetu, lakini mmegundua hawa omba omba  wetu ukiwapa vyakula hawapokei, wanataka hela tu? au nyie hamjakutana nao? Naomba leo niwape angalizo kwamba, sio wote unawaona mjini kule ni Ombaomba wa ukweli, wengine sio wanadamau. Jamani, shetani amepanga mikakati ya kuharibu uchumi wako, utajiri wako, na kuku-initiate weee na fedha zako zipotelee kuzimu, yaani unapompa ile pesa yako, yeye anakwenda kuiwakilisha kuzimu, utashangaa tu mambo yako hayaendi, madili yako tena hayafanikiwi, unapata pesa nyingi huoni ulichokifanya, kumbe ndugu yangu ulimpa omba omba kule posta au kariakoo, ukadhani ni genuine omba omba kumbe sivyo. Mengine ni mapepo yanavaa miili ya wandamu, ili kukaa pembe za njia na kuiba pesa za watu. Wandugu, nimeona LIVE  kwa macho  yangu haya mawili, mtu akiombewa na kufungulia na kuanza kuelezea jinsi kule kuzimu alivyokuwa anatumwa mjini kujifanya omba mwenye donda ndugu kubwa sna au mlemavu, wengine wanatumwa hospitalini kujifanya wagonjwa wanalazwa kabisa kumbe wako kwenye special mission ya ibilisi kuua wagonjwa wa Hospitali ile, tena huyu ni mwanamke niliona akishuhudia kwamba yeye alikuwa akilazwa tu, wodi ile wagonjwa watakufa woooooooooooote, anapona yeye na kupewa discharge, akirudi huko chini, anapewa cheo kikubwa kwa kadiri ya idadi ya watu aliowaua pale hospitalini.
 
Wandugu wa Dar, mtakumbuka ile story ya yule mwanamke mwenye RAV alitoweka pale daraja la salenda, mnakumbuka wandugu wa dar? basi ile story haikuwa na kutunga ni ya kweli tupu, mama yupo kenye foleni, akatokea omba omba, akamuhurumia akampa hela ghafla yule amba omba mkono wake ukageuka kama wa paka mwenye manyoya na yule mwanamke akatoweka, iliripotiwa sna kwenye vyombo vya habari, nadhani mnakumbuka, basi ile wapendwa ni story ya ukweli.
 
sasa huu ni mfano wa pili wa rafiki yangu ambaye yupo kwenye hii hii mail list yangu. Sitamtaja bila ridhaa yake, unless yeye aamue kutuandikia. wandugu, tuko hapa kujengana na kushauriana, ili tupone. Hata sadaka yako usiitoe popote bila kuiombea, nasisitiza ukichukua pesa zako benki ziombee pale pale, hata kama unaenda kutoa kanisani au msikitini au kumpa mtu yoyote au kununua kitu, mpendwa, OMBEA PESA YAKO. Yesu alisema hazina yako ilipo , ndipo na moyo wako utakapokuwepo, sasa wewe utatoaje hazina yako  mahali usipopajua au usipokuwa na uhakika napo? usitoe sadaka bila kuiombea aidha ni kwenye nyumba ya Ibada au unampa mtu, hata kama ni mchango wa harusi au rambi rambi,iombee pesa yako tangu leo! uchumi wako unatafutwa sna na ibilisi, anaitumia hiyo pesa uliyonayo kuzivuta nyingine.
sasa, huyu dada yangu, alikuwa kwenye foleni, anato kwake Mbezi beach, anakwenda mahali fulani Privacy kujifungia ili kumwomba Mungu, aliona hakuna utulivu wa kutosha pale nyumbani, anasema ilikuwa ni siku ya jumamosi pale kwenye mataa ya Morocco, alikuwa amefunga siku hiyo, ana maombi yake ya KUHITAJI MTOTO.Yaani amefunga na kuomab ili Mungu amkumbuke ampe mtoto, sasa kufika pale kwenye foleni, akaja omba omba dirishani, akaomba hela kwa fujo, yani aligonga kioo kwa nguvu sna, huyu rafiki yangu, akashangaa huyu omba omba gani mwenye fujo hivi? akaamua kupandisha vioo mpaka juu. Guess what? Yule begger akaanza kutukana matusi,akamwabia wee mwanamke una roho mbaya sna, ndio maana HUZAI! wandugu sio story ya kitabu muhusika yupo hapa! Good enough huyu dada amejaa Mungu, kwahiyo hakuogopa, but alishangaa sna huyu omba omba kajuaje kama mimi sina mtoto? halafu mind you , alikuwa kwenye maombi y akufunga ANAENDA KUJIFUNGIA MAHALI ILI KUMUOMBA MUNGU AMPE MTOTO. Unapata picha hapo mpendwa? Anasmea, yaani alilia kwa uchungu sna mpaka anafika kule kwenye maombi, analia badala ya kuomba, adui alitaka kumkatisha tamaa ili asikutane na Mungu.
Kufupisha story, huyu dada akajua kabisa kwamba, huyu hakuwa omba omba wa "kawaida, bali alikuwa ni pepo  ndani ya mwili wa Mwanadamu.
 
Dear friends of mine, najua leo ni week end, ngoja nifupishe hii mada, ninachotaka ukijue my darling friend, ni kwamba ulimwengu huu tunaoishi, sio mwema hata kidogo,umejaa uovu na mambo mengi ya nguvu za kishetani.
 
Najua tuko watu wa Imani tofauti tofauti humu ndani, bali TUNAYE MWOKOZI MMMOJA TU, YESU KRISTO.Sasa huyu mwokozi, kabla hajaondoka na kurudi kwa Baba yake ambaye pia ni Baba yetu, aliujua huu ulimwengu anaotuacha ukoje, ndio maana akasema, naenda kuwaandalia makao, halafu nitakuja tena NIWACHUKUE, ili nilipo mimi na ninyi pia muwepo.Kwa hiyo, akaacha ametuombea Divine Protection, yaani ulinzi wa Kimungu, ukisoma Yohana 17:9-15,utaona pale maombi yake, anasema, "Mimi  nawaombea hao, siuombei ULIMWENGU, bali hao ulionipa kwakuwa ni wako, akasema, wala siombi kwamba uwatoe katika ulimwengu, BALI UWALINDE NA YULE MWOVU".
 
Mpo hapo wandugu? Alituombea kwamba Mungu atulinde na yule Mwovu.
Nawatakia mapumziko mema marafiki zangu wazuri, hebu tukae katika ulinzi huu ambao Mungu ametuahidi, na tusichoropoke ili tusiangamie.
 
Sasa wiki ijayo, tutawaangalia wale maharusi, wanaokwenda kupiga picha baharini, yaani mtu unafunga ndoa yako takatifu pale kanisani, halafu unatoka hapo, UNAENDA BAHARINI NA MKEO na familia yako kupiga picha, hivi kweli, hakuna maeneo mengine mazuri tu ya kuvuti ya kupigia picha zako za harusi mpaka uende baharini? ee? kwa nyie mliokwisha funga ndoa, basi Mungu awarehemu but kwa sisi maharusi tarajiwa, tukutane darasa lijalo.
 
God Bless you presious people.
Stella Egidio.
 




Reply all
Reply to author
Forward
0 new messages