M'masly

6 views
Skip to first unread message

salote...@gmail.com

unread,
Jun 26, 2019, 12:44:19 PM6/26/19
to Udakuzi Mtandaoni

DAR ES SALAAM: Mpenzi wa sasa wa mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Tanasha Donna Oketch ameibua gumzo kufuatia muonekano wake wa sasa unaomuonesha akiwa na dalili zote za kuwa mjamzito. 

 

Hayo yameibuka baada ya hivi karibuni mwanadada huyo raia wa Kenya kutupia picha mtandaoni ambayo iliwafanya wajuvi wa mambo kuikagua vilivyo na kuhitimisha kuwa ni mjamzito.

 

“Kitumbo bado hakijatoka kivile lakini ana kila dalili kwamba amenasa mimba. Ukitaka kujua kwamba kweli ana ujauzito angalia mashavu yake, pua na hata sehemu ya kifuani, unaona kabisa ana kitu tumboni,” alisema Fatuma Kija wa Sinza jijini Dar baada ya kuiona picha hiyo.

 

Aidha, picha hiyo ambayo imesambaa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii, baadhi ya waliokomenti waliishia kumpongeza kwa kukubali kuzaa na Mondi huku wengine wakimtahadharisha kuwa, asipoangalia yatamkuta yaliyowakuta waliomtangulia (Zari na Mobeto).

 

“Anabeba mimba kabla ya ndoa, asubirie kutoswa tu,” alikomenti mdau mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Double J kwenye mtandao wa Instagram.  Mwingine akaandika: “Waoo shemeji langu la nguvu, zaa mama… zaa umzalie Simba, pesa ya kukutunzia ipo.”

 

Huko huko Insta baada ya Diamond kuona watu wakimpongeza mpenzi wake, naye alikomenti kwenye picha hiyo akisema: “Kileee, nakiona kwa mbali (akimaanisha anakiona kibendi kwa mbali). http://mmasly.wordpress.com/



UDAKUZI MTANDAONI

unread,
Jun 26, 2019, 1:43:42 PM6/26/19
to salote...@gmail.com, Udakuzi Mtandaoni
Aiseee ni noma

--
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Udakuzi Mtandaoni" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to udakuzi-mtanda...@googlegroups.com.
To post to this group, send email to udakuzi-...@googlegroups.com.
To view this discussion on the web visit https://groups.google.com/d/msgid/udakuzi-mtandaoni/86d66f37-d6d9-4d82-a537-d0ed158acbe4%40googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
Reply all
Reply to author
Forward
0 new messages