RE: IT IS DONE! MAHABUSU YA WATOTO.

7 views
Skip to first unread message

stella egidio

unread,
Dec 11, 2012, 1:29:58 AM12/11/12
to Grace Owden, Shadrack Mrita, Helena Mcharo, Ibra Kipanje, isabe...@gmail.com, Hawa Tundui, katuye Ndabagoye, juda semali, grace sabuka, Grace Makani, Grace Temu, Ichikaeli Maro, Grace Busara, Agnes RWEGASHA, Jiang Alipo, Joyce Gervas, jenipher lema, Ephraim Luvinga, Justin Kaleb, jsmu...@yahoo.com, Isadini Mushi, jpc...@yahoo.com, Jane Kimweri, Joseph C. Mnzava, Gloria Mwasamwaja, Gabriel Mwangosi, helly.do...@rocketmail.com, Highness Chacky, Hakim Kimungu, Honester Ndunguru, Julius Ceasar, Joyce Lukwaro, John Mziray, Joseph Mtandika, Julius J.B. Ng'webeya, harieth mtae, iza...@yahoo.com, Hawa Tundui, janet...@hotmail.com, Tina geleja, Jane Makoye, Holipa...@nbctz.com, Goshen Family, Hobo Kela, Doreen Ruta, Joaven Wifi, irene mwakatundu, joycekalamule, John mcharo, Eliasifu Mlay, SELELI EDWIN, Vero James, veronica James, Zahara Amiri, Twitike Mwamundela, Sayuni Mariki, Tulibako Ulanga, Vicky Kamata, Ntuli, stella simkoko, Harold Sungusia, Tumsifu Elly, scholastica mhando, tutty mwankusye, Wende Caren Luvinga, Stella Jambo, shija msikula, Shija Msikula, Stella Mngodo, seme kennedy, vicky david, Tausi Ingabire, samora macrice, smw...@gmail.com, Tunu Mwiru, Tunu Mwiru, Shogo Mlozi, Dr. Turuka, Wanagosheni, Straton Kimario, Sarah Seme, Sydney Mkamba, steve...@gmail.com, Upendo Mfalila, v_m...@yahoo.com, Zablon Mdeka, Salum S. Yusufu, Tuwaha J. Mkunga, Veneranda N.. Lyimo, Victor Kimaro, Wolfgang E. Salia, Zawadi Nzota, Atupele Edward, vgamb...@yahoo.com, wvi...@yahoo.com, suzan otieno, swafia....@tigo.co.tz, tengani...@yahoo.co.uk, Veila Shoo
Dear friends of mine, Ukweli ni huruma za Bwana kwamba hatuangamii, kwa kuwa rehema zake hazikomi" Hivi kama Mungu angehesabu maovu yetu, ni nani angesimama mbele zake wandugu?
 
Napenda kuchukua nafasi hii kuwapa ushuhuda  kwamba, BINTI YETU HAWA,YUKO HURU SASA! yaani kesi yake imefutwa. Napenda kuwashukuru sana wandugu wote mliochanga kumlipia deni lake, kama ambavyo na sisi pia YESU ametulipia deni la dhambi zetu, katika mti wa Msalaba! I'm overwhelmed by joy kwa ajili ya kale kabinti ketu. Asanteni sana kwa michango yenu, siwezi kuwataja mmoja mmoja lakini Mungu anawajua wote kwa majina yenu!
 
Sasa basi, baada ya binti yule kufunguliwa, zinahitaji kiasi cha shilingi laki 3 tu, kumsafirisha yeye na afisa wa Ustawi wa Jamii ili kumrudisha kijinini kwao, of course namimi nitakwenda nao, lakini naweza kujilipia gharama za usafiri. Imeamriwa na MAHAKAMA ya , kwamba arudishwe kijini kwao, awe chini ya uangalizi wa Maafisa ustawi wa jamii kule kwao, kwa kipindi cha miezi 6,then kama kuna wasamaria tunapenda kumchukua na kumsaidia kimasomo au  kwa lolote basi tumfate akiwa chini ya himaya ya wazazi wake!
 
Utaratibu wa serikali ni kuwasafirisha wafungwa wote wadogo kwa wakubwa na kuwarudisha makwao, pindi wanapoachiliwa, lakini nilipoongea na mkuu wa gereza, akasema utaratibu huu huwa unachukua muda mrefu sana, kwa watu wazima au wenye ndugu huwa wanawapigia na kuwatumia nauli au kuja kuwachukua toka gerezani, lakini kwakuwa huyu ni mtoto mdogo na hana ndugu yeyote hapa mjini, kwa hiyo anahitaji kusindikizwa kwao. Sasa baada ya kuambiwa kwamba zoezi hili la kuwasafirisha huwa linachukua muda mrefu, na kwa muda huo wa kusubiri nauli ya serikali, bado mtoto atakuwa pale pale jela, kiasi ambacho muda aliokaa mle ndani na muda wa kusubiri nauli anaweza akakaa zaidi, kwa hiyo asubuhi hii, kanipigia simu mkuu wa gereza anaomba wahisani tuchangie hiyo pesa ili mtoto yule arudi kwao, kuliko kusubiri serikali.
 
Kwakweli kwa mazingira aliyonieleza Hawa mwenyewe juzi jumapili nilipopita pale, nimagumusna kwake, wakati naondoka mtoto yule alikuwa ananililia niondoke naye lakini sikuweza! wandugu hebu tuchangeni hizi pesa mtoto atoke mle ndani, maana mkuu wa gereza mwenyewe anamtaka kimapenzi, mlinzi wa gereza naye anamtaka kimapenzi, sasa itakuwaje jamani wandugu? Nasikitika kuwafahamisha kwamba, akiwa pale jela, alitoa mimba ya miezi minne, sasa sina uhakika kama aliitoa kwa makusudi au ilitoka yenyewe, japo nilipomhoji juzi, aliniambia kwamba "Ilitoka yenyewe", na wala hakuwa anajua kama ni mja mzito kwa sababu ya umri wake kuwa mdogo! Anasema alikuwa anacheza mpira na watoto wenzage kule jela, mwenzie akampiga na mpira tumboni, baadaye damu nyingi zikamtoka, baadaye akaenda WC anasema kikamtoka kitu fulani kikubwa kubwa, akapiga kelele, wakaja watu wazima, wakamwita daktari, kuja pale akapewa dawa, then  kikatoka kitu kama utumbo mkubwa, basi, ndo akaambiwa kwamba "ulikuwa na mimba na imetoka". Ndugu wazazi, hebu tufanye kitu kwa ajili ya huyu mtoto tuweze kumtoa kwenye yale mazingira hatarishi. Nimechukua likizo kwa lengo la kumrudisha kwao mtoto huyu, Naomba mwenye nauli au mchango wowote ili kufanikisha safari hii, awasilishe mchango wake kwangu kwa njia ya tigo pesa au Mpesa, namba zangu ni zile zile, na zote nimezisajili.
 
God Loves a cheerful giver!
 
Tigopesa 0715 972 862
Mpesa 0754 972 862
 
Stella Egidio


Reply all
Reply to author
Forward
0 new messages