Heri ya mwaka mpya kwa wale ambao bado hatujaonana wala kutumiana salamu! Basi mie ndugu yenu nilikuwa likizo, katika likizo hiyo kuna mambo nilijifunza, ambayo ningependa kuwashirikisha nikiamini kabisa kwamba, kama jinsi mimi yalivyonijenga,basi nanyie pia mnaweza kusaidika in one way or the other.
Kwa kuanzia, tuanzie na hilo somo tajwa hapo juu,
kuhusu kulea watoto. kusema ukweli malezi ya watoto ni changamoto kubwa sana kwa familia nyingi sna si za Kiafrika tu, lakini ni global! Na wala kulea watoto hakuna ufundi wala ustadi wala uzoefu! Mara nyingi Watoto wakiwa nyumbani wakati wa likizo they use to behave very good, lakini wakiwa shuleni ukiambia vituko vyao unawza kuzimia, na haya mambo ya facebook na internet, pia yamechangia kwa kiasi kikubwa sna kuharibu
maadili ya watoto wetu. Bila kuzisahau cartoon pia. Kuna wale wazazi ambao huwaona watoto wao kama vile ni malaika, lakini sivyo walivyo katika uhalisia, nina jirani yangu aliitwa shuleni kwa mtoto wake huko moshi, kufika kule akakabidhiwa mtoto wake, kwamba hatumtaki tena kwa sababu ya tabia zake, kuuliza walimu mwanangu mbona mwema tu,ana tabia gani? akaambiwa kwamba binti yako ni " msagaji" mama yule alizimia wandugu, ni binti wa 14 only, yupo kidato cha pili, mamayule hakuamini. Si hayo tu kuna na mengine mengi huku kwenye mtandao yanafanyika,bila sisi wazazi kufahamu. Kwa kweli kulea watoto ni challenge kubwa sna.
But katika hayo yote ipo ahadi ya Mungu kuhusu hao watoto wetu, Kwanza lazima mzazi utambue kwamba, we are parents, are just custodians, but children belongs to God, we have been entrusted by the Creator kuwalea hao watoto, ndio maana Mungu alitupa! ukisoma Isaya 54:13,
nenola Mungu linasema, " Na watoto wako wote watafundishwa na Bwana na amani ya watoto wako itakuwa nyingi". Hebu kama mzazi, uwe na tabia ya kuwaombea watoto na kuwakabidhi kwa Mungu awezaye kuwalea katika njia zake za haki na katika uadilifu Mkubwa! Shikilia ahadi za Mungu kama hiyo hapo juu kila unapowaombea watoto wako!
Tujifunze pia kwa ndugu yetu Ayubu. Kwa wale wasomaji wa Biblia, wanajua habari za huyu bwana Ayubu, imeandikwa kwamba, huyu Ayubu alikuwa ni mwenye kumcha Mungu sna, na alikuwa ni mwadilifu na muelekevu, akimcha Mungu na kuepuka uovu, but kuna kitu cha ziada ambacho huyu bwana alikifanya, kilichonigusa moyo wangu sana. Biblia inasema hivi, " Huyu Ayubu alikuwa akitubu kwa ajili ya watoto wake akisema, yamkini wamemkufukuru Mungu mioyoni mwao, na alikuwa akitoa sadaka kwa ajili yao sawa sawa na idadi ya watoto wake". Kuna siri wapendwa katika kutubu
dhambi kwa niaba ya watoto wako na kutoa SADAKA KWA AJILI YAO PIA. Tunaambiwa kwamba Mungu alimzingira Ayubu na watoto wake kwa wigo wa ulinzi na shetani hakuwaweza kuwagusa, mpaka alipoaruhusiwa na Mungu (wakati wa lile jaribu lake).
Ninachotaka kusema hapa ni nini basi wazazi wenzangu? Ni kwamba, hatuwezi kulea watoto wetu sisi wenyewe bila msaada wa Mungu, mambo wanayofanya kwa siri huko vyuoni, mashuleni moshi,arusha iringa n.k sisi huwa hatupo pamoja nao, lakini Our God is Omnipotent Father of Mercy and Grace, kwa wewe kuwaombea na kutoa sadaka kwa ajili yao, una draw attention ya Mungu juu ya mwanao, sijui nimeeleweka hapo wandugu?
Kwa mfano una mwanao anaitwa Mercy kule Kibosho Girls, wee mzazi hujui huyo Mercy ana mwenendo gani huko shuleni au ana mashambulizi gani katika masomo yake au ana marafiki wa aina gani, but kwa ile SADAKA yako uliyoipeleka mbele
za Mungu kwa ajili ya Mercy, Mungu atamwangalia kwa jicho la rehema na kumnusuru na majanga mbali mbali. Ndugu zanguni, watoto wana mashambulizi mengi sna, hatujui tu. KUna mtoto juzi nimeambiwa na mamayake, kwamba he was very inteligent lakini siku ya mtihani wa darasa la saba ulipofika, alikuwa anatoka machozi tu na anaiona karatasi yamtihani ni nyeupe tu haina maandishi yoyote,hivimnapta picha? kwa hiyo hakuweza kufanya mtihani wake, wakaishia kushikana uchawi na shangazi yake! Unaweza ukasema mwanangu mie bado mdogo hata vidudu hajafika, je, unajua usalama wake na yule house girl anayemlea pale nyumbani? Unajua analishwa nini, au binti anamtunzaje? maana mwanao abdo mdogo, na hawezi kujieleza. Kuna shangazi wa rafiki yangu alikuwa na house girl ambaye ni mchawi, basi kila siku usiku akienda kuwanga anapanda ungo na mtoto wa huyo shangazi kwenda kuwanga naye, matokeo yake mtoto akawa na vipele vyambu na malaria hazimuishi
kumbe alikuwa analiwa na mbu huko nje, tusiamini kabisa wadada wa kazi, hebu tujifunze kumwamini Mungu kwa ajili ya watoto wetu, na kwa kuwaombea pia hao wadad awawe na upendo juu ya watoto wetu wanaotulelea. unaweza ukasema , wanangu mie wote watu wazima, wanajitegemea, je, unajua huko anakoenda kuuolewa binti yako ataishije au kijana wako atapata mke wa aina gani? Ndugu wazazi, hebu tuliangalie hili suala kwa upana sana, TUNAMUHITAJI MUNGU SANA KWA AJILI YA WATOTO WETU! Tujifunze kutoka kwa huyu bwana Ayubu, " alitubu na kutoa sadaka kwa ajili ya watoto wake kwa kadiri ya idadi yao". kwa mfano wee una watoto watatu, Fatma, Lissa na Samweli, basi unatubu kwa ajili yao kwamba Mungu ninatubu kwa ajali ya Lissa, maana sijui kule chuoni Mzumbe anaishije na sadaka hii Mungu nakupa kwa ajili ya Lissa, mwangalie Mungu, mlinde mwanangu, mwepushe na marafiki wabaya,n.k huo ni mfano tu, hebu Mzazi mwenzangu, jaribu kufanya hivyo
kuanzia sasa kila mwezi unapeleka sadaka kwa Mungu kwa ajili ya watoto wako, na kila siku usiku unapotaka kulala unatubu na kuwaombea tuone kama hapatakuwa na mabadiliko kwenye tabia za watoto wetu, au la!
Nisiwachoche kwa waraka huu, but najua kwa mzazi makini, umejifunza kitu hapo.
Waslaamu,
Stella